Je ni kweli mwanaume anatakiwa kumzidi mwanamke vitu hivi ili mahusiano yadumu?

Nomadiq

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
8,572
Reaction score
22,926
Wasalaam wakuu
Kuna hili jambo nimelisikia kwa muda sasa kuwa ili mwanamke amtii mwanaume kwenye mahusiano; iwe ni urafiki wa mwanzo,uchumba ama ndoa inabidi mwanaume amzidi mwanamke hivi vitu;-

  • UMRI
  • PESA
  • ELIMU/AKILI
 
Sio kweli, mimi baba yangu kamzidi mama kila kitu Urefu, pesa, elimu, muonekano n.k ila tokea tunakua ilikua kila siku mama ana chokochoko na ubabe mwingi.

Issue huwa malezi tu sio mpaka awe na pesa otherwise wanawake wa uswahilini ndio wangekua wastaarabu sana maana hata buku ya mchezo kwa siku tu inawashinda.
 
Lakini kwa namna unavyoona faza kumzidi mama si ilisaidia mahusiano kudumu mda mrefu ingekua hajamzidi huenda ingeenda tofauti!
 
Hizo chokochoko na ubabe anamletea baba yenu? Bila shaka mshua alikua anammudu bi mkubwa sema anapuuza tu kwa sababu anaelewa chaotic nature ya wanawake.
 
Ni kujitambua tu, unaweza kumzidi mwanamke kila kitu, ila ukiwa bogus utaendeshwa, utagombanishwa na marafiki na ndugu zako wote, mi naona kit kikubwa zaidi ni kujitambua na kutokuwa mshamba wa mapenzi.

Kuna watu ni makini, na kuna mijitu ni bogus kwa wanawake.
 
Kuna radha flani hivi inapatikana kama mwanaume utamzidi mwanamke wako hivyo vitu. Ila pia kuna wengine wanazidiwa na wanawake zao ila maisha yanasonga vizuri
Kabisa hata mimi nilitegemea jibu kama hili maana mwanamke kumzidi mwanaume hata kimojawapo ni changamoto kubwa sana ya kupelekea mahusiano kuyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…