Je, ni kweli Mtumishi wa KKKT Kijitonyama kadokoa sadaka madhabahuni?

Je, ni kweli Mtumishi wa KKKT Kijitonyama kadokoa sadaka madhabahuni?

Acha uzushi kama hujui ni afadhali ukanyamaza.....hilo ni sanduku la Maombi na limeandikwa kabisa SANDUKU LA MAOMBI...sasa hayo ni mambo na siri za watu zimeandikwa humo kwenye hizo bahasha na yakimaliza kuombewa huwa yanachomwa moto chini ya uangalizi wa Mtu anayeweza kutunza siri..

Kwa hiyo kuna nyingine unakuta zinachanganyika na sadaka kwa hiyo nilazima zitolewe kama wakati wa maombi ikigundulika kuna Fedha ili zisije kuchomwa na Karatasi za maombi baada ya kuombewa..
Hata ukitumia akili ya kawaida utaona kuwa huo ni uzushi,huyo mchungaji anajua kuwa hapo kuna camera na pia yuko na watu wengine hapo atawezaje kujilipua kiasi hicho? Huu uzi umeletwa mahsusi kuzidi kuchochea mgogoro KKKT na mods nao wamekubali kushiriki kampeni hii chafu. Mbona zikianzishwa nyuzi za uzushi zikiihusu CCM faster tu zinafutwa na mhusika kupigwa ban.
 
Waafrika tutachezewa sana na viongozi wa hizi dini za kuletewa na maboti
 
Moderators tafadhalini futeni huu uzushi wa kulichafua Kanisa na watumishi wake. Video iliyoambatishwa kwenye uzi huu inaonyesha wazi kuwa lile ni sanduku la maombi na siyo sadaka,na pia inaonyesha wazi mchungaji amefungua bahasha na kutoa ile karatasi ndani ya bahasha na kuirudisha ndani ya sanduku. JF inaanza kupoteza mwelekeo kwa kuonekana inatumika kuchafua watu na taasisi.
Mwambie arudishe pesa ya watu kwanza
 
Mama mwenye nguo nyeusi na miwani kapita na ten arudishe sadaka.
 
Acha uzushi kama hujui ni afadhali ukanyamaza.....hilo ni sanduku la Maombi na limeandikwa kabisa SANDUKU LA MAOMBI...sasa hayo ni mambo na siri za watu zimeandikwa humo kwenye hizo bahasha na yakimaliza kuombewa huwa yanachomwa moto chini ya uangalizi wa Mtu anayeweza kutunza siri..

Kwa hiyo kuna nyingine unakuta zinachanganyika na sadaka kwa hiyo nilazima zitolewe kama wakati wa maombi ikigundulika kuna Fedha ili zisije kuchomwa na Karatasi za maombi baada ya kuombewa..
mkuu usipende ku romantisize kila kitu kwa nini asisubiri maombi yaishe kisha wachambue bahasha zenye pesa ya sadaka wazitenge? kukagua bahasha moja na kuondoka na pesa unaona ni sahihi?
 
SAsa mbona bahasha zingine hazijafunguliwa,
Bahasha za kuchoma huwa zote zinafunguliwa.
Pili kwann aifinye hela mkononi kwa siri? Mwambie huyo mtumishi arudishe hio ten.
Hawa ndio uwavunja moyo watu kutoa
 
mkuu usipende ku romantisize kila kitu kwa nini asisubiri maombi yaishe kisha wachambue bahasha zenye pesa ya sadaka wazitenge? kukagua bahasha moja na kuondoka na pesa unaona ni sahihi?
Hata ukiangalia dhamira unaona kabisa nia ya kukwapua ipo
 
Wizi ni roho na sio umasikini.
Pana mzee ana v8 tena la kwake alionekana Bank akipita na kiswaswadu yaani kitorch cha elf 30 bank mteja asisahau simu wakati anajaza formu.
Unaiba torch wakati unamiliki iphone.
Thus mwizi akikosa cha kuiba ujiibia mwenyewe hapa ishu ni spirit na sio uchumi.
 
Kuna Video nimeona sehemu, ambayo watu wanasema Mtumishi huyu wa Mungu kadokoa Sadaka Madhabahuni mwa Bwana.

Mimi naiangalia mara mbilimbili siamini macho yangu. Nimeamua kupost hapa ili wataalamu wa Video wasaidie kudadavua.

Je, huyu Kadokoa sadaka? Kama kadokoa sadaka, karma itamuacha salama?Camera za Kanisa ndizo zimemdaka au ni miujiza?

Karibuni.
View attachment 2500547

Pia soma Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
Hivi kumbe kimaro ni mwanamke!!!
mona hapo mtumishi anayechukua pesa kwenye bahasha ni mwanamke aliyevaa miwani
au macho yangu yameona vibaya?
 
Hata ukiangalia dhamira unaona kabisa nia ya kukwapua ipo
kama ndio utaratibu wao huo wa kkkt basi kuna shida mahali maana hata makanisa haya ya kilokole ambayo nabii ndio top wa kila kitu hawawezi kufanya kitu cha hivi madhabahuni
 
Msipende kushadadia msivyo vijua, hizo sio sadaka, hayo ni maombi, na unaona kabisa pameandikwa Sanduku la Maombi. Na wakati wa kuyakusanya huwa wanaambiwa kabisa msiweke sadaka. Hizo ni bahasha, ndani yake kuna maombi ambayo watu wameyaandika, sasa ingawa wanatangaziwa wasiweke Sadaka, bado kuna watu huwa wanaweka, so ni kawaida viongozi huwa wanaangalia bahasha kama kuna hela, na kuiweka kwenye sanduku lingine la Sadaka ambalo hapo halionekani, so huyo mchungaji alichofanya ni kuhamisha kuipeleka sehemu husika.
Kwanini sasa hilo zoezi la kuhakiki bahasha zenye hela limefanyika kwa hiyo hahasha moja tu?
 
Moderators tafadhalini futeni huu uzushi wa kulichafua Kanisa na watumishi wake. Video iliyoambatishwa kwenye uzi huu inaonyesha wazi kuwa lile ni sanduku la maombi na siyo sadaka,na pia inaonyesha wazi mchungaji amefungua bahasha na kutoa ile karatasi ndani ya bahasha na kuirudisha ndani ya sanduku. JF inaanza kupoteza mwelekeo kwa kuonekana inatumika kuchafua watu na taasisi.
Kumbe nawe ni taahira?

Hujaona kwamba ametoa karatasi ya maombi ila akaondoka na hela iliyokuwa imewekwa pamoja na karatasi ya maombi?
 
Kula mchicha ni bei nafuu hizo ni bahasha za maombi huyo mwanamke katoa kikaratasi na sio pesa
Angalia vizuri tena!

Katoa karatasi ya maombi na hela, vyote vilikuwa kwenye bahasha moja ameondoka na hela ila karatasi ameiacha
 
😁😁😁👇
 
Huo mfumo wa kuombea sadaka sio wa ki KKKT, labda ndio maana Kimaro aliondolewa. Sadaka unashikashika za nini? Maombi unaandika kwenye barua? Mi najua watu wanatakiwa watoe sadaka Ila wainuizie kwa Imani mioyoni mwao Yale wanayotaka Mungu awatendee
Aliondolewa kisa boksi la maombi?
Hivi barua ilitolewa kusema sababu na kanisa lenu la KKKT?

Imesemwa tayari yupo bado anarudi baada ya likizo hiyo kuendelea kama Mchungaji Kiongozi.
 
Back
Top Bottom