Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

Da nimekaribia kufika mwishoni but sijamaliza maana nimeona mengi umeyarudia kwa kutumia lugha tofauti,swali langu ni moja kwa nini unga wa sembe uzalishe glucose nyingi kuliko dona huku sembe imetokana na dona??? na katika maelezo yako hujaseme kama kuna virutubisho vyovyote labda vinaongezwa kwenye sembe??
Hilo ni swali zuri sana.

Hata Mimi nilipiga hesabu Kama zako.

Kwamba mahindi ya dona ndio sources ya mahindi ya sembe.

How comes mahindi yaliyopunguzwa baadhi ya virutubisho yakawe bora kuliko yale ya asili.
 
Nianze kwa kumshukuru mtoa mada kwa mada yako nzuri. Niseme tu mimi nimevutiwa na sehemu moja tu kwenye mada yako nayo ni "Sumu kuvu" japo wewe umeiita sumu kuvu (jina siyo sahihi). Mimi binafsi nataka niongezee hapo kwenye sumu kuvu maana ni eneo langu ambalo nimelifanyia utafiti na ninaendelea kulifanyia utafiti.

Sumu kuvu ni Sumu unayozalishwa na fungi aina ya "Aspergillus" fungi hawa imeripotiwa wanavamia sana nafaka wakati wa kuvuna, kusafirisha mazao, wakati wa kuyaongezea thamani mazao na wakati wa kuyahifadhi. Mahindi na karanga ndio mazao mama yanayoonekana kuvamiwa na fungi hawa kwa wepesi ukilingamisha na mazao mengine, kwasababu mada yetu ni ugali naomba nijikite kwenye mahindi zaidi.

Kama nilivyo sema mahindi na karanga ndo mazao mama yanayoshambuliwa na fungi hawa wanaosababisha sumu kuvu kuliko mazao mengine yote, hivyo basi kushambuliwa kwa mahindi kunaweza kupunguza usalama wa ugali pia. Swali la msingi ambalo tunatakiwa kulijua ni sehemu gani ya mahindi ambayo inashambiwa na fungi hawa?

Ukweli ni kwamba ganda la juu la mahindi ndo mhanga wa kwanza wa shambulio hilo, na ndipo sumu kuvu huzalishwa kwa wingi. Kitu pekee cha kuelewa zaid sumu kuvu ni compound zikibahatika kuingia mwilini kwa kiwango kizuri zinaweza kusababisha kansa, na compound (chemikali) hizi hiziodolewi kwa kuosha au kuchemsha au kupika (very stable compound).

Njia moja ya kupungu kadhia hii ni kutoa ganda la juu la mahindi, japo haiondoi tatizo kwa asilimia mia lakini inapunguza tatzo. Kwa matiki hiyo basi Mtu anaye kula dona kwa sana anauwezekano mkubwa wa kupata matitizo yatokanayo na sumu kuvu.

Hitimisho:
"Ugali wa sembe" ni bora kiafya kuliko "Dona", kwasababu tumeona kwakutoa maganda ya juu ya mahindi yaani kukoboa kunapunguza sumu kuvu kwenye mahindi pia ugali.

Mwisho kabisa Dawa zinazotumika kutunza mahindi wakati wa kuyahifadhi au wakati wa kulima siyo chazo cha sumu kuvu kama mtoa mada alivyotaka kusema, bali wadudu (insect) wanaovamia mahindi ndo chazo kikubwa cha sumu kuvu, pili uhifadhi mbaya wa mazao (mahindi) ni chazo kikubwa cha sumu kuvu, kuhifadhi mazao kwa muda mrefu nichazo pia cha sumu hii, kulima mazao kwenye maeneo ya ukame kunaongeza hatari ya mazao kupatwa na sumu hii na kuchelewa kuvuna mazao au kuyavuna mabichi yaweza kuongeza tatizo hili.

Kwakuhitimisha njia pekee ya kupunguza tatizo is la sumu kuvu ni kutumia njia bora za kilimo na uhifadhi mzuri wa mazao baada ya kuvunwa, lakini njia ya kupunguza tatizo hili ni kukoboa mahindi yaani kutumia sembe badala ya dona.

Therefore sembe is better than Dona, nimekubaliana na hoja zako zote za kibaiologia, Mimi ni Mchemia by professional.
 
...wa Dar katika kutetea sembe...

Endelea kushangilia glucose kujazwa mwilini

Endelea pia kushangilia kupata virutubisho kutoka vyakula ambavyo ni artificial

Tuache sisi tuendelee na dona ilimradi tu ni ratified
 
Wewe kuwa alive sio guarantee kwamba ulaji wa dona ni salama.

Anyway endelea kula dona mpaka uwe dona kantree(donor country)ile ya magu
Unaongea usichokijua, ninaandika haya kwa sababu najua na ninajua kuwa najua. hata hivyo usijali endelea kula ukipendacho. Very likely uko kwenye group la elite, the brain washed ones. Ila fahamu kuwa nina kijua chakula kuliko wewe
 
Nianze kwa kumshukuru mtoa mada kwa mada yako nzuri. .........
Therefore sembe is better than Dona, nimekubaliana na hoja zako zote za kibaiologia, Mimi ni Mchemia by professional.
Asante kwa post.
Sijui tumesoma wapi, sijui!!!
Sijui sample size yako ya utafiti kuhusu hiyo "sumu kuvu" ipoje!!!!
Kama kweli mpo serious, na hilo la sumu kuvu, nilitarajia mtakuwa mnaendelsha kampeni kali ya kufa mtu kupiga vita ulaji wa karanga, ambazo ni mostly contaminated with it.

Jibu ni hapana, why?

Ni wazi hoja yako haina mashiko kwa sababu, sumukuvu huzalishwa kwenye chakula ambacho hakijakauka vizuri. Kwa bahati nzuri Tanzania iko ukanda wa tropical ambao una jua saa 24/7.

Soma kazi nzuri ya PhD ilifanywa na Dr.mmoja (sitaji jina lake) wa SUA akiwa chuoni Australia kuhusu sumu kuvu kwenye mahindi. He didn't end up his work with this nonsense conclusion. Msituletee conclusion za akina Trump za majuzi kuwa maziwa ya kopo ni mazuri kuliko ya mama.

Yes that how your conclusion is, mnapata wapi ujasiri wa kusema "mahindi yaliyopunguzwa baadhi ya virutubisho ni bora kuliko yale ya asili. Mlienda shuleni kufanya nini? Even if all members will support this stupidity, I will not, I better stand alone on this. Tukutane uzeeni
 
Unaongea usichokijua, ninaandika haya kwa sababu najua na ninajua kuwa najua. hata hivyo usijali endelea kula ukipendacho. Very likely uko kwenye group la elite, the brain washed ones. Ila fahamu kuwa nina kijua chakula kuliko wewe
Sawa
mjuzi wa chakula kuliko mimi
 
Dona ndio bora kuliko sembe, nyingine ni blah blah tu kwa sababu sembe ni tamu na inavutia kuliko dona.
 
Dona ndio bora kuliko sembe, nyingine ni blah blah tu kwa sababu sembe ni tamu na inavutia kuliko dona.

Dona la kulima mwenyewe na kuandaa mwenyewe na sio hii ya kununua madukani
 
Mjadala...
------------
Sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania inaamini kwamba ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa dona ni bora kuliko ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa sembe! Je! Ni kweli?

Twende Taratibu; wanaoamini kuwa dona ni bora zaidi wanatoa sababu kuu mbili; moja ni kuwa ugali wa dona unamfanya mtu awe na nguvu zaidi, pili una virutubisho zaidi kwa sababu haujakobolewa na hivyo kubaki na kiini chake. Je! Sababu hizo mbili zinatosha kuufaya ugali wa dona kuwa bora zaidi?

Kabla ya kutoa majibu yangu, nieleze kwa ufupi namna mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unavyofanya kazi.

Binadamu anatakiwa kula ili aishi, na ameumbwa kusikia njaa ili 'akumbuke' kula kwa wakati. Mfumo wa fahamu (ubongo, ugwe mgongo na neva za fahamu) ndiwo unaongoza mifumo mingine ya mwiki ukiwemo mfumo wa mmeng'enyo wa chakula...ili mifumo hiyo ifanye kazi kwa ufasaha na kiumbe (binadamu) apate kuishi.

Kuna sababu nyingi zinazomfanya binadamu aanze kusikia njaa...lakini sababu kubwa kuliko zote ni kusinyaa kwa kuta za mfuko wa chakula (tumbo) kunakosababishwa na kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni. Nimesema kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni -sio kutokuwapo kwa chakula, kuna sababu za kusema hivyo.

Mtu anapotia 'kitu' tumboni iwe ni chakula au kitu kinachofanana na chakula kisicho na madhara, kuta za mfuko wa chakula (tumbo) zitavutika (stretch) kwa sababu mfuko huo umeumbwa kutanuka na kusinyaa - mithili ya 'elastiki'. Kutanuka huko husababisha mishipa ya neva za fahamu kupeleka taarifa kwenye mfumo mkuu wa fahamu (ubongo na ugwe mgongo/spinal cord) ili mfumo mkuu uanze kuratibu matukio muhimu ya mmeng'enyo wa chakula huko tumboni.

Moja kati ya matukio hayo ni kupunguza hamu ya kula (au njaa) taratibu hadi pale tumbo linapovutika kwa kiasi cha kutosha na njaa hukoma.

Kumbuka - kinachofanya kuta za mfuko wa chakula zivutike ni 'kitu' kilichopo tumboni, sio lazima iwe chakula. Kwa lugha nyingine - ni kuwa mtu anaweza kusikia ameshiba kwa sababu kuna kitu tumboni...hata kama kitu hicho si chakula.

Ukiyaelewa maelezo haya machache tutakuwa tumevuka hatua ya kwanza katika kutafuta jibu la swali letu; dona ni bora kuliko sembe?

Pointi ya Kwanza: Ingawa Ni kweli ugali wa dona unaweza kumfanya mtu ajisikie ameshiba zaidi kuliko kiasi sawa cha ugali wa sembe, bado haitoshi kusema ugali wa dona ni chakula bora kuliko ugali wa sembe, kwa sababu si kila kinachompa mtu hisia za kushiba ni chakula.

Dona ni nini?
Dona ni jina linalopewa unga usiokobolewa. Pamoja na kwamba unga wa dona unabaki na kiini cha punje ya hindi chenye protini, vilevile unabaki na ganda la nje la punje ya hindi - ganda ambalo huitwa pumba endapo mahindi yatakobolewa.

Sembe ni unga unaotokana na mahindi yaliyosagwa baada ya kukobolewa, na hivyo hauna kiini na maganda ya nje ya punje za hindi (pumba).

Je, Dona ni bora kuliko sembe?
Sehemu kubwa ya unga wa mahindi ni wanga (carbohydrate) aina ya hamirojo (starch). Wakati kiwango cha hamirojo kwenye dona kinafikia 75% na 25% za protini, virutubisho-madini na vitamini, kiwango cha hamirojo kwenye unga wa sembe kinakaribia 90%, na 10% inabaki kuwa ya virutubisho-madini na baadhi ya vitamin na protini kwa kiwango kidogo sana.

Protini iliyopo kwenye kiini cha punje ya hindi ambayo hubaki kwenye unga wa dona ni protini isiyo timilifu kwa sababu imepungukiwa baadhi ya viungo vya lazima vinavyofanya protini iwe timilifu. 'Viungo' hivi huitwa 'amino acids', na vimegawanyika katika makundi makuu mawili - Essentials amino acids (EAA) na Non - essential amino acids (NAA).

Tofauti kubwa ya virutubisho hivi ni kuwa EAA hazitengenezwi ndani ya mwili na hivyo ni lazima zipatikane kutoka nje kwenye vyakula mbalimbali, wakati NAA zinaweza kutengenezwa ndani ya mwili kutokana na virutubisho vya aina nyingine. Protini iliyopo kwenye punje ya hindi haina idadi ya kutosha ya EAA, (ambazo ni lazima zipatikane nje ya mwili).

Virutubisho vingine vilivyomo kwenye dona ni Vitamin B, madini ya chuma, madini ya Calcium, Magnesium, Potash nk, ambavyo vina umuhimu wake mwilini.

Pointi ya pili: Ugali wa dona una kiasi kidogo cha wanga kulinganisha na kiasi kilekile cha ugali wa sembe. Hata hivyo ugali wa dona una virutubisho zaidi ya ugali wa sembe.

Kumbuka, kila aina ya chakula ina kazi zake mwilini. Itoshe kurudia elimu ya sayansi kimu ya darasa la tano hata kama haitoi picha halisi, kwamba Protini hujenga mwili, Wanga (carbohydrate) unasidia mwili kupata nguvu, na Fat & Oil (mafuta) husaidia kudumisha jotoridi la mwili. Muhimu hapa ni hiyo pointi ya -wanga unasaidia mwili kupata nguvu.

Ndio. Vyakula aina ya wanga huanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni kwa nguvu ya 'enzyme' iliyopo kwenye mate (salivary amylase) ambayo huvunjavunja molekyuli zinazounda wanga na kupata aina nyingine ya wanga nyepesi iitwayo Maltose. Zao hilo linapofika tumboni na baadae kwenye utumbo mwembamba huendelea kumeng'enywa kwa nguvu ya enzyme nyingine iitwayo 'Maltase' na kupatikana wanga nyepesi zaidi inayoitwa 'Glucose'. Hiyo glucose ndio inanyonywa na kuingia kwenye mzunguko wa damu na kusambazwa sehemu zote za mwili -na huko hutumika kama malighafi ya kuzalisha nguvu zinazohitajika ili binadamu andelee kuwa hai.

Pointi ya tatu: Glucose, ndiyo malighafi inayohitajika kuzalisha nguvu mwilini, glucose ni zao la wanga - ambao upo kwa wingi zaidi kwenye unga wa sembe kuliko wanga uliyopo kwenye kiasi sawa cha unga wa dona.

Hitimisho
Kwanza, si kweli kwamba ugali wa dona unamfanya mtu apate nguvu kuliko sembe kwa sababu ugali wa sembe una zalisha glucose kwa haraka zaidi na kwa wingi zaidi kuliko dona. Glucose ndio zao la ugali wa mahindi ambalo ndio malighafi ya kwanza inayohitajika kuzalisha nguvu za mwili.

Kinachotokea kwa dona ni kuchelewa kumeng'enywa na kukaa tumboni muda mrefu na hivyo kufanya mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu 'ujue' bado kuna kitu kwenye mfumo wa chakula. Hali hii hufanya mfumo wa fahamu uridhike kwa muda mrefu na mtu kutopata hisia ya njaa.

Kwanini dona linakaa muda mrefu kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula? Ni kwa sababu ya uwepo wa maganda ya punje za hindi (ambayo yangekuwa pumba endapo mahindi yangekobolewa). Maganda haya hutengenezwa kwa aina nyingine ya wanga inayoutwa Cellulose ambayo haiwezi kumeng'enywa mwilini. Mwili wa binadamu hauna enzyme aina ya cellulase inayohitajika kwa ajili ya kumeng'enya Cellulose. Homoni hii hupatikana kwa wanyama aina ya 'ruminants' kama Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo nk.
Hata hivyo kuna faida moja ya 'pumba' zilizopo kwenye dona - nayo ni kupata choo chepesi.

Pili, Dona lina virutubisho vingi kuliko sembe, ingawa faida si ya maana Sana kwa sababu mtu hali ugali wa dona bila kitoweo. Protini iliyopo kwenye mboga kama maharage, samaki/dagaa au nyama ni nyingi mno kiasi cha kufanya protini ya kwenye dona isiwe na maana yoyote. Madini ya chuma, calcium, potash magnesium nk yanapatikana kwenye mboga za majani kwa wingi kiasi kwamba kiwango kilichopo kwenye dona hakina maana. Vitamini zilizopo kwenye matunda zinafanya vitamini za kwenye dona zisiwe na maana. Zaidi, pamoja na kuwa na virutubisho vya ziada, Bado virutubisho hivyo vya ziada vinavyopatikana kwenye dona - si vya kiwango cha kutosha kuusaidia mwili wa binadamu kama hatakula vyakula vingine. Kwahiyo; uwepo wa virutubisho vya ziada kwenye dona si faida ya kujivunia juu ya sembe. Mwili hauwezi kutegemea protini, madini na vitamini zilizopo kwenye dona.

Tatu. Kuhusu sumu kavu. Ingawa hili si suala la ki-baiolojia lakini pengine ndio muhimu kuliko yote niliyoandika. Mahindi mengi huhifadhiwa kwa kupuliziwa madawa ya kuzuia wadudu ili yasiharibike. Ukiacha madawa hayo (kemikali) bado kuna vumbi na vitu vingine vinavyoambatana na mahindi tangu kuvunwa, kupukuchuliwa na kuhifadhiwa. Mashine ya kusaga haiondoi kemikali au vumbi au vitu vingine vilivyogandamana na mahindi, lakini ikiwa mahindi yatakobolewa angalau vitu hivyo vitapungua kwa kiasi kikubwa.

Vipi? Dona ni bora kuliko sembe?

Tazama zile pumba zinazopatikana baada ya kukoboa mahindi, zitazame tena. Unapokula dona unakula pamoja na hizo pumba. Faida yake ni moja - kupata choo bila shida. Lakini matunda yenye nyuzinyuzi/roughages (mfano; maganda ya ndani ya chungwa) mapapai, maji ya kutosha, kushughulisha mwili, vitasaidia kupata choo chepesi.

Ushauri
Hakuna shida kula unga wa dona ikiwa mahindi yametoka shambani na kusagwa mara moja. Lakini ikiwa mahindi yametunzwa kwa muda mrefu na kwa dawa za kuzuia wadudu - ni jambo la kutafakari kuyasaga bila kukoboa. Sumu kavu - vumbi na dawa za kuzuia wadudu waharibifu vinaweza kuleta madhara ya kiafya mwilini. Nirudie tena, faida pekee ya ziada na maana ya dona juu sembe ni kupata choo chepesi.

-Sio kweli kwamba Dona linaleta nguvu kuliko sembe (neno 'nguvu' linaweza kuhutaji ufafanuzi zaidi).

-Ziada ya virutubisho vya dona haina faida ya maana juu ya sembe kwa sababu havitoshi kuunufaisha mwili bila kuongeza kutoka vyakula vingine.

Dona ni bora kuliko sembe?
Amua...
mtoa mada ametupatia elimu nzuri, ukisoma vyema na kutafàkari yaliondikwa kwenye pointi zake, hazina "nguvu ", naona sehemu nyingi "dona ina kiasi kidogo cha wanga..." haujatuambia ni kivipi...
 
Back
Top Bottom