Je, ni kweli Ugali wa Dona ni bora kuliko wa Sembe?

mkuu kwahiyo faida kuu ya dona ni choo kua chepesi
Mjadala...
------------
Sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania inaamini kwamba ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa dona ni bora kuliko ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa sembe! Je! Ni kweli?

Twende Taratibu; wanaoamini kuwa dona ni bora zaidi wanatoa sababu kuu mbili; moja ni kuwa ugali wa dona unamfanya mtu awe na nguvu zaidi, pili una virutubisho zaidi kwa sababu haujakobolewa na hivyo kubaki na kiini chake. Je! Sababu hizo mbili zinatosha kuufaya ugali wa dona kuwa bora zaidi?

Kabla ya kutoa majibu yangu, nieleze kwa ufupi namna mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unavyofanya kazi.

Binadamu anatakiwa kula ili aishi, na ameumbwa kusikia njaa ili 'akumbuke' kula kwa wakati. Mfumo wa fahamu (ubongo, ugwe mgongo na neva za fahamu) ndiwo unaongoza mifumo mingine ya mwiki ukiwemo mfumo wa mmeng'enyo wa chakula...ili mifumo hiyo ifanye kazi kwa ufasaha na kiumbe (binadamu) apate kuishi.

Kuna sababu nyingi zinazomfanya binadamu aanze kusikia njaa...lakini sababu kubwa kuliko zote ni kusinyaa kwa kuta za mfuko wa chakula (tumbo) kunakosababishwa na kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni. Nimesema kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni -sio kutokuwapo kwa chakula, kuna sababu za kusema hivyo.

Mtu anapotia 'kitu' tumboni iwe ni chakula au kitu kinachofanana na chakula kisicho na madhara, kuta za mfuko wa chakula (tumbo) zitavutika (stretch) kwa sababu mfuko huo umeumbwa kutanuka na kusinyaa - mithili ya 'elastiki'. Kutanuka huko husababisha mishipa ya neva za fahamu kupeleka taarifa kwenye mfumo mkuu wa fahamu (ubongo na ugwe mgongo/spinal cord) ili mfumo mkuu uanze kuratibu matukio muhimu ya mmeng'enyo wa chakula huko tumboni.

Moja kati ya matukio hayo ni kupunguza hamu ya kula (au njaa) taratibu hadi pale tumbo linapovutika kwa kiasi cha kutosha na njaa hukoma.

Kumbuka - kinachofanya kuta za mfuko wa chakula zivutike ni 'kitu' kilichopo tumboni, sio lazima iwe chakula. Kwa lugha nyingine - ni kuwa mtu anaweza kusikia ameshiba kwa sababu kuna kitu tumboni...hata kama kitu hicho si chakula.
Ukiyaelewa maelezo haya machache tutakuwa tumevuka hatua ya kwanza katika kutafuta jibu la swali letu; dona ni bora kuliko sembe?

Pointi ya Kwanza: Ingawa Ni kweli ugali wa dona unaweza kumfanya mtu ajisikie ameshiba zaidi kuliko kiasi sawa cha ugali wa sembe, bado haitoshi kusema ugali wa dona ni chakula bora kuliko ugali wa sembe, kwa sababu si kila kinachompa mtu hisia za kushiba ni chakula.

Dona ni nini?
Dona ni jina linalopewa unga usiokobolewa. Pamoja na kwamba unga wa dona unabaki na kiini cha punje ya hindi chenye protini, vilevile unabaki na ganda la nje la punje ya hindi - ganda ambalo huitwa pumba endapo mahindi yatakobolewa.

Sembe ni unga unaotokana na mahindi yaliyosagwa baada ya kukobolewa, na hivyo hauna kiini na maganda ya nje ya punje za hindi (pumba).

Je, Dona ni bora kuliko sembe?

Sehemu kubwa ya unga wa mahindi ni wanga (carbohydrate) aina ya hamirojo (starch). Wakati kiwango cha hamirojo kwenye dona kinafikia 75% na 25% za protini, virutubisho-madini na vitamini, kiwango cha hamirojo kwenye unga wa sembe kinakaribia 90%, na 10% inabaki kuwa ya virutubisho-madini na baadhi ya vitamin na protini kwa kiwango kidogo sana.

