Ndugu yangu. Kuna kitu kinaitwa
Entropy katika hii universe yetu. Kwa kifupi tu ni kwamba hakuna kitu kitakachodumu milele maana tangu kitu tu kinapoanza tayari kinaanza kuelekea katika uharibifu na kutoweka.
Albert Einstein katika mahesabu yake ya mwanzo aliamini katika kitu kinaitwa cosmological constant - yaani kwamba universe ilikuwepo na itaendelea kuwepo na wala haibadiliki. Lakini baadaye Edwin Hubble alionyesha wazi kwamba galaxies zote zilikuwa zinakimbia kwa kasi kuelekea mbali zaidi na hii ilimaanisha kwamba universe yetu inapanuka kwa kasi ya ajabu. Kama inapanuka, maana yake ni kwamba hapo mwanzo basi ilikuwa mahali pamoja katika infinitively small single point. Kumbe hata universe yetu hii tuliyomo nayo ina mwanzo, na kama ina mwanzo basi ina entropy pia.
Baadaye ikaaminika kwamba pengine nyota kama jua letu hili ndizo hudumu milele. Akina Hawking nao majuzi juzi hapa wakaonyesha kuwa siyo kweli kwa sababu kumbe nazo zikiishiwa Hydrogen na Helium ya kuwasha hapo katikati basi huweza kuripuka kama supanova na au kunywea na kuwa black holes. Iliaminika kwamba black holes pengine ndizo hudumu milele maana humo nguvu ya uvutano ni kubwa mno kiasi kwamba hakuna kitu kinachoweza kutoka hata kiwe na spidi kali kama ya mwanga. Na katika black holes HAKUNA MUDA na KANUNI ZOTE ZA KISAYANSI TUZIJUAZO HAZIFANYI KAZI. Labda kuna sayansi nyingine na ambayo kanuni zake hatuzijui bado ndiyo inafanya kazi huko; na pengine hata umilele unaweza kupatikana huko.
Baadaye Hawking akaonyesha kwamba hata katika black holes kuna nguvu za mnunurisho (radiation) ambazo huponyoka (Hawking Radiation); na hata black holes nazo kumbe zinaandamwa na entropy.
➡️➡️➡️ Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba katika mtazamo wa kisayansi hakuna kitu kinachodumu milele. Hii maana yake ni kwamba mifumo changamano na tata inayoendesha uhai katika mwili wako ikifikia kikomo chake cha uchakavu (kwa umri, magonjwa, ajali n.k) ni lazima ufe haijalishi kama sijui malaika mtoa roho umemkubalia ama la!
Entropy!
Samahani kwa maelezo marefu 🚶🏿♂️🚶🏿♂️🚶🏿♂️🚶🏿♂️