Kwa sie tunaopenda burudani ya muziki wa nyumbani...uchambuzji wako umegusa karibu maswali yote niliyokua najiulizda.
Kuna tetesi nilizisikia japo sina ukweli kwamba alimuoa mdada mmoja nae alikua msanii (bethy??..sina uhakika) ila anakijungu na viuno vya kutosha. Baada ya ndoa ni kama alitangaza kuachana na muziki...sina uhakika pia.
Kuhusu kutumika ktk kampeni...kwa kiasi kikubwa nakubaliana na mtazamo wako.
Tofauti ya yeye na wasanii wengine ni kwamba wimbo wake uliovuma sana hadi Mzee Sita akasema ana cd yake (wimbo wa pi..pi..pi..pi) ulikua uko juu sana nadhani kuliko wasanii wote, alipotumia wimbo huo kuweka vionjo vya politik na kuonekana kama remix....hapo ndipo alipotuondoa wengi kwy anga zake maana remix mara nyingi inavuma kuliko ule wa mwanzo....
sasa ukiangalia maudhui ya kutoka mapenzi kuja ccm...ni kama kuongezea mafuta badala ya maji ili ugali uive...akatupoteza wengi.....namuimbiaje switiii vesi za ccm??
Wenzie japo waligeuza mashairi lkn remix zao hazikuvuna na kuwakera mashabiki....sikusikia Dangote kubadirisha vesi za mbagala kuweka ccm au Dar mpaka Moro kuwa nambari wani.
Kiujumla nyimbo zake dogo zilikua kali sana...mpaka leo hazipiti siku 3 bila kusikiliza nyimbo zake chache kama...Si mimi, Bado Umenuna etc.
Pole zake sie sasahivi tuko busy na Dangote - Ntampata wapi, bado ananijia ndotoni, haki ya Mungu sio masiharaa.....
Labda alishindwa kutofautisha kati ya eksi(mkasi-kuanguka) na kuzidisha (kuzidi kupaa). Wala tatizo sio nyota ila kujumlisha na Msalaba yeye kamiksiiii...