Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Mwislamu haruhusiwi kushiriki jambo lolote linaloendeshwa kinyume na taratibu za kiislamu zilizofundishwa na mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم
Sasa mnakujaga kufanya nini?
 
Basi hiyo ni dini ya ajabu sana inayohamasisha na kuelekeza kila aina ya njia ya kuongeza gap katika ubaguzi. By the way, hatupungukiwi na wala hawatuongezei chochote kwa wao kutoshiriki mambo ya Kikristo. Acha wakomae na hali zao.
Kwakuongezea nyinyi wakristo mnapohudhuria hafla za kidini za waislamu katika mambo ya musiba au sherehe tunaona kuwa mnajipendekeza kushiriki mambo ambayo hayawahusu. Kila mtu aangalie mambo ya dini yake.
Washirikina wa Makka walipomuomba mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ashiriki baadhi ya mambo ya dini yao ya ushirikina Allaah سبحانه وتعالى aliteremsha suuratul Kaafiruna ambapo inayosema :

"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }
( 1 ) Sema: Enyi makafiri!

{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
( 2 ) Siabudu mnacho kiabudu;

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
( 3 ) Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }
( 4 ) Wala sitaabudu mnacho abudu.

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
( 5 )Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
( 6 ) Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Kwahiyo ninyi wakristo mna taratibu zenu za kuzika wafu wenzenu na sisi waislamu tuna taratibu zetu za kuwazika wafu wetu. Kila mtu aangalie yanayomhusu.
 
Sasa mnakujaga kufanya nini?
Nawashangaa hao wanaokuja!.
Mimi mama yangu alisilimu toka ukristo na hadi leo wajomba zangu wengi bado ni wakristo na hadi leo sitii mguu kwenye misiba yao kwakuwa taratibu zao za kuzikana ziko kinyume na taratibu za dini yangu.
 
Nanukuu: "Na ni kweli kwamba kila analolifanya muislamu lazima liwe lina maelekezo kutoka kwenye Quran au hadithi au tafsiri na maelekezo ya wanachuoni wanaotambulika."
OK. 1. Sasa ghorofa la K/K limeporomoka na ww upo hapo. Unaanza kutafuta Quran ili upate kifungu chenye maelekezo nn cha kufanya au ?
2. Umepata safari ya kuelekea Mwanza haraka e.g. ww ni Askari; kutoka kwa boss wako. Ww unaenda kutafuta kitabu chenye maelekezo?
3. Wewe umekuja hapa jukwaani na kuandika hiki ulichoandika. Naomba utoe ni kifungu gani kwenye Quran kilichokupa maelekezo.
Maswali ya chekechea!
Kama akili yako inakwambia kwamba umeniuliza maswali magumu basi umejidanganya sana.
Ungekuwa umeuliza kwa nia ya kuelewa ningekupa majibu yote toka ndani ya Quran , hadithi za mtume na maelekezo ya wanachuoni.
Ila kwa sababu nia yako ni kushindana na kila mwenye mtazamo kama nilionao mimi nimeamua kukuacha na upumbavu wako!
Lakini Lau nakutana na muislamu mwenye nia ya kujifunza dini yake akiniuliza maswali kama uliyouliza wewe nitamjibu ndani ya muda mfupi sana na sitatumia nguvu kubwa kutafuta majibu ya maswali mepesi sana kama uliyouliza wewe.
 
Unajishaua tu
 
Hivi wewe unatumia akili yako sawasawa, kaombe tafsiri ya Surat qaafirun , uislamu unatufundisha mpaka namna ya kulala, kuzungumza, ku ingiliana na mkeo nk, uislamu haujaacha kitu, narudia ni mgonjwa sawa, kusaidia au kutoa sadaka tumeusiwa kila palipozungumzwa kusimamisha swala basi lazima pasemwe na kutoa sadaka ama zaka, lakini hatujaambiwa tushiriki ibada za Imani nyingine kwa maana kila mtu ana dini yake full stop
 
Kwakuongezea nyinyi wakristo mnapohudhuria hafla za kidini za waislamu katika mambo ya musiba au sherehe tunaona kuwa mnajipendekeza kushiriki mambo ambayo hayawahusu. Kila mtu aangalie mambo ya dini yake.
Washirikina wa Makka walipomuomba mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ashiriki baadhi ya mambo ya dini yao ya ushirikina Allaah سبحانه وتعالى aliteremsha suuratul Kaafiruna ambapo inayosema :

"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }
( 1 ) Sema: Enyi makafiri!

{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
( 2 ) Siabudu mnacho kiabudu;

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
( 3 ) Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }
( 4 ) Wala sitaabudu mnacho abudu.

