Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Haikatazwi kuhudhuria misiba ya wasio waislamu ila usivuke mipaka. Kwa mfano waislamu huwa hawaagi maiti kwa hivyo watu wakiwa wanaaga wewe unakaa pembeni. Na pia kwa upande wa wanawake hawatakiwi kwenda makaburini, sasa unakuta mwanamke muislamu lakini anaenda mpaka makaburini kuzika ndio mana mashehe wanagomba.
Nanukuu:
"Haikatazwi kuhudhuria misiba ya wasio waislamu ila usivuke mipaka".
Swadakta. Hii 👆 👆 ni kauli dhabiti. Wanawake wa Kiislamu kama wanafahamu hilo sidhani wapo wanaokiuka - labda hawa wa kizazi kipya.
 
Wataalam wa mambo weken sawa haya mambo maana tunakoelekea sio pazur ,hii Ina ukwel gan?
 
Ndiyo haruhusiwi kuhudhuria mazishi ya mtu yeyote anae mshirikisha Mungu (mshirikina)
 
Wapo kibao. Ungia TikTok na Instagram. Na uzuri waumini wanawalewa sana, wana wapa big up.
OooooH! Kumbe ni mkakati wa watu fulani wanaovaa baraghashia na kujitanda nguo nyekundu shingoni. Labda watawapata watakaochangia ujenzi wa madrasa.
 
Ndiyo kwani lazima?
Hawajalazimishwa lakini machoni mwa Jamii jambo hilo sio poa kwani linachipusha mbegu ya Ubaguzi wa kidini na kuigawa Jamii mahalia. Kwani wakihudhuria walau kama wasindikizaji tu kuna shida gani??
 
Msilazimishe. Kama hamtakiwi achaneni na misiba siyo lazima au kulia lia
Nimesema haujalazimishwa. Ni maamuzi yako kusuka au kunyoa. Kumbuka huyo ni sheeee (sio Shekhe)aliyesema sio Mamlaka au Msemaji katika Imani. Ni mhubiri tuu na anaweza akawa anahubiri ya kwake anavyojisikia.
 
Back
Top Bottom