The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Hakuna uhusiano na hata Biblia hakuna mahali imesema mwafrika kalaaniwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je aliyechungulia utupu wa Baba ake ni nani?Hakuna uhusiano na hata Biblia hakuna mahali imesema mwafrika kalaaniwa
Je aliyechungulia utupu wa Baba ake ni nani?
OkayZa muda huu Wana JF,
Sii kweli kuwa mtu mweusi alipata laana kwa kumchungulia babaake. Hizo hadithi huwa mnazitoa wapi? Ndani ya biblia? Je, wafahamu chanzo cha biblia? Kama haujui, Tafadhali nakuomba fanya utafiti mdogo bila ya kuegemea dini yoyote. Fatilia watafiti wa mambo Kale, hasa wale waliochimbua makazi ya kale kule Mesopotamia au Summer, kwa sasa ni Iraqi na sehemu za Iran. Huko ndiko mambo yalikoanzia, biblia imechukuwa sehemu za simulizi toka kwa Wa Sumerians, wakayaandika na kuongeza interest zao, halafu wewe ukamezeshwa hivyo hivyo bila kutafuna. Hebu cheua kwanza ili uanze kutafuna upya ili ukiona kitamu na ukweli, unaweza ukameza sasa, la kama ni shubiri, basi waweza tema.
Mtu mweusi alipata ujuzi mapema sana baada ya dunia kufikiwa, na aliambatana na miungu yake hadi kujenga ma piramids, pia walisafiri hao miungu yake hadi America ya kusini na kuanzisha ustaarabu huko na wengine wakatokea kama Aztecs.
Toka nje ya box/chupa uuone ukweli wa hii dunia. Unavyoiona sivyo ilivyo. Kwa nini hujiulizi hawa wazungu walikuwa na wanaendelea kutumia matrilioni ya fedha kufuatilia mambo kale?
Wewe hapo ulipo, nikikuuliza hata chimbuko la ukoo, kabila lako, lilitoka wapi, nini na nani, hakika utabaki mdomo wazi. Kisa, sii kuwa una laana, la hasha, ni kuwa hujishughulishi. Jirani yako hapo ni tajiri, ana magari na ghorofa za kutosha, lakini wewe hauna. Nikikuuliza sababu ni nini. Utatoa jibu rahisi kuwa ni Mungu kakuumba hivyo. Sii kweli. Ni uvivu wako, akili yako imebweteka, haujishughulishi, ama uu mbinafsi na umejishusha/umejidharau au kuridhika for nothing!
Haya funguka sasa
kama kuna kosa alilifanya Mungu (kama yupo anyway) ni kumuumba mtu mweusiJe ni kweli mtu mweusi alipata laana baada ya kuchungulia utupu wa Baba yake ?
Ukweli ni upi maana duniani kote mtu mweusi anachapika hatari.