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
( 5 )Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
( 6 ) Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Kwahiyo ninyi wakristo mna taratibu zenu za kuzika wafu wenzenu na sisi waislamu tuna taratibu zetu za kuwazika wafu wetu. Kila mtu aangalie yanayomhusu.
Akhi, umeniwahi nami nimemwambia aombe tafsir ya surat qaafirun ili aelewe
 
za ndaaani kabisa inasemekana sio kosa Mwislamu kuua mtu asiyekuwa wa dini yake, Quran inaruhusu kabisa
Hakuna mahala kwenye Quran wala hadithi za mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala maelekezo ya wanazuoni hasa wa madhehebu yangu ya ahlissunna Wal jamaa , hakuna mahala popote ambapo waislamu wameruhusiwa kuwaua makafiri ( wenye kufuata dini kinyume na uislamu ) kiholela bila sababu yoyote. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoutawala mji wa Madina palikuwa na wafuasi wa dini ya kiyahudi na katika mambo ambayo mtume aliyafanya mwanzoni kabisa ni kufanya mikataba ya kuishi kwa amani na mayahudi waliopo katika mji wa Madina. Hali iliendelea hivyo hadi wayahudi walipovunja mikataba ya amani waliyowekeana na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa kujiunga na washirikina wa kiarabu kutoka katika mji wa Makka waliokuwa wanampiga vita Mtume na waislamu ndipo hapo Mtume alipowapiga vita wayahudi kutokana na uhaini waliomfanyia na akawafukuza katika mji wa Madina wakakimbilia katika mji wa khaibar.
Uislamu ni dini ya amani ambayo haiwaruhusu wafuasi wake kuua watu kiholela bila sababu za kisheria, ama matendo ya ugaidi na uharamia unaofanywa na baadhi ya makundi yaliojifunika mwamvuli wa uislamu kama Al Qaida , Al shabaab, Boko Haram Iss nk mambo wanayoyafanya makundi haya ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini ya kiislamu.
 
Inaruhusiwa kuua mtu ambaye si Muislamu. Wala si tatizo na tena hapo unapewa mabikra 72
Wewe ni muongo. Halafu hii habari ya mabikra 72 sijui mliiokota jalala gani! Ni kweli moja ya starehe za peponi ni wanawake wasafi ambao ni mabikra.
Lakini ni nani aliyewaambia kuwa idadi ya hao wanawake ni 72 ?!
 
Hivi wewe unatumia akili yako sawasawa, kaombe tafsiri ya Surat qaafirun , uislamu unatufundisha mpaka namna ya kulala, kuzungumza, ku ingiliana na mkeo nk, uislamu haujaacha kitu, narudia ni mgonjwa sawa, kusaidia au kutoa sadaka tumeusiwa kila palipozungumzwa kusimamisha swala basi lazima pasemwe na kutoa sadaka ama zaka, lakini hatujaambiwa tushiriki ibada za Imani nyingine kwa maana kila mtu ana dini yake full stop
Sawa mkuu.
 
Maswali ya chekechea!
Kama akili yako inakwambia kwamba umeniuliza maswali magumu basi umejidanganya sana.
Ungekuwa umeuliza kwa nia ya kuelewa ningekupa majibu yote toka ndani ya Quran , hadithi za mtume na maelekezo ya wanachuoni.
Ila kwa sababu nia yako ni kushindana na kila mwenye mtazamo kama nilionao mimi nimeamua kukuacha na upumbavu wako!
Lakini Lau nakutana na muislamu mwenye nia ya kujifunza dini yake akiniuliza maswali kama uliyouliza wewe nitamjibu ndani ya muda mfupi sana na sitatumia nguvu kubwa kutafuta majibu ya maswali mepesi sana kama uliyouliza wewe.
Mbona itakuwa mwislam atakayekuuliza maswali kama niliyouliza mimi si naye atakuwa ni mpumbavu kma mimi? Bora mimi umeniacha na upumbavu wangu.
 
Kwakuongezea nyinyi wakristo mnapohudhuria hafla za kidini za waislamu katika mambo ya musiba au sherehe tunaona kuwa mnajipendekeza kushiriki mambo ambayo hayawahusu. Kila mtu aangalie mambo ya dini yake.
Washirikina wa Makka walipomuomba mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ashiriki baadhi ya mambo ya dini yao ya ushirikina Allaah سبحانه وتعالى aliteremsha suuratul Kaafiruna ambapo inayosema :

"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }
( 1 ) Sema: Enyi makafiri!

{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
( 2 ) Siabudu mnacho kiabudu;

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
( 3 ) Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }
( 4 ) Wala sitaabudu mnacho abudu.

{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
( 5 )Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
( 6 ) Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Kwahiyo ninyi wakristo mna taratibu zenu za kuzika wafu wenzenu na sisi waislamu tuna taratibu zetu za kuwazika wafu wetu. Kila mtu aangalie yanayomhusu.
Sawa mkuu.
 