Protini iliyopo kwenye kiini cha punje ya hindi ambayo hubaki kwenye unga wa dona ni protini isiyo timilifu kwa sababu imepungukiwa baadhi ya viungo vya lazima vinavyofanya protini iwe timilifu. 'Viungo' hivi huitwa 'amino acids', na vimegawanyika katika makundi makuu mawili - Essentials amino acids (EAA) na Non - essential amino acids (NAA).

Tofauti kubwa ya virutubisho hivi ni kuwa EAA hazitengenezwi ndani ya mwili na hivyo ni lazima zipatikane kutoka nje kwenye vyakula mbalimbali, wakati NAA zinaweza kutengenezwa ndani ya mwili kutokana na virutubisho vya aina nyingine. Protini iliyopo kwenye punje ya hindi haina idadi ya kutosha ya EAA, (ambazo ni lazima zipatikane nje ya mwili).

Virutubisho vingine vilivyomo kwenye dona ni Vitamin B, madini ya chuma, madini ya Calcium, Magnesium, Potash nk, ambavyo vina umuhimu wake mwilini.

Pointi ya pili: Ugali wa dona una kiasi kidogo cha wanga kulinganisha na kiasi kilekile cha ugali wa sembe. Hata hivyo ugali wa dona una virutubisho zaidi ya ugali wa sembe.

Kumbuka, kila aina ya chakula ina kazi zake mwilini. Itoshe kurudia elimu ya sayansi kimu ya darasa la tano hata kama haitoi picha halisi, kwamba Protini hujenga mwili, Wanga (carbohydrate) unasidia mwili kupata nguvu, na Fat & Oil (mafuta) husaidia kudumisha jotoridi la mwili. Muhimu hapa ni hiyo pointi ya -wanga unasaidia mwili kupata nguvu.

Ndio. Vyakula aina ya wanga huanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni kwa nguvu ya 'enzyme' iliyopo kwenye mate (salivary amylase) ambayo huvunjavunja molekyuli zinazounda wanga na kupata aina nyingine ya wanga nyepesi iitwayo Maltose. Zao hilo linapofika tumboni na baadae kwenye utumbo mwembamba huendelea kumeng'enywa kwa nguvu ya enzyme nyingine iitwayo 'Maltase' na kupatikana wanga nyepesi zaidi inayoitwa 'Glucose'. Hiyo glucose ndio inanyonywa na kuingia kwenye mzunguko wa damu na kusambazwa sehemu zote za mwili -na huko hutumika kama malighafi ya kuzalisha nguvu zinazohitajika ili binadamu andelee kuwa hai.

Pointi ya tatu: Glucose, ndiyo malighafi inayohitajika kuzalisha nguvu mwilini, glucose ni zao la wanga - ambao upo kwa wingi zaidi kwenye unga wa sembe kuliko wanga uliyopo kwenye kiasi sawa cha unga wa dona.

Hitimisho
Kwanza, si kweli kwamba ugali wa dona unamfanya mtu apate nguvu kuliko sembe kwa sababu ugali wa sembe una zalisha glucose kwa haraka zaidi na kwa wingi zaidi kuliko dona. Glucose ndio zao la ugali wa mahindi ambalo ndio malighafi ya kwanza inayohitajika kuzalisha nguvu za mwili.
Kinachotokea kwa dona ni kuchelewa kumeng'enywa na kukaa tumboni muda mrefu na hivyo kufanya mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu 'ujue' bado kuna kitu kwenye mfumo wa chakula. Hali hii hufanya mfumo wa fahamu uridhike kwa muda mrefu na mtu kutopata hisia ya njaa...

Kwanini dona linakaa muda mrefu kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula? Ni kwa sababu ya uwepo wa maganda ya punje za hindi (ambayo yangekuwa pumba endapo mahindi yangekobolewa). Maganda haya hutengenezwa kwa aina nyingine ya wanga inayoutwa Cellulose ambayo haiwezi kumeng'enywa mwilini. Mwili wa binadamu hauna enzyme aina ya cellulase inayohitajika kwa ajili ya kumeng'enya Cellulose. Homoni hii hupatikana kwa wanyama aina ya 'ruminants' kama Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo nk.
Hata hivyo kuna faida moja ya 'pumba' zilizopo kwenye dona - nayo ni kupata choo chepesi.

