Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sie tunaopenda burudani ya muziki wa nyumbani...uchambuzji wako umegusa karibu maswali yote niliyokua najiulizda.
Kuna tetesi nilizisikia japo sina ukweli kwamba alimuoa mdada mmoja nae alikua msanii (bethy??..sina uhakika) ila anakijungu na viuno vya kutosha. Baada ya ndoa ni kama alitangaza kuachana na muziki...sina uhakika pia.
Kuhusu kutumika ktk kampeni...kwa kiasi kikubwa nakubaliana na mtazamo wako.
Tofauti ya yeye na wasanii wengine ni kwamba wimbo wake uliovuma sana hadi Mzee Sita akasema ana cd yake (wimbo wa pi..pi..pi..pi) ulikua uko juu sana nadhani kuliko wasanii wote, alipotumia wimbo huo kuweka vionjo vya politik na kuonekana kama remix....hapo ndipo alipotuondoa wengi kwy anga zake maana remix mara nyingi inavuma kuliko ule wa mwanzo....
sasa ukiangalia maudhui ya kutoka mapenzi kuja ccm...ni kama kuongezea mafuta badala ya maji ili ugali uive...akatupoteza wengi.....namuimbiaje switiii vesi za ccm??
Wenzie japo waligeuza mashairi lkn remix zao hazikuvuna na kuwakera mashabiki....sikusikia Dangote kubadirisha vesi za mbagala kuweka ccm au Dar mpaka Moro kuwa nambari wani.
Kiujumla nyimbo zake dogo zilikua kali sana...mpaka leo hazipiti siku 3 bila kusikiliza nyimbo zake chache kama...Si mimi, Bado Umenuna etc.
Pole zake sie sasahivi tuko busy na Dangote - Ntampata wapi, bado ananijia ndotoni, haki ya Mungu sio masiharaa.....
Labda alishindwa kutofautisha kati ya eksi(mkasi-kuanguka) na kuzidisha (kuzidi kupaa). Wala tatizo sio nyota ila kujumlisha na Msalaba yeye kamiksiiii...
Alienda kwa misifa kivipi mkuu? Mbona alichokifanya yeye ndicho wasanii wote walifanya? Nyimbo zote za wasanii zilibadilishwa mashairi yake yakawa ni ya kupigia kampeni. Ulipata nafasi ya kuzisikia nyimbo za temba na chege (mambo bado / mkono mmoja), mwasiti (hao), Diamond (Mbagala) na kadhalika.
Au ulitaka kumaanisha nini ndugu? Kipi alifanya extra hadi akakuboa?
kuna ukweli mkubwa uyasemayoWasanii Wote Wa Bongo Waliopata Kuoa Wamepotea Kimziki Kwasababu Ya Majukumu Na Mambo Ya Ujinga Kuacha
Hivi kwani kondom ikishatumika inaweza kujirudisha kwenye paketi yake?Huyo kijana alifanya kosa kubwa sana kwenye maisha yake kujiingiza kwenye siasa za ccm. Bila shaka alikuwa na matumaini makubwa kwamba ccm ingemsaidia kutoka zaidi.huyu ni kijana aliye na kipaji cha hali ya juu na alitumika kisiasa na chàma cha mapinduzi wakati wa kampeni za mwaka 2010. Tangu wakati huo hajatoa hata wimbo mmoja,kulikoni jamani?kapewa nini kilichofanya ubongo wake ukaganda?
huyu ni kijana aliye na kipaji cha hali ya juu na alitumika kisiasa na chàma cha mapinduzi wakati wa kampeni za mwaka 2010. Tangu wakati huo hajatoa hata wimbo mmoja,kulikoni jamani?kapewa nini kilichofanya ubongo wake ukaganda?
sio kwamba hatoi nyimbo anatoa ila hazipati airplay hata kwa ccm wenzie clouds and co wamemtema wamemsusa hata kutafutwa hatafutwi kipindi kile nilikua na kanda yake moja nyumbani albam ya bembeleza
Kama ni kweli, naanza kuuona mwisho wa Mr. Project