Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Je, ni kweli Waislamu mnakatazwa kuhudhuria mazishi ya kikristo?

Utapokimbilia mahala kwenye msiba kitendo hicho ni ibada iwe kwako au kwao
Unataka kushiriki ibada ipi tena

Kesho mtakuja kusema kumsaidia mtu ambae sio imani yako utakuna umeririki ibada ya mtu mwingie ni kosa
Mnasahau ya kua kutenda jambo jema ni ibada
Hivo ni vitu viwili , ku kimbilia msibani au ugonjwa na kushiriki maziko
 
Ngoja tukaulize kwa ma sheikh , lakini hapo hapana maziko in short huyo atazikwa na city , kama ingelikuwa mtoto sawa
Kama mazishi ya mkristo hayahudhuriwi na muislam kiku-quruan, na ikatokea mkristo amefia Pemba na hana ndugu, ataoza anuke kwa kuwa na kuitenga maiti yake ?
 
Siyo kweli,Muislamu anahudhuria misiba ya wakristo na hata ya wale wasioamini dini yoyote isipokuwa haruhusiwi kushiriki ibada na wanawake hawaruhusiwi kwenda makaburini haijalishi msiba wa Mkristo au Muislamu.
 
Sasa wewe una bisha nini, na huo msiba wa mkristo ana hudhuria kwa ruhusa ya nani, nani alimuona aki do hivo , kila kitu kipo wazi, shiriki kwa kumpinga ALLAH sawa ni juu yako
 
Nimemsikia sheeee uko tik tok kuwa muislamu anapo hudhuria ibada ya mazishi ya kikristo wakati yeye muislamu anakuwa amekiukya taratibu za kiislamu
Mazishi ni ibada

Kila mtu achunge ibada zake

Muislamu akihudhuria misiba ya wakristo Kuna mambo hatakiwi kuyafanya

Yale yote yanayohusu ibada au imani zao

Hata mkristo hawezi kwenda kwenye msiba wa kiislamu kisha akamswalia maiti au kushiriki dua labda awe mnafiki.

Muislamu anaweza kwenda msibani kuwafariji na kushiriki baadhi ya shughuli zisizokuwa za ibada ya kikristo, wakianza ibada zao anatembea zake
NB
UISLAMU HAUTAKI UNAFKI NA KUJIONESHA KWA WATU
 
Sasa wewe una bisha nini, na huo msiba wa mkristo ana hudhuria kwa ruhusa ya nani, nani alimuona aki do hivo , kila kitu kipo wazi, shiriki kwa kumpinga ALLAH sawa ni juu yako
Umeuliza tunakujibu hutaki! Sasa kama ulikuwa na majibu yako umeuliza ili iweje?Waislamu tunahudhuria misiba ya mtu yeyote isipokuwa kwenye ibada hatushiriki,wakiumwa tunakwenda kuwajulia hali iwe nyumbani au hospitali, wakitukaribisha chakula tunakula ili mradi viwe halali kwa mujibu wa dini yetu na ikitokea amekudanganya na wewe hukubaini yeye ndiye atakayepata dhambi na ataadhibiwa na Mwenyezi Mungu, yaani kwa kifupi hakuna katazo lolote katika kushirikiana na asiye Muislamu ili mradi lisiwe ni jambo la kumuasi Mwenyezi Mungu.
 
Dini ni ujinga na uwa sipend kabisa kuendekeza huo ujinga sijui kitoweo aje sheikh achinje nachinja mwnyw na atakaekula ale na hata km wamekuja kwang watanitazama nachinja na vikiiva natenga wakula atakula tu.

Kuna kpnd nilikuwa napikia mafuta ya nguruwe chakula nyumban kwng nishawalisha sna hao wanaojiita mashekh walivyo walafi et chakula kitamu na wengne washajua na ndy kwnz wanakuja na wanakula i am a man of my principal at my home utake usitake utafata taratibu zng otherwise uwe kwko
 
Kwa hiyo ,uislam na Quran, vimemtenga mkristo na kumbagua tangu akiwa hai hadi Maiti yake ? Vipi na wahindu watengwa kadhalika ? Wahindu nao wametengwa ?
Sasa mkuu kumbagua kivipi, nimekwambia mgonjwa sawa, hata awe muhindu, ktk maziko kuna Misa , ibada, maombolezo na mila za ukristo hayo muislamu kakatazwa pia wanaume uchanganyika na wanawake
 
Wao ndio wanatutenga sisi
Mkuu ukifatilia familