Je, ni kweli Tanzania ni nchi ya wajinga?!

Je, ni kweli Tanzania ni nchi ya wajinga?!

Tanzania kwa siku za hivi karibuni imedhihirisha kile ambacho Naibu waziri wa Afya Dk. Mollel aliwahi kusema; kwamba Tanzania wajinga ni wengi.

Kwa bahati mbaya sana hata viongozi wakubwa na wasaidizi wa Rais, nachelea kusema kwamba na wao wamejidhihirisha kwamba ni wajinga. Hii pamoja na mambo mengine, imekuja baada ya Mkataba wa Kimangungo-mangungo wa DP World.

Hivi kama kweli siyo ujinga na umbumbumbu, utaingia mkataba ambao hauna kikomo na wenye masharti ya kuondoa uhuru wa nchi na wananchi wake katika kutumia rasilimali walizojaaliwa na Mwenexi Mungu?!

Hivi kama kweli hatuongozwi na wajinga, mtatuleteaje mkataba ambao tayari Rais alishasaini yapata mwaka mzima huko nyuma, eti tuujadili (kupitia wawakilishi wetu wabunge ambao pia wamedhirisha ni wajinga wa kutupwa!?)? Kama siyo ujinga huu, nini basi??

Viongozi wengi wa Tanzania ni waoga!
Wengi wako kwa ajili ya maslahi ya matumbo yao wenyewe na familia zao.
Na huwezi kuutenganisha uoga na ujinga. Wengi wanajidhalilisha kwa kutetea mambo ya kijinga ili tu waendelee kuwepo kwenye nafasi zao au wapewe promotion!
Hivi kweli hadi lini tutaendelea kuongozwa na wajinga wa aina hii?!

Mwisho, japo siyo kwa umuhimu; mjinga huwa hapendi kukosolewa, maana utashangaa baada ya ujumbe huu kusomwa na wanajamvi (ambao pia wajinga ni wengi), utashangaa uzi unatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha na kumfuatilia mwandishi badala ya kuhangaika na kuondokana na ujinga!

Hatuwezi kuendelea kushuhudia mambo ya kijinga yakifanywa na viongozi wajinga yakiendelea katika nchi yetu.

Yaani kina Nyerere walifanya juhudi za kututoa utumwani, halafu wajinga wachache wanataka kuturidisha huko tena kwa bei chee kabisa; HAIWEZEKANI.

Amandraaaaaaaa..................

Aluta continua.
Majizi ya bandari ndio yanapinga mkataba wa DP W
 
We ndo mjinga.
Na kama ushaona hii ni nchi ya wajinga na wewe ni Mtz basi huwezi kujitoa kwenye ujinga huo unless uhame nchi
Natafuta nchi ya kuhamia.
Inshallah, nitahama siku moja.
 
Wajinga ni wale wanaochezeshwa Ngoma na "ma spin Doctors"wa mitandaoni kama wewe...

Kwanza ilianza ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani...Kamala Harris...
Watu walichezeshwa Ngoma humu Jf na mitandao yote kuwa Yule mama anakuja kusimamia watanzania wakubali mapenzi ya jinsia moja...
Hadi maandamano uchwara yakafanyika...bonge moja la kampeni Hadi Viongozi wa dini ambazo huko Ulaya ndo main supporter wa hizo ndoa hapa nchini wakajifanya wao ndo wako mbele kuongea kitu hata hao Wamarekani hakiko kwenye agenda zao walipokuja hapa......

Sasa limekuja la Bandari..."ma spin Doctors"kazi moja tu...
Haipiti dakika 20 threads tatu mpya zote Bandari na kutukana na kuponda serikali ....

Wajinga washasahau Ngoma waliyo chezeshwa wakati wa ziara ya Kamala Harris....wapo wanajazwa hofu na kuambiwa "waarabu wamepewa" bandari milele...🤣🤣🤣🤣🤣

Kweli hii nchi ina wajinga Wengi sana
Ulikuwa AGAINST, sasa upo FOR so just learn to live with it.
In fact, those supporting the current regime are the most halfwit persons I've ever seen!
 
Ulikuwa AGAINST, sasa upo FOR so just learn to live with it.
In fact, those supporting the current government are the most halfwit persons I've ever seen!
"Nchi hii wajinga ni wengi sana"! By . H.E Dr. Mollel.
 
