Al maktoum
JF-Expert Member
- Nov 23, 2022
- 499
- 678
Sheikh wa TikTok Yuko sahihi kabisa.Huyo shekhe wa Tiktok atakua hana hata D ya mchongo,atakuwa ni Shehena huyo
Aliyoyazungumza ndiyo yaliyoandikwa kwenye vitabu vinaelezea taratibu za kuzikana katika uislamu.
Katika uislamu anapokufa mwislamu mwenzetu sisi tunawajibika kumfanyia mambo manne (4)
1. Kumuosha.
2. Kumvika sanda.
3. Kumswalia.
4. Kumzika. Na kati ya mambo hayo manne hakuna hata moja tuloruhusiwa kumfanyia mtu aliyekufa hali ya kuwa ni mfuasi wa dini tafauti na uislamu.
Kwa maana akifa mtu nje ya dini ya kiislamu,
A. Haturuhusiwi kumuosha.
B. Haturuhusiwi kumvika sanda.
C. Haturuhusiwi kumswalia.
D. Na haturuhusiwi kumzika isipokuwa kama amefia katika mazingira ambayo hamna wafuasi wa dini yake hapo tutaruhusiwa kumfukia kwenye shimo la aina yoyote mbali na makazi ya watu na pia mbali na makaburi ya waislamu ili asije akatunukia pale ambapo itakuwa hakuna wafuasi wa dini yake wa kumzika kwa taratibu zao.