Je, ni Kweli Tayari Imeshapangwa Portugal achukue World Cup 2026?

Je, ni Kweli Tayari Imeshapangwa Portugal achukue World Cup 2026?

Mjomba Malume

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2025
Posts
927
Reaction score
1,368
Wakuu!

Siku hizi kila nikifungua mtandao nakutana na theory mpya kuhusu Portugal kupangwa kuwa mabingwa na kundi la siri.

Kuna wanaotaja ile scene ya The Simpsons katika “The Cartridge Family” (Season 9, Episode 6) ya mwaka 1997 Mexico vs Portugal wakicheza fainali ya World Cup.

Wengine wanaingiza vita ya Adidas na Nike, wakisema World Cup iliyopita ilikuwa ya Messi, sasa hii ni ya Ronaldo.

Kama kweli kuna watu wamekaa mahali wakapanga Portugal awe bingwa...

👉 Ni kina nani hao?

👉 Na wanafaidika na nini?

👉 Hizi timu nyingine 47 hazijui?

👉 Kama zinajua, mbona zinaendelea kujitutumua, kutumia mabilioni na kupambana uwanjani,wakiumia na mbaya zaidi wametumia miaka 4 ya maandalizi? 😂😂😂

👉 Na kama hawajui kwa nini tusiwasanue?😅

Nauliza tu wakuu...
 
Back
Top Bottom