Nchi imejaa vilaza na waoga hii ,mbunge mzima anakuja hadharani kukiri alienda Dubai Ila hajui alienda kufanyeje ,Nina Imani ng'ombe nnaowafuga wangeapishwa ,wanaiongoza nchi ya keyboard warriors kiulaini Sana , vilaza tusio na spine
 
Sio nchi ya wajinga ila ni nchi ya watu wasiojijal na wepesi kusahau na kusamehe na weng hawajitambui ila sio wajinga ni jinsi ya maisha waliochagua kuishi ndo inakuchanganya

Sasa kama hujali, hujitambui, mwepesi kusahau mambo muhimu katika maisha yako hiyo si ndio tafsiri ya mjinga.
 
Nchi imejaa vilaza na waoga hii ,mbunge mzima anakuja hadharani kukiri alienda Dubai Ila hajui alienda kufanyeje ,Nina Imani ng'ombe nnaowafuga wangeapishwa ,wanaiongoza nchi ya keyboard warriors kiulaini Sana , vilaza tusio na spine
System ndo imetufanya hivyo ndugu yangu, tutafanyaje sasa?!
Labda iko siku Mungu atatuinulia kina "Musa" wetu watakaotutoa katika nchi ya utumwa wa ujinga hadi nchi ya asali na maziwa. Nchi ambayo raia wote wananufaika na raslimali za nchi yao kwa usawa.
Inshallah.
 
akili zao zipo kwenye kinyeo na mdomoni.
kile kitabu cha abunuwasi, mfalme jua,nchi ya kusadikika kilikuwa kinaongelea tanzania
 
Tz sio wajinga ila tunaongozwa na wajinga swali langu ilikuwaje wajinga wakawa vipngozi
Ukiona kiongozi wenu ni mjinga, popote pale, maana yake ni kuwa mmechagua mmoja wenu(wajinga) kuwaongoza.

Having said that, kwa hili taifa, huenda....nasema huenda kabisa, from top-botttom, ni wale wale tu!!
 
Naunga mkono hoja hili...hongo inatolewa bungeni waazi tukiona ya mitungi ya gas na tupo tu ,uoga mwingi bongo ...nlikuwa sehemu kkoo natoa point ,jamaa wanasema ongea polepole ,cid wasikuskie ....wajinga ndo sisi
 
System ndo imetufanya hivyo ndugu yangu, tutafanyaje sasa?!
Labda iko siku Mungu atatuinulia kina "Musa" wetu watakaotutoa katika nchi ya utumwa wa ujinga hadi nchi ya asali na maziwa. Nchi ambayo raia wote wananufaika na raslimali za nchi yao kwa usawa.
Inshallah.
System ingolewe ,viongozi wamekuwa jeuri Sana ,mtaani vijana ambao wangechangia ujenzi wa nchi wanashinda vijiweni kucheza bao na kucheki zari ,zuchu au mondi kafanyeje , daah bongo sijui tuendako
 
akili zao zipo kwenye kinyeo na mdomoni.
kile kitabu cha abunuwasi, mfalme jua,nchi ya kusadikika kilikuwa kinaongelea tanzania
Umenikumbusha mbali sana Mkuu.
Tatizo mjinga hataki kuambiwa ukweli.
Anataka sifa za kijinga kijinga zile ambazo hata mvua ikinyesha, anashukuriwa yeye kwa kuleta mvua.
Wakosoaji wa hawa viongozi wajinga wajinga, mara nyingi huishia jera au kuuawa.
Ndiyo maana Shaaban Robert, akaamua kuandika vitabu vyake kwa lugha ngumu, isiyoeleweka kwa urahisi.
Nakumbuka pia hata kile kisa cha Mfalme mwenye masikio marefu kama ya punda!
Mwamba kinyozi alipoona ameshindwa kukaa na hiyo siri, akaenda kuchimba shimo na kuliambia shimo ukweli!
Japo, hilo shimo lilikuja kunsaliti baadaye maana liliruhusu mti uote, ambao baadaye ulikuja kufichua siri ya mfalame!
Hawa waandishi wa vitabu wa zamani walikuwa na akili sana..
 
Ukiona kiongozi wenu ni mjinga, popote pale, maana yake ni kuwa mmechagua mmoja wenu(wajinga) kuwaongoza.

Having said that, kwa hili taifa, huenda....nasema huenda kabisa, from top-botttom, ni wale wale tu!!
Exactly
 
System ingolewe ,viongozi wamekuwa jeuri Sana ,mtaani vijana ambao wangechangia ujenzi wa nchi wanashinda vijiweni kucheza bao na kucheki zari ,zuchu au mondi kafanyeje , daah bongo sijui tuendako
Aya sasa ndo "mwenye nchi" keshasema kaziba masikio.
 
Attachments

  • 5394886-774acdfc87d3afa8f4140ab87cefff5c.mp4
    1.1 MB
Back
Top Bottom