Kwanza ifahamike si kila mtu anayevaa kanzu au kujiita Sheikh ni Sheikh kweli,kwahiyo msiyapokee mambo kibubusa tu
Pili,Uislamu umeweka mkazo mkubwa sana katika utengamano na jamii,yani ni muhimu sana jamii kushirikiana kwa hali na mali,ndio maana ujirani katika mtazamo wa kiislamu ni jambo kubwa na muhimu sana.
Mtume Muhammad rehema na amani ziwe juu alikuwa anahusiwa sana na Malaika Jibril mara kwa mara wanapokutana juu ya swala zima la kuwajali majirani
Sasa je utawajali vipi majirani kama hauhudhurii furaha yao au wakati wa huzuni yao?
Kwahiyo kuhudhuria misiba inaruhusiwa ila kuna baadhi ya mambo hatutakiwi kushiriki kama kuangalia maiti kama wasio waislamu wanavyofanya,hata ndani ya uislamu maiti inaangaliwa na ndugu wa karibu tu lkn sio kila mtu anaweza kumuangalia maiti
Kwahiyo kushiriki misiba ni ruhusa na hata kuzika ila kuna baadhi ya ibada tunajitenga nazo,je kuna mwenye shida na hilo?