Mazishi ni ibada
Kila mtu achunge ibada zake
Muislamu akihudhuria misiba ya wakristo Kuna mambo hatakiwi kuyafanya
Yale yote yanayohusu ibada au imani zao
Hata mkristo hawezi kwenda kwenye msiba wa kiislamu kisha akamswalia maiti au kushiriki dua labda awe mnafiki.
Muislamu anaweza kwenda msibani kuwafariji na kushiriki baadhi ya shughuli zisizokuwa za ibada ya kikristo, wakianza ibada zao anatembea zake
NB
UISLAMU HAUTAKI UNAFKI NA KUJIONESHA KWA WATU
Kwa mtazamo wako huo, shekhe yupo sahihi, kwa maana shughuli ya maziko, toka mwanzo mpaka mwisho, ni ibada? Kwa maana kwenye maziko, utaratibu wote ni wa kidini kuanzia kwenye sala/swala, mpaka tendo la kumwingiza marehemu kaburini.
Ila haya mambo ya utengano kwenye maisha ya kijamii, ni upuuzi inaofanywa na sisi wapokea dini, tofauti na walioleta dini.
Kule Uturuki, Papa Francis alipotembelea nchi hiyo, shekhe mkuu aliruhusu na kuambatana na papa msikitini ambapo Papa na shekhe mkuu walifanya ibada ya pamoja.
Kule India, kuna eneo moja lina wakristo wengi na waislam idadi yao ni ndogo sana. Waislam wa mahali pale, hawana hata msikiti. Paroko wa kanisa la mahali pale aliruhusu waislam pia wawe wanafanyia ibada kanisani kuliko nje kwenye jua na mvua. Kanisa linatumika Ijumaa na waislam, Jumapili linatumika na wakristo.
Mafundisho ya dini zote yanasisitiza upendo. Upendo uko wapi kama huwezi kusaidiana na jirani au ndugu yako? Kuna watu wamechakachua mafundisho ya kweli, halafu wanaeneza chuki kupitia dini. Ninachoamini ni kuwa kama Mungu hataki dini fulani iwepo Duniani, hashindwi kuiangamiza au kuifuta, wala hahitaji msaada wa mwanadamu kuofuta au kuiadhibu. Dini zote zinafundisha kuwa Mungu ni muweza wa yote. Kilichopo kiwe kibaya au kizuri, kwa hekima yake, ameruhusu kiwepo. Tuendelee kufundishana yote yaliyo mema kwa kadiri ya mpango wa Mungu, lakini mwamuzi wa mwisho ni Mungu mwenyewe, maana yeye anayaona na kuyajua hata yale ambayo tuna uwezo wa kuyaficha kwa wanadamu wenzetu.
Watu wenhgi hawajui, ila kiuhalisia uislam na ukristo, kwenye masuala ya msingi ya kiimani, vinakaribiana sana kuliko dini yoyote. Wote wanaamini:
1) Uwepo wa Mungu mmoja (waislam hawatambui utatu mtakatifu)
2) Yesu Kristo/ Isa ni mteule wake Mungu, alizaliwa na Bikira Maria kwa njia ya muujiza, alipaa mbinguni akiwa na mwili, atarudi tena (waislam hawamtambui kama ni nafsi ya Mungu bali ni nabii, hawakubali kuwa alikufa msalabani kwa vile alikuwa mteule wake Mungu, atakaporudi itaitawala Dunia yote).
3) Upendo na huruma kwa maskini.
4) Kumpenda na kumtii Mungu
5) Wizi, uzinzi, kuabudu miungu n.k., ni dhambi
Tofauti Kubwa:
Wakristo, rejea mafundisho ya Masiha Yesu Kristo, wanaamini sana katika msamaha, kisasi ni cha Mungu; waislam wanaamini sana katika kuadhibu na kisasi. Hii inawafanya waislam kuwa na misimamo mikali dhidi ya wanayeamini ametenda dhambi, kama vile kuua wazinzi, kukata mikono wevi, kuwaua wanaomkufuuu Allah na mtume wake, n.k. Lakini wakati huo huo, Mtume Mohamad anasema kuwa yeye ni mfuasi namba moja wa Isa bin Mariam; na huyo anayesema yeye ni mfuasi wake namba moja, alisema kuwa tuwasamehe hata maadui zetu maana kama hatutawapenda maadui zetu, tukawapenda tu marafiki zetu, tutatofautiana vipi na wale wasiomjua Mungu, maana nao huwapenda marafiki zao na kuwachukia madui zao?
Al Jazeera
Pope Francis prays in Istanbul’s Blue Mosque
Pope prays for stronger ties between Vatican and Islam during second leg of his three-day visit to Turkey.
Pope Francis has taken part in a Muslim prayer alongside the Grand Mufti of Istanbul on the second leg of his three-day visit to Turkey.
Francis stood on Saturday morning with his head bowed and hands clasped in front of him for two minutes of silent prayer inside the 17th-century Sultan Ahmet mosque, aiming to show respect for Islam and encourage stronger ties between the two faiths.
“May God accept it,” Rahmi Yaran, the Grand Mufti of Istanbul told the pope at the end of the prayer.