Swali zuri sana lakini hatahivyo siwezi kukujibu tafuta vyanzo mbalimbali vinavyochambua ibada ni nini
Kwenye uislamu tunaambiwa mwenyezi Mungu hakuumba majini na watu isipokuwa ni kwa ajili ya kumuabudu yeye tu. Maana yake mwislamu kila utakachokifanya kama uislamu ulivyoelekeza au kila utakachoacha kukifanya kama uislamu ulivyokataza basi utahesabiwa umefanya ibada (unaandikiwa thawabu)
Kuna mambo fulani fulani tunachanganyika na wasio waislamu lakini mambo mengine yana ibada maalumu ndani yake hivyo haturuhusiwi kuchanganyika. Vivyo hivyo kuna ibada maalumu ambazo ndani yake kuna matendo yanayoruhusiwa kuchanganyika
Ndoa na taratibu zake zote ni jambo la kiibada lakini ndani yake kuna matendo yanayoruhusiwa kuchanganyika mfano kula ubwabwa wa harusi pamoja lakini ikifika sasa watu waingie kanisani kwa ajili ya misa maalum kwa wanandoa tayari hilo ni jambo la kimaalumu zaidi kwakuwa lina taratibu zake hivyo muislamu atajitenga kwa kuwa imani yake haihusiani na yanayokwenda kufanyika humo
Mfano mwingine ni kwenye matatizo majanga na maafa tutasaidiana bila kujali dini mfano kuokoa watu, kujengea, kutetea watu au kitu, kuondosha hatari nk lakini ikifika kwenye swala la umaalumu mfano kuzika tayari sisi waislamu itatupasa kuishia nyumba ya msiba na kutoa pole tu; kuzika kwa kuwa ni jambo la kiibada tutawaachia waumini wa dini husika wakaperform ibada hiyo
Kuna watu wakiona hivyo wanatafsiri vibaya, kuna wanaoona sisi kujitenga kwenye mambo kama hayo eti tuna nongwa na ni wabaguzi hatutaki kutangamana na wenzetu na kuna wanaoona eti sisi tunajidai wasafi sana wa roho na tunajiona sisi ndio tulio sahihi sana na wengine wote wamepotea hivyo tunawanyanyapaa. Sikia wewe unayefuatilia maneno haya
Kwanza kabisa kila muumini kutoka dini yoyote ile lazima ajione yeye ndiye aliye sahihi zaidi na dini yake na wengine wote walio kinyume na dini yake wamepotea! Kama hujioni hivyo basi wewe hujawa muumini bado rudi kwa viongozi wako wa dini haraka sana ukasaidiwe
Pili ni kwamba ukiwa muumini wa dini fulani ukaenda kwenye ibada za wengine inaleta mushkeli. Hivi kweli niingie kanisani unafikiri kitatokea nini wakati ibada ikiendelea? Kutazaliwa kuchunguzana, kukebehiana, chuki, nk maana nitavuruga mambo mengi, nitakuwa nachunguza sana wewe utaona nakosea makusudi nawasanifu nk na of course lazima yatokee hayo ya kukebehiana na kutazamana vibaya
Hivyo kuzuiwa huko ni kwa ajili ya kujenga zaidi na wala siyo kubomoa. Imagine siyo mwislamu halafu uingie msikitini wakianza kuswali lazima utaona kero kuinama kuinuka, kujikunja miguu nk. Vivyo hivyo kwa asiye mkristo akifika kwenye ibada za kikristo ataona usumbufu kufunga macho kupiga magoti nk sasa ili mwishowe asije kuvuruga ibada za watu bure basi kwa usalama wake na wengine ni bora asishiriki