Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

Nadhani hilo andiko la sumu ya kuvu hukulielewa vizuri. Nenda kalisome tena kwa jicho la kitaaluma. sio kilaymen. Kama ungekuwa sahihi, basi mimi ningekuwa marehemu sasa, Maana dozi yangu ya ugali ni aina ya dona
Wewe kuwa alive sio guarantee kwamba ulaji wa dona ni salama.

Anyway endelea kula dona mpaka uwe dona kantree(donor country)ile ya magu
 
Hata kama sivuni mimi,iwe nanunua dukani lakini nayaosha vizuri kwa maji mengi mpaka maji ya kuoshea yanakuwa meupee then nayaanika nasaga bado tuko salama.

Nikila dona yangu na mchicha na samaki mida ya saa 7 basi hapo nakula tena saa2 usiku tena napiga vitunda tunda tuu

Dah basi ww una muda wa kufanya hayo mambo
 
Dah basi ww una muda wa kufanya hayo mambo
Hata wewe huo muda unao.

Kununua mahindi ni dakika 5 tu.

Kuyachambua na kutoa mahindi mabovu tufanye ni 45mins kwa sababu dona halisagwi kilo nyingi nyingi.

Then kuyakosha ni 10mins

Jumla ni lisaa limoja tu.

Kisha unayaanika unafanya mambo mengine.

Ni mda mchache kwa mpenzi wa dona.
 
Hunijui, sikujui. Hiyo habari ya ugumu wa kuelewa ni tusi kwangu. Si ajabu hata umri nakuzidi, please tumia lugha yenye staha. Nina tofautiana sana nawe, kwa sababu mimi nakijua chakula kwa maana ya kukijua. Hapa Tanzania wakisema wapite mbele wanaokijua chakula nitapita. You have been brain washed to hate yourself kwa peremende.
na wewe acha kupaniki, wapi alipokutukana. Kama unajijua una mihemko usiwe unachangia mada humu uwe unasoma tu na ku like
 
Mahitaji ya aina ya chakula anachotakiwa kula mwanadamu inategemea sana aina ya kazi anayofanya.
Kwa hiyo matumizi wa sembe au dona ni 'relative', au unategemeana na aina ya shughuli anazofanya mtu na nyongeza ya vyakula vingine anavyokula pamoja na ugali n.k.
Ugali anaokula kuli wa kubeba magunia na ugali anaotakiwa kula Daktari ni tofauti kwa wingi na ubora.
Ugali anaotakiwa kula mtoto au mgonjwa ukilinganisha na mtu mzima unatofauti kubwa ukilinganisha wingi au ubora.
La msingi hapa katika kulinganisha aina hizi mbili za vyakula si kuangalia 'energy value' bali ni kulinganisha 'nutrition value'.
Energy value ni kipengere ndani ya nutrition value.
Tunapolingalisha hivo vitu viwili ni lazima 'sample' ya mahindi iwe katika ubora wa juu au grade one.
Mahindi yaliyooza au ambayo hayajakauka vizuri au madogo dogo au yameliwa na wadudu hayafai kufanyiwa malinganisho katika ubora.
Pia unga uliosagwa una namna bora za kuhifadhi. Unaweza ukuwa na dona nzuri au sembe nzuri lakini ukahifadhi vibaya na mwisho ya siku ukipika ugali unakuwa mbaya na hiyo nguvu au lishe zaidi usiione.
Kwa lugha rahisi, 'layman language', ugali wa dona una lishe au nutrition value kubwa kuliko sembe pia ugali wa dona una nguvu zaidi kuliko ugali wa sembe.
Ugali wa sembe unafaa zaidi kwa watu wanaofanya kazi za kutumia kichwa zaidi na ugali wa dona unawafaa watu wanaofanya kazi zinazotumia nguvu nyingi (labor intensive).
 
Daah, umepatia sana mkuu.Mi kila mara huwa nabishana na wadau kuhusu sembe, sembe ni chakula bora na salama ukilinganisha na dona.

Dona lina madhara mengi sana mwilini ukilinganisha na hizo faida zake chache.

Vumbi, uchafu na madawa yanayotumika kuhifadhia mahindi ni hatari kwa afya zetu.

Epuka dona, ni hatari kwa afya yako. KULA SEMBE.
Kwa aina yetu ya kilimo na utunzaji wa mahindi dona ina changamoto zake haswa sumukuvu (mycotoxins) inayozalishwa na aina fulani za fangasi lakini pia mabaki ya chemikali za kuhifadhia mazao. Vinginevyo isingekuwa na shida kubwa
 
Sili tena Sembe aiseee..!!
Kama utaamua kula dona nakuomba mahindi yaandae mwenyewe kwa kuchambua yote machafu, yenye dalili ya fangasi na yaliyotoboka alafu yaoshe ndo yawe tayari kusagwa. Vinginevyo unaiweka familia yako kwenye hatari ya sumukuvu
 
Kula dona ni kula sumu na uchafu.
Mi nitaendelea kula sembe na mhogo.
Matunda na Mboga mboga zitanisaidia
Mahindi ukiyaosha na kuanika halafu ukayasaga mwenyewe hiyo sumu na uchafu vitatoka wapi? Ukiwa mchafu ndio utakula uchafu na sumu. Dona ndio mpango mzima
 
Kula papai, pia maybe huo ni ugonjwa nenda hospitali
Basi ujue papai ndo lonaleta choo na sio sembe kama sembe.

