Je, ni kweli Vigogo wamewahi kukataa TISS kuwa taasisi huru inayoshughulikia usalama wa taifa Pekee?

Hatari sana.
 
haya mawazo ya kishamba huwa mnayatoa wapi ?
mimi nawajua watu ambao hawajawahi hata kuwa na rafiki mwanaccm achilia mbali wao wenyewe kuwa wanaccm ambao wanafanya kazi kwenye vyombo vya ulinzi na ofisi za umma.
Hata mapolisi wanaotumwa kuzuia mikutano ya CDM sio wote wanaipenda CCM au wanajuana na wanchama wa chama tawala
 
100%. Toka nishudie mtu wa chombo amevaa suti Tena ndo alikuwa msimamizi mkuu wa kituo Cha kupigia kura ..KIONGOZI x akaja usiku saanane kwa helicopter .matokeo yakabadlishwa .alieshinda akatangazwa ameshinda alieshindwa akashinda ..

Toka huo mwaka ,niliapa na naapa sitaaka nipige kura mpaka KATIBA ibadilishwe
 

Huyu mpumbavu hajui kwamba CIA inashughulika na mambo ya nje ya nchi tu ya ndani kuna taasisi kibao za usalama wa ndani ya USA
 
TISS ya Tz utasikia
Mgombea wa CCM ana upinzani gani huko vitongojini, Vijijini
Ni nani Wananchi wanampenda yaani wao hawaulizi wagombea wa vyama vingine wanafanya vetting kwa wagombea wa CCM tu.
 
Ukiifanya TISS iwe huru nnje ya siasa, maana yake unaenda kuizika CCM na kuifanya Tanzania ipae kimaendeleo.

Kwa hawa wanaojipa uongozi, na ambao wanarithishana uongozi mpaka kwa wajukuu, tutegeemee kweli kwa TISS huru kutokea!!!??

Haiwezekani kwa wao kukubali hili bila shinikizo la wananchi, maana kuundwa kwa TISS huru maana yake ni kufa kwa CCM, na kifo cha CCM kinamaanisha ni kifo (na pengine kufilisika kwa mali) cha familia zao ambazo zinanufaika na CCM kuwa chama dola.

Ndio maana katiba mpya (ambayo ndani yake TISS huru itaundwa), kunapingwa kwa kufa, kuua na kupona na wanaCCM wanufaika wa mfumo huu wa "TISS siasani".
 
Sahihi kabisa...

Halafu CIA haihusiki kabisa na 'Covert operations' ndani ya ardhi ya Marekani kama kuna umuhimu huo basi FBI ambayo ni kitendea kazi chadepartment of justice (Idara ya Sheria) itachukua hilo jukumu.
 
CIA yenyewe inaeleza kwamba kazi yake ni kutoa objective intelligence, na kwamba CIA haifanyi politics ; politics inaamuliwa na viongozi wa kisiasa.
Utakuwa umeisahau hii hapa chini.
===
Former CIA Director and Secretary of State Mike Pompeo stated in April 2019, "We lied, we cheated, we stole," describing the operational realities and training of the CIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…