Nadhani umeelewa vibaya au aliyekuambia amechanganya maelezo.. Ngoja nikupe uhalisia ulivyokuwa. Ni kisa kirefu lakini chakusisimua.
Tetesi zinasema yule mama (na wenzake wote yaani Asharose Migiro na Magufuli) hadi kufikia hatua ile ya fainali ya kinyang'anyiro alibebwa na upepo wa misuguano ya kisiasa, kukatana, kususiana na kukomoana baina ya kambi ya Lowassa na Membe (JK). Na kwakuwa mkutano mkuu ule huenda kwa zaidi ya 90% ulikuwa una wajumbe ambao wagombea wao tayari walikuwa wameshakatwa, ni wazi yoyote kati yao angeweza kubebwa na chochote kile kutoka kwa wale wajumbe.
Hakukuwa na chochote cha kupoteza (sio kwa wagombea wala wajumbe), hakuna haja ya sera, suala ni kuongea chochote kile ili kwenda na upepo wa kisiasa uliopandikizwa vichwani mwa wajumbe. Unaweza kuwa upepo wa kidini, kikabila, kikanda au kikundi. Kijinsia, Mama akaona upepo wa kikundi (team Lowassa) ulikuwa na nguvu zaidi na umebeba mwelekeo wa ushindi, hapo hapo akaswitch na kutambaa nao, na kwa ile kauli yake ya kusema anamuunga mkono Lowassa ilipokelewa kwa shangwe, nderemo na vifijo ukumbi mzima hii inatoa picha huenda kura zilitosha lakini wahuni ndani ya mfumo wakageuza matokeo kwa sababu walijua wazi mama hataweza kutoshea kuongoza hii nchi.