Bado sembe ni chakula hatari sana kwa afya ya tumboo.

Hata sembe lenyewe kama hujaliosha linamadhara tuu
 
Mahindi ukiyaosha na kuanika halafu ukayasaga mwenyewe hiyo sumu na uchafu vitatoka wapi? Ukiwa mchafu ndio utakula uchafu na sumu. Dona ndio mpango mzima
Yani ukiangalia hata mtoa mada hyo ndo hoja yake kubwa.

Wakati huo hata hilo sembe kama hukuosha mahindi na kuyasafisha unaweza kusema kwamba lina madhara piaaa
 
Hata nikila papai, kosa nikila sembe hata ukifululiza wali sana Choo napata kigumu, ili nipate choo kizuri nile Dona au viazi vitamu
Sahihi mkuu.hivi vyakula vya ajabu sana yani.
Ukila wali labda ule kidogo sana na mboga iwe nyingi na matunda.

Ila dona bwana ndio habare ya mujini kwa kweli.

Yani mtu anayekula sembe nusu na mtu anayekula dona nusu.basi huyu mtu wa sembe ili amfikie wa dona inabidi atafute machungwa yaliko ale zile nyama za machingwa ili alainishe choo.

Wakati huo mtu wa dona hana haja ya kula machungwa kwa sababu ganda la indi linafaida hizo ambazo zinapatikana kwenye nyama ya chungwa[emoji23][emoji23]
 
Kama utaamua kula dona nakuomba mahindi yaandae mwenyewe kwa kuchambua yote machafu, yenye dalili ya fangasi na yaliyotoboka alafu yaoshe ndo yawe tayari kusagwa. Vinginevyo unaiweka familia yako kwenye hatari ya sumukuvu
Hapo hata yakikaa miaka miwili Ukiyachambua na ukayaloweka kidogo na kuyakosha yakawa masaaaafiiii mzee unaenjoy life fresh.
 
Kwa aina yetu ya kilimo na utunzaji wa mahindi dona ina changamoto zake haswa sumukuvu (mycotoxins) inayozalishwa na aina fulani za fangasi lakini pia mabaki ya chemikali za kuhifadhia mazao. Vinginevyo isingekuwa na shida kubwa
Katika mbegu ya hindi yale mabaki ya kemikali na sumu kuvaa hukaa sehemu gani ya punje ya mhindi..?
 
Basi ujue papai ndo lonaleta choo na sio sembe kama sembe.

Bado sembe ni chakula hatari sana kwa afya ya tumboo.

Hata sembe lenyewe kama hujaliosha linamadhara tuu

Umeanza kusoma comments au umeanza kusoma habari yenyewe? Umeambiwa sembe ni mzuri coz inasagwa haraka tumboni na kutengeneza grocos ambayo inasaidia kuongeza nguvu But dona kutokana na yale makamba kamba yake inachelewa kusagwa ndio maana ukila dona saa saba mpaka saa 12 bado umeshiba
 
Tunashauri kula vyakula visivyozalisha sukari kwa haraka. Sasa kwa mazingira yetu ya afrika mashariki tunataja Dona, au ugali wa Mtama. Wagonjwa wa kisukari ulaya na Amerika hawasauriwi kula Dona kwa sababu sio chakula chao.
Mkuu nakuomba jibu maswali ya watu! Ili tupate somo zaidi
 
Katika mbegu ya hindi yale mabaki ya kemikali na sumu kuvaa hukaa sehemu gani ya punje ya mhindi..?
Asilimia kubwa ya sumu kuvu inakaa kwenye ganda la nje na ukichambua na ya kuyaosha vizuri inapunguza sana sumu kuvu hadi kwa zaidi ya asilimia 80
 
Sahihi mkuu.hivi vyakula vya ajabu sana yani.
Ukila wali labda ule kidogo sana na mboga iwe nyingi na matunda.

Ila dona bwana ndio habare ya mujini kwa kweli.

Yani mtu anayekula sembe nusu na mtu anayekula dona nusu.basi huyu mtu wa sembe ili amfikie wa dona inabidi atafute machungwa yaliko ale zile nyama za machingwa ili alainishe choo.

Wakati huo mtu wa dona hana haja ya kula machungwa kwa sababu ganda la indi linafaida hizo ambazo zinapatikana kwenye nyama ya chungwa[emoji23][emoji23]
Ila pia hizo fibre ziko kwa wingi kwenye matunda, mboga za majani na maharagwe. So kukoboa kuna faida zake kwa usalama wa mahindi (food safety). Kinachopotea wakati wa kukoboa huwa kinafidiwa na vyakula vingine kirahisi tu.
 
Back
Top Bottom