Pili, Dona lina virutubisho vingi kuliko sembe, ingawa faida si ya maana Sana kwa sababu mtu hali ugali wa dona bila kitoweo. Protini iliyopo kwenye mboga kama maharage, samaki/dagaa au nyama ni nyingi mno kiasi cha kufanya protini ya kwenye dona isiwe na maana yoyote. Madini ya chuma, calcium, potash magnesium nk yanapatikana kwenye mboga za majani kwa wingi kiasi kwamba kiwango kilichopo kwenye dona hakina maana. Vitamini zilizopo kwenye matunda zinafanya vitamini za kwenye dona zisiwe na maana. Zaidi, pamoja na kuwa na virutubisho vya ziada, Bado virutubisho hivyo vya ziada vinavyopatikana kwenye dona - si vya kiwango cha kutosha kuusaidia mwili wa binadamu kama hatakula vyakula vingine. Kwahiyo; uwepo wa virutubisho vya ziada kwenye dona si faida ya kujivunia juu ya sembe. Mwili hauwezi kutegemea protini, madini na vitamini zilizopo kwenye dona.

Tatu. Kuhusu sumu kavu. Ingawa hili si suala la ki-baiolojia lakini pengine ndio muhimu kuliko yote niliyoandika. Mahindi mengi huhifadhiwa kwa kupuliziwa madawa ya kuzuia wadudu ili yasiharibike. Ukiacha madawa hayo (kemikali) bado kuna vumbi na vitu vingine vinavyoambatana na mahindi tangu kuvunwa, kupukuchuliwa na kuhifadhiwa. Mashine ya kusaga haiondoi kemikali au vumbi au vitu vingine vilivyogandamana na mahindi, lakini ikiwa mahindi yatakobolewa angalau vitu hivyo vitapungua kwa kiasi kikubwa.

Vipi? Dona ni bora kuliko sembe?

Tazama zile pumba zinazopatikana baada ya kukoboa mahindi, zitazame tena. Unapokula dona unakula pamoja na hizo pumba. Faida yake ni moja - kupata choo bila shida. Lakini matunda yenye nyuzinyuzi/roughages (mfano; maganda ya ndani ya chungwa) mapapai, maji ya kutosha, kushughulisha mwili, vitasaidia kupata choo chepesi.

Ushauri.
Hakuna shida kula unga wa dona ikiwa mahindi yametoka shambani na kusagwa mara moja. Lakini ikiwa mahindi yametunzwa kwa muda mrefu na kwa dawa za kuzuia wadudu - ni jambo la kutafakari kuyasaga bila kukoboa. Sumu kavu - vumbi na dawa za kuzuia wadudu waharibifu vinaweza kuleta madhara ya kiafya mwilini. Nirudie tena, faida pekee ya ziada na maana ya dona juu sembe ni kupata choo chepesi...
-Sio kweli kwamba Dona linaleta nguvu kuliko sembe (neno 'nguvu' linaweza kuhutaji ufafanuzi zaidi)
-Ziada ya virutubisho vya dona haina faida ya maana juu ya sembe kwa sababu havitoshi kuunufaisha mwili bila kuongeza kutoka vyakula vingine...

Dona ni bora kuliko sembe?
Amua...
 
Haya kula tatizo mababu zetu walifungwa minyororo miguuni shingoni na mikononi lakini heri yao maana Leo hii sisi tumefungwa akilini. Hao mababu walikula dona kwa kipindi kirefu mtu hakuwahi kuathiriwa na hizo sumu kuvu ujanja wa wazungu kutuhafifisha tumeupa kipaumbele. Waliweza kufanya kazi hadi uzeeni lakin Leo baada ya kulishwa vitu hafifu sembe n.k kijana akitembea kilometa 1 hoi kulima hata majani yanayozunguka nyumba yake hawezi bora niendelee na ubishi wangu kama wanzuki
Acha kuishi kwa mazoea....
 
utafiti huu wa kisayansi labda ni wa darasa la 5. haiwezekani useme

utafiti huu wa kisayansi labda ni wa darasa la 5. haiwezekani useme maganda ya mahindi ni pumba kama vile maganda hayo hayana kazi, ukiacha virutubisho vilivyomo, ni roughage, husaidia kupata choo na kuondoa tatizo la constipation. Hizo unazoita pumba ndiyo zinanenepesha mifugo, kutagisha kuku, kuongeza maziwa kwa ng'ombe n.k. Huwezi linganisha uchafu sembe na special diet dona.
Kwa hiyo kwa sababu yananenepesha mifugo pia yanaweza kutunenepesha sisi? Mwili wa binadamu hauproduce enzyme ya cellulase kwa ajili ya kudigest hizo pumba tofauti na wanyawa. So kwako wewe kazi ya hizo pumba ni kulainisha choo tu, kazi inayoweza kufanywa na vyakula vya aina nyingine. Mbna watu mnakuwa na vichwa vigumu?
 
