Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

sio dona tu, yaani kwa ujumla sina urafiki sana na ugali, mara moja moja sana huwa naula kwa ratiba zangu au ugenini.
 
Unga na nguvu za kiume wapi na wapi mbona mnakuwa wajinga
Hahaha nilipokuwa chuo nilikuwa na ma girl friends wengi, rafiki zangu walini sema sana kwamba naweza kupata ukimwi, nilikuwa nawaambia mimi nafanya mazoezi kama wale wanao beba vyuma kutunisha misuri ya kufua na mikono mimu nilikuwa najipa zoezi la mkuyenge. Jamaa walikuwa wanacheka sana. Niliwaambia kila kiungo kinahitaji mazoezi hawakukubaliana na sababu zangu. Nahisi hao ndio wala Dona siku hizi, wanatafuta nguvu za kiume uzeeni.
 
kingine nilichojifunza kupitia huu uzi na nyuzi nyingine za JF ni hawa wasomi wetu uchwara ambao wakisoma uzi wa mtu na kama hajakubaliana na kilichoandikwa badala ya kujibu kwa hoja utakuta anajibu 'mpaka naona kichefu chefu kusoma', mara 'ujinga umeandika; nk.
 
Nimekuwa nikipingana na watu wengi sana kuhusiana na hili swala.....afadhali leo nimeona kuna mtu anawaza kama mimi juu ya hii issue
Kwaujibu wa mtoa mada hasara za sembe zitakuwa katika mazingira yafuatayo..

ikiwa yatasagwa bila kuoshwa jambo ambalo litafanya mahindi yasagwe pamoja na zile madawa ambayo yatakuwa yapo katika layer ya nje ya punje za hindi.

Lakini mimi naomba kumuuliza mtoa mada..

Aliposema kwamba dona linasaidia kupata choo chepesi,jee ina maana kuna vyakula vizuri ambavyo ukila unapata shida ya choo na kuwa kigumu..?
 
Kwaujibu wa mtoa mada hasara za sembe zitakuwa katika mazingira yafuatayo..

ikiwa yatasagwa bila kuoshwa jambo ambalo litafanya mahindi yasagwe pamoja na zile madawa ambayo yatakuwa yapo katika layer ya nje ya punje za hindi.

Lakini mimi naomba kumuuliza mtoa mada..

Aliposema kwamba dona linasaidia kupata choo chepesi,jee ina maana kuna vyakula vizuri ambavyo ukila unapata shida ya choo na kuwa kigumu..?

Lakini pia jee hayo maganda ya nje ya hindi ambayo kazi yake kubwa inayopatikana ni kulainisha kinyesi yanatofauti gani na yale makapi ya ndani ya machungwa ambayo umekiri kwamba nayo yana kazi ya kulainisha kinyesi ama choo?

Kwa hyo hapo huoni kwamba mtu anayekula sembe inabidi afanye kazi ya ziada ya kutafuta kilainisha choo kyliko yule mtu wasembe..?

Lakini pia ikiwa dona lina faida mara dufu ya sembe na ni faida ambazo hazina tatizo wala madhara,jee huoni kama mtu wa dona anapata faida ambazo mtu wa sembe pia anapata na yule mtu wa sembe hapati zile faida ambazo mtu wa dona anapata..?

Niishie hapo kwanza mtoa mada
 
Kwa hyo ukiosha vizuri mahindi ama ukiyatoa shamba moja kwa moja dona haina madhara kabisa mkuu..?
 
We janaa unatumia ujuzi wako kuwadanganya watu panya mwenyewe ana akili sana maana hayo mahindi yeye hula kiini pekee na kuacha hayo masalia mengine.
Ila we kazana na sembe tuu siye tuachie dona
Dona lina sumu kuvu na hilo limethibitishwa na jopo la wataalamu. Tatizo mnaendekeza ubishi kama wanzuki
 
Kiukweli Dona ni chakula cha hovyo sana basi tu, mi sipendi hata kuuona, mtu ukila kidogo tu unashiba siku mbili 🤣
 
Dona lina sumu kuvu na hilo limethibitishwa na jopo la wataalamu. Tatizo mnaendekeza ubishi kama wanzuki
Haya kula tatizo mababu zetu walifungwa minyororo miguuni shingoni na mikononi lakini heri yao maana Leo hii sisi tumefungwa akilini. Hao mababu walikula dona kwa kipindi kirefu mtu hakuwahi kuathiriwa na hizo sumu kuvu ujanja wa wazungu kutuhafifisha tumeupa kipaumbele. Waliweza kufanya kazi hadi uzeeni lakin Leo baada ya kulishwa vitu hafifu sembe n.k kijana akitembea kilometa 1 hoi kulima hata majani yanayozunguka nyumba yake hawezi bora niendelee na ubishi wangu kama wanzuki
 
Ki ujumla Ugali ni chakula kisichofaa mazoea yanatuponza na ndio chanzo cha kudumaa mwili!
Ujiulize kwanini mataifa walioendelea hawali wanalishia mifugo?

True ugali udumaza akili,thus waafrica wamedumaa akili sababu ya ugali.
Ukitaka akili kula ngano
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Dona Salama ni uliloandaa mwenyewe ni Salama kula sembe kuliko dona kama ujajua liliandaliwa vipi.Wafanyabiashara wanaangalia pesa yako sio afya yako ulisaga Bila kusafisha mahindi hivo ni hatari kwako kulishwa sumu kuvu,au sumu ya kuhifadhia mahindi. Hawana muda wa kuosha mahindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…