Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Jf imekua kijiwe cha udini siku hizi
Sidhani kama umefanya upembuzi yakinifu ndo ukaleta hitimisho hili kwamba Jf imekua kijiwe cha udini siku hizi. Tuthibitishie jambo hilo vinginevyo huo ni uzushi.
 
Nimemsikia sheeee uko tik tok kuwa muislamu anapo hudhuria ibada ya mazishi ya kikristo wakati yeye muislamu anakuwa amekiukya taratibu za kiislamu
Kila mtu si ana dini na imani yake, sasa inakuwaje wachanganye ibada ya pamoja!
 
Hakuna mahali ilipokatazwa. Huku kwetu, Jamii yote bila kujali Imani ya mtu wote tunashiriki mazishi awe mwislamu au mkristo au asiye na dini. - tunakutanaga kuanzia nyumbani kwa marehemu, Kanisani (tena ndani ya kanisa)hadi makaburini. Hakuna shida. La msingi hapo ni kuheshimu kinachoendelea.
Kama huna ujualokunyamanza ni bora kuliko kutoa hukumu ya jambo usilolojua.
Nikikuuliza kitabu kinachoruhusu muislamu kumzika kafiri utakipata wapi?!
 
Ni kweli. Yatakiwa waislamu wawaache wafu wazike wafu wao.
Kuzika ni ibada , na kama ni ibada ina taratibu zake, hafanyiwi kila mtu.
Dah! Kwani ibada ya mazishi wanafanyiwa watu hai waliohudhuria hapo au anafanyiwa marehemu??
 
Kama huna ujualokunyamanza ni bora kuliko kutoa hukumu ya jambo usilolojua.
Nikikuuliza kitabu kinachoruhusu muislamu kumzika kafiri utakipata wapi?!
Ama kweli mtu wa kitabu! Hivi ww kila unalofanya au kutenda lipo kwenye kitabu?
Hoja iliyopo hapa ni kuhusu Uwepo wa katazo kwa mtu Mwislamu kushiriki mazishi ya mtu Mkristo. Labda iwe sijaielewa mada.
Ninajua kwamba wapo baadhi ya watu (wakiwemo Waislam wachache sana) hutoa visingizio vya Udini kwa kutohudhuria mazishi ya wakristo au hata ya Waislam wenzao madhehebu tofauti (Shia au Suni au Ahmadiya etc)lakini ukweli ni kwamba; ama ni wavivu au wanaogopa kufika maeneo ya makaburi n.k. halafu wanatumia udini kama kichaka cha kujificha kwa mambo yao.
 
Sidhani kama umefanya upembuzi yakinifu ndo ukaleta hitimisho hili kwamba Jf imekua kijiwe cha udini siku hizi. Tuthibitishie jambo hilo vinginevyo huo ni uzushi.
Kila siku humu wafia dini mnakaa mnatukanana humu
 
Mkuu, kwa uislamu siyo lazima, nina maana ya kwamba haulazimishi kua muislamu, pia Allah hato pungukiwa chochote au kuzidi chochote wewe ukiwa muislamu au kutokua muislamu, hivo ni maamuzi yako
Bado hujanielewa tu, mpaka hapo mimi siko tayari kutumika ktk kutangaza utamaduni wa mtu mwigine kwa sababu nilizaliwa mwafrika na nitakufa mwafrika. Period.
 
Nilichoona hata hoja za wenyewe kwa wenyewe humu Zina mikinzano...hatari sana sheikh!
Miafrika ni mijitu ya kuletewa tu na tunapokea bila hata kuuliza, kupembua etc!
Ndivyo tulivyo...
 
Haikatazwi kuhudhuria misiba ya wasio waislamu ila usivuke mipaka. Kwa mfano waislamu huwa hawaagi maiti kwa hivyo watu wakiwa wanaaga wewe unakaa pembeni. Na pia kwa upande wa wanawake hawatakiwi kwenda makaburini, sasa unakuta mwanamke muislamu lakini anaenda mpaka makaburini kuzika ndio mana mashehe wanagomba.
 
Back
Top Bottom