uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Swali la kujiuliza,ni je huyo mama amejuaje kwamba hiyo bahasha pekee ndiyo ina sadaka?Msipende kushadadia msivyo vijua, hizo sio sadaka, hayo ni maombi, na unaona kabisa pameandikwa Sanduku la Maombi. Na wakati wa kuyakusanya huwa wanaambiwa kabisa msiweke sadaka. Hizo ni bahasha, ndani yake kuna maombi ambayo watu wameyaandika, sasa ingawa wanatangaziwa wasiweke Sadaka, bado kuna watu huwa wanaweka, so ni kawaida viongozi huwa wanaangalia bahasha kama kuna hela, na kuiweka kwenye sanduku lingine la Sadaka ambalo hapo halionekani, so huyo mchungaji alichofanya ni kuhamisha kuipeleka sehemu husika.
Mbona kulikuwemo bahasha nyingi,akachagua moja.
Na nijuavyo mimi kanisa lina wazee wanaojihusisha na sadaka. Iweje mtumishi aliyetakiwa kujihusisha na maombi
kwa wakati ule ajihusishe na sadaka ilihali kuna wahudumu wanaohusika na sadaka?
Sadaka zinazochanganywa na maombi kwenye bahasha,ikibidi zinatolewa
mara ya maombi kuombewa,na wahudumu wale wanaohusika kuchoma hayo maombi
na si pale madhabahuni. Hata kama huyo mtumishi hana nia mbaya lakini kuna la kujifunza
ajirekebishe. Kazi ya sadaka awaachie wazee wa kanisa