Well articulated. Nakupongeza mwandishi. Safi sana.....
 
Kwa hiyo kwa sababu yananenepesha mifugo pia yanaweza kutunenepesha sisi? Mwili wa binadamu hauproduce enzyme ya cellulase kwa ajili ya kudigest hizo pumba tofauti na wanyawa. So kwako wewe kazi ya hizo pumba ni kulainisha choo tu, kazi inayoweza kufanywa na vyakula vya aina nyingine. Mbna watu mnakuwa na vichwa vigumu?
Kwa hyo Ina maana ikilainisha choo hayo makapi yanabakia humo humo tumboni kwa kuwa hayameng'enywi..?
 
Dona ni unga mzuri sana bora hasa kwa wale wanao lialia nguvu za kiume. Ila chakuzingatia ni kupata mahindi yali hifadhiwa bila dawa au yaliotoka shambani moja kwa moja.
mkuu sio tu kuwa umetoka shamban
dona kwa kilimo hichi cha kisasa cha mahindi haufai kiafya
kwanza ukiuhifadhi zaidi ya miezi miwili hata kama umetoka kuvuna shambani ukausaga moja kwa moja
unakuwa mchungu hii ni kutokana na mbegu hizi za kilimo cha kisasa pamoja na mbolea na madawa mengi tangu HINDI likiwa shambani
sipati picha zile mbegu za GMO zingeruhusiwa na tulivyoiamini dona jinsi madhara tungeyapata
DONA ni bora sana tena sana lakini teknolojia na mabadiliko ya kimazingira na sayansi ya kilimo si rafiki tena kwa binadamu binafsi BIBI yangu ameishi miaka 101 amefariki miaka 15 iliyopita katika maisha hakuwai kula sembe yeye ni dona tu
lkn kwa maisha haya ya sasa kula dona hvyo hata 50 hutoboi

hvyo kwa sasa bora sembe tu
 
Daah, umepatia sana mkuu.Mi kila mara huwa nabishana na wadau kuhusu sembe, sembe ni chakula bora na salama ukilinganisha na dona.

Dona lina madhara mengi sana mwilini ukilinganisha na hizo faida zake chache.

Vumbi, uchafu na madawa yanayotumika kuhifadhia mahindi ni hatari kwa afya zetu.

Epuka dona, ni hatari kwa afya yako. KULA SEMBE.
hapana mkuu kwa mahindi sembe ni chakula salama kiasi kwa kilimo hichi cha kisasa
ila kwa Ubora wa virutubisho hitaji mwilini DONA ni bora zaidi
ila kwa mabadiliko haya ya kimazingira na sayansi ya kilimo sembe ni bora
lakini kwa virutubisho Uhitaji wa mwili DONA ni bora zaidi
dhana ya vumbi uchafu haina mashiko
tabu ni viua sumu mbolea na hizi mbegu za kisasa
tafuta documentary flani inaitwa FOOD PRODUTION utaelewa kwann sembe ni salama ila DONA ni bora
hata maji yanaweza kuwa safi lakini yasiwe salama na yanaweza kuwa safi na salama lakini yasiwe bora kiafya
kumbuka ukizungumzia ubora kwenye CHAKURA na AFYA ni kitu ambacho kinakuumiza taratibu matokea ya madhara hutolea hata miaka 3 mpk 10 mbere baada kula chakula ambacho si bora leo hii
hvyo muhimu kuzingatia tunavyokurla leo lakini ukila chakula ama maji ambayo si salama kama tumbo lako ni legelege hakikwepeshi utapata majibu yake tu ndani ya masaa 24
 
Protein zinapatikana kwenye mayai. Nyama. Maziws. Maharagwe.
 
Mjadala...
------------
Sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania inaamini kwamba ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa dona ni bora kuliko ugali unaopikwa kwa kutumia unga wa sembe! Je! Ni kweli?

Twende Taratibu; wanaoamini kuwa dona ni bora zaidi wanatoa sababu kuu mbili; moja ni kuwa ugali wa dona unamfanya mtu awe na nguvu zaidi, pili una virutubisho zaidi kwa sababu haujakobolewa na hivyo kubaki na kiini chake. Je! Sababu hizo mbili zinatosha kuufaya ugali wa dona kuwa bora zaidi?

Kabla ya kutoa majibu yangu, nieleze kwa ufupi namna mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unavyofanya kazi.

Binadamu anatakiwa kula ili aishi, na ameumbwa kusikia njaa ili 'akumbuke' kula kwa wakati. Mfumo wa fahamu (ubongo, ugwe mgongo na neva za fahamu) ndiwo unaongoza mifumo mingine ya mwiki ukiwemo mfumo wa mmeng'enyo wa chakula...ili mifumo hiyo ifanye kazi kwa ufasaha na kiumbe (binadamu) apate kuishi.

Kuna sababu nyingi zinazomfanya binadamu aanze kusikia njaa...lakini sababu kubwa kuliko zote ni kusinyaa kwa kuta za mfuko wa chakula (tumbo) kunakosababishwa na kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni. Nimesema kutokuwapo kwa 'kitu' tumboni -sio kutokuwapo kwa chakula, kuna sababu za kusema hivyo.

Mtu anapotia 'kitu' tumboni iwe ni chakula au kitu kinachofanana na chakula kisicho na madhara, kuta za mfuko wa chakula (tumbo) zitavutika (stretch) kwa sababu mfuko huo umeumbwa kutanuka na kusinyaa - mithili ya 'elastiki'. Kutanuka huko husababisha mishipa ya neva za fahamu kupeleka taarifa kwenye mfumo mkuu wa fahamu (ubongo na ugwe mgongo/spinal cord) ili mfumo mkuu uanze kuratibu matukio muhimu ya mmeng'enyo wa chakula huko tumboni.

Moja kati ya matukio hayo ni kupunguza hamu ya kula (au njaa) taratibu hadi pale tumbo linapovutika kwa kiasi cha kutosha na njaa hukoma.

Kumbuka - kinachofanya kuta za mfuko wa chakula zivutike ni 'kitu' kilichopo tumboni, sio lazima iwe chakula. Kwa lugha nyingine - ni kuwa mtu anaweza kusikia ameshiba kwa sababu kuna kitu tumboni...hata kama kitu hicho si chakula.
Ukiyaelewa maelezo haya machache tutakuwa tumevuka hatua ya kwanza katika kutafuta jibu la swali letu; dona ni bora kuliko sembe?

Pointi ya Kwanza: Ingawa Ni kweli ugali wa dona unaweza kumfanya mtu ajisikie ameshiba zaidi kuliko kiasi sawa cha ugali wa sembe, bado haitoshi kusema ugali wa dona ni chakula bora kuliko ugali wa sembe, kwa sababu si kila kinachompa mtu hisia za kushiba ni chakula.

Dona ni nini?
Dona ni jina linalopewa unga usiokobolewa. Pamoja na kwamba unga wa dona unabaki na kiini cha punje ya hindi chenye protini, vilevile unabaki na ganda la nje la punje ya hindi - ganda ambalo huitwa pumba endapo mahindi yatakobolewa.

Sembe ni unga unaotokana na mahindi yaliyosagwa baada ya kukobolewa, na hivyo hauna kiini na maganda ya nje ya punje za hindi (pumba).

Je, Dona ni bora kuliko sembe?

Sehemu kubwa ya unga wa mahindi ni wanga (carbohydrate) aina ya hamirojo (starch). Wakati kiwango cha hamirojo kwenye dona kinafikia 75% na 25% za protini, virutubisho-madini na vitamini, kiwango cha hamirojo kwenye unga wa sembe kinakaribia 90%, na 10% inabaki kuwa ya virutubisho-madini na baadhi ya vitamin na protini kwa kiwango kidogo sana.

Protini iliyopo kwenye kiini cha punje ya hindi ambayo hubaki kwenye unga wa dona ni protini isiyo timilifu kwa sababu imepungukiwa baadhi ya viungo vya lazima vinavyofanya protini iwe timilifu. 'Viungo' hivi huitwa 'amino acids', na vimegawanyika katika makundi makuu mawili - Essentials amino acids (EAA) na Non - essential amino acids (NAA).