Mwislamu haruhusiwi kushiriki jambo lolote linaloendeshwa kinyume na taratibu za kiislamu zilizofundishwa na mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم
Ndo mana nikasema komaeni na hali zenu - hatujawaita mje huku.
 
Mbona itakuwa mwislam atakayekuuliza maswali kama niliyouliza mimi si naye atakuwa ni mpumbavu kma mimi? Bora mimi umeniacha na upumbavu wangu.
Mwislamu atakayeniuliza atakuwa anataka kujua linalofaa alifanye na lisilofaa aliache.
Wewe unataka ligi na mimi lakini unakuja na maswali ya chekechea kisha ujisifu kuwa unajua kujenga hoja kwa kuuliza maswali ya kitoto!.
 
Ibada ni nini?
Swali zuri sana lakini hatahivyo siwezi kukujibu tafuta vyanzo mbalimbali vinavyochambua ibada ni nini

Kwenye uislamu tunaambiwa mwenyezi Mungu hakuumba majini na watu isipokuwa ni kwa ajili ya kumuabudu yeye tu. Maana yake mwislamu kila utakachokifanya kama uislamu ulivyoelekeza au kila utakachoacha kukifanya kama uislamu ulivyokataza basi utahesabiwa umefanya ibada (unaandikiwa thawabu)

Kuna mambo fulani fulani tunachanganyika na wasio waislamu lakini mambo mengine yana ibada maalumu ndani yake hivyo haturuhusiwi kuchanganyika. Vivyo hivyo kuna ibada maalumu ambazo ndani yake kuna matendo yanayoruhusiwa kuchanganyika

Ndoa na taratibu zake zote ni jambo la kiibada lakini ndani yake kuna matendo yanayoruhusiwa kuchanganyika mfano kula ubwabwa wa harusi pamoja lakini ikifika sasa watu waingie kanisani kwa ajili ya misa maalum kwa wanandoa tayari hilo ni jambo la kimaalumu zaidi kwakuwa lina taratibu zake hivyo muislamu atajitenga kwa kuwa imani yake haihusiani na yanayokwenda kufanyika humo

Mfano mwingine ni kwenye matatizo majanga na maafa tutasaidiana bila kujali dini mfano kuokoa watu, kujengea, kutetea watu au kitu, kuondosha hatari nk lakini ikifika kwenye swala la umaalumu mfano kuzika tayari sisi waislamu itatupasa kuishia nyumba ya msiba na kutoa pole tu; kuzika kwa kuwa ni jambo la kiibada tutawaachia waumini wa dini husika wakaperform ibada hiyo

Kuna watu wakiona hivyo wanatafsiri vibaya, kuna wanaoona sisi kujitenga kwenye mambo kama hayo eti tuna nongwa na ni wabaguzi hatutaki kutangamana na wenzetu na kuna wanaoona eti sisi tunajidai wasafi sana wa roho na tunajiona sisi ndio tulio sahihi sana na wengine wote wamepotea hivyo tunawanyanyapaa. Sikia wewe unayefuatilia maneno haya

Kwanza kabisa kila muumini kutoka dini yoyote ile lazima ajione yeye ndiye aliye sahihi zaidi na dini yake na wengine wote walio kinyume na dini yake wamepotea! Kama hujioni hivyo basi wewe hujawa muumini bado rudi kwa viongozi wako wa dini haraka sana ukasaidiwe

Pili ni kwamba ukiwa muumini wa dini fulani ukaenda kwenye ibada za wengine inaleta mushkeli. Hivi kweli niingie kanisani unafikiri kitatokea nini wakati ibada ikiendelea? Kutazaliwa kuchunguzana, kukebehiana, chuki, nk maana nitavuruga mambo mengi, nitakuwa nachunguza sana wewe utaona nakosea makusudi nawasanifu nk na of course lazima yatokee hayo ya kukebehiana na kutazamana vibaya

Hivyo kuzuiwa huko ni kwa ajili ya kujenga zaidi na wala siyo kubomoa. Imagine siyo mwislamu halafu uingie msikitini wakianza kuswali lazima utaona kero kuinama kuinuka, kujikunja miguu nk. Vivyo hivyo kwa asiye mkristo akifika kwenye ibada za kikristo ataona usumbufu kufunga macho kupiga magoti nk sasa ili mwishowe asije kuvuruga ibada za watu bure basi kwa usalama wake na wengine ni bora asishiriki
 
Basi hiyo ni dini ya ajabu sana inayohamasisha na kuelekeza kila aina ya njia ya kuongeza gap katika ubaguzi. By the way, hatupungukiwi na wala hawatuongezei chochote kwa wao kutoshiriki mambo ya Kikristo. Acha wakomae na hali zao.
Christmass si kesho kutwa tu, observe bwana kafir.
 
Huyo shekhe wa Tiktok atakua hana hata D ya mchongo,atakuwa ni Shehena huyo
 
Back
Top Bottom