Tofauti kubwa ya virutubisho hivi ni kuwa EAA hazitengenezwi ndani ya mwili na hivyo ni lazima zipatikane kutoka nje kwenye vyakula mbalimbali, wakati NAA zinaweza kutengenezwa ndani ya mwili kutokana na virutubisho vya aina nyingine. Protini iliyopo kwenye punje ya hindi haina idadi ya kutosha ya EAA, (ambazo ni lazima zipatikane nje ya mwili).

Virutubisho vingine vilivyomo kwenye dona ni Vitamin B, madini ya chuma, madini ya Calcium, Magnesium, Potash nk, ambavyo vina umuhimu wake mwilini.

Pointi ya pili: Ugali wa dona una kiasi kidogo cha wanga kulinganisha na kiasi kilekile cha ugali wa sembe. Hata hivyo ugali wa dona una virutubisho zaidi ya ugali wa sembe.

Kumbuka, kila aina ya chakula ina kazi zake mwilini. Itoshe kurudia elimu ya sayansi kimu ya darasa la tano hata kama haitoi picha halisi, kwamba Protini hujenga mwili, Wanga (carbohydrate) unasidia mwili kupata nguvu, na Fat & Oil (mafuta) husaidia kudumisha jotoridi la mwili. Muhimu hapa ni hiyo pointi ya -wanga unasaidia mwili kupata nguvu.

Ndio. Vyakula aina ya wanga huanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni kwa nguvu ya 'enzyme' iliyopo kwenye mate (salivary amylase) ambayo huvunjavunja molekyuli zinazounda wanga na kupata aina nyingine ya wanga nyepesi iitwayo Maltose. Zao hilo linapofika tumboni na baadae kwenye utumbo mwembamba huendelea kumeng'enywa kwa nguvu ya enzyme nyingine iitwayo 'Maltase' na kupatikana wanga nyepesi zaidi inayoitwa 'Glucose'. Hiyo glucose ndio inanyonywa na kuingia kwenye mzunguko wa damu na kusambazwa sehemu zote za mwili -na huko hutumika kama malighafi ya kuzalisha nguvu zinazohitajika ili binadamu andelee kuwa hai.

Pointi ya tatu: Glucose, ndiyo malighafi inayohitajika kuzalisha nguvu mwilini, glucose ni zao la wanga - ambao upo kwa wingi zaidi kwenye unga wa sembe kuliko wanga uliyopo kwenye kiasi sawa cha unga wa dona.

Hitimisho
Kwanza, si kweli kwamba ugali wa dona unamfanya mtu apate nguvu kuliko sembe kwa sababu ugali wa sembe una zalisha glucose kwa haraka zaidi na kwa wingi zaidi kuliko dona. Glucose ndio zao la ugali wa mahindi ambalo ndio malighafi ya kwanza inayohitajika kuzalisha nguvu za mwili.
Kinachotokea kwa dona ni kuchelewa kumeng'enywa na kukaa tumboni muda mrefu na hivyo kufanya mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu 'ujue' bado kuna kitu kwenye mfumo wa chakula. Hali hii hufanya mfumo wa fahamu uridhike kwa muda mrefu na mtu kutopata hisia ya njaa...

Kwanini dona linakaa muda mrefu kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula? Ni kwa sababu ya uwepo wa maganda ya punje za hindi (ambayo yangekuwa pumba endapo mahindi yangekobolewa). Maganda haya hutengenezwa kwa aina nyingine ya wanga inayoutwa Cellulose ambayo haiwezi kumeng'enywa mwilini. Mwili wa binadamu hauna enzyme aina ya cellulase inayohitajika kwa ajili ya kumeng'enya Cellulose. Homoni hii hupatikana kwa wanyama aina ya 'ruminants' kama Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo nk.
Hata hivyo kuna faida moja ya 'pumba' zilizopo kwenye dona - nayo ni kupata choo chepesi.

Pili, Dona lina virutubisho vingi kuliko sembe, ingawa faida si ya maana Sana kwa sababu mtu hali ugali wa dona bila kitoweo. Protini iliyopo kwenye mboga kama maharage, samaki/dagaa au nyama ni nyingi mno kiasi cha kufanya protini ya kwenye dona isiwe na maana yoyote. Madini ya chuma, calcium, potash magnesium nk yanapatikana kwenye mboga za majani kwa wingi kiasi kwamba kiwango kilichopo kwenye dona hakina maana. Vitamini zilizopo kwenye matunda zinafanya vitamini za kwenye dona zisiwe na maana. Zaidi, pamoja na kuwa na virutubisho vya ziada, Bado virutubisho hivyo vya ziada vinavyopatikana kwenye dona - si vya kiwango cha kutosha kuusaidia mwili wa binadamu kama hatakula vyakula vingine. Kwahiyo; uwepo wa virutubisho vya ziada kwenye dona si faida ya kujivunia juu ya sembe. Mwili hauwezi kutegemea protini, madini na vitamini zilizopo kwenye dona.

Tatu. Kuhusu sumu kavu. Ingawa hili si suala la ki-baiolojia lakini pengine ndio muhimu kuliko yote niliyoandika. Mahindi mengi huhifadhiwa kwa kupuliziwa madawa ya kuzuia wadudu ili yasiharibike. Ukiacha madawa hayo (kemikali) bado kuna vumbi na vitu vingine vinavyoambatana na mahindi tangu kuvunwa, kupukuchuliwa na kuhifadhiwa. Mashine ya kusaga haiondoi kemikali au vumbi au vitu vingine vilivyogandamana na mahindi, lakini ikiwa mahindi yatakobolewa angalau vitu hivyo vitapungua kwa kiasi kikubwa.

Vipi? Dona ni bora kuliko sembe?

Tazama zile pumba zinazopatikana baada ya kukoboa mahindi, zitazame tena. Unapokula dona unakula pamoja na hizo pumba. Faida yake ni moja - kupata choo bila shida. Lakini matunda yenye nyuzinyuzi/roughages (mfano; maganda ya ndani ya chungwa) mapapai, maji ya kutosha, kushughulisha mwili, vitasaidia kupata choo chepesi.

Ushauri.
Hakuna shida kula unga wa dona ikiwa mahindi yametoka shambani na kusagwa mara moja. Lakini ikiwa mahindi yametunzwa kwa muda mrefu na kwa dawa za kuzuia wadudu - ni jambo la kutafakari kuyasaga bila kukoboa. Sumu kavu - vumbi na dawa za kuzuia wadudu waharibifu vinaweza kuleta madhara ya kiafya mwilini. Nirudie tena, faida pekee ya ziada na maana ya dona juu sembe ni kupata choo chepesi...
-Sio kweli kwamba Dona linaleta nguvu kuliko sembe (neno 'nguvu' linaweza kuhutaji ufafanuzi zaidi)
-Ziada ya virutubisho vya dona haina faida ya maana juu ya sembe kwa sababu havitoshi kuunufaisha mwili bila kuongeza kutoka vyakula vingine...

Dona ni bora kuliko sembe?
Amua...
in general ugali wa dona ndo una virutubisho
 
Ugali uwe dona ama sembe chakula cha hovyo kabisa...
 
Sawa wacha mi nipite ili kesho nikirudi nitakuwa na cha kusema juu ya hili.
 
Kwa Mara ya kwanza kutumia sembe nilikaa wiki na siku kadhaa bila kwenda chooni halafu hata hiyo haja huipati ipasavyo hii ni kwa sababu ulioitoa mwenyewe kwenye point ya kwanza kwa hiyo acha wengine tuendelee na dona yetu chamsingi Hayo mahindi yaoshwe kabla ya kusaga
 
Na hyo ndo ilikuwa point yakee kubwa ya kuifadhilisha sembe dhidi ya dona..
 
Mleta mada nakusifu kwa kuandika makala hii ndefu..

Mimi pia ni mtaalamu wa Nutrition lakini kiukweli ni mvivu kuandika...
Umenena vizuri sana mkubwa, mwenye macho na aone asisubr kuadithiwa, wanaume wa dar washazoea kula sembe afu miguu juu kutizama season mazoezi hawafanyi matokeo yake kila mtu ana kitambi na uzito uliokithiri
 
Umeeleza vzr sana mzee lkn umesahau kitu kinachoitwa mfumo wa utoaji taka mwilini kulingana na mwenyewe maelezo yako hapo juu tu Dona litabaki kuwa bora kwakuwa unapata choo kwa haraka na chepesi kuliko Sembe ambapo waweza kaa hata wiki nzima bila kupata haja inayoeleweka na ukijakutoa utakunya kma mbuzi wacha tupige Dona bwana
 
Back
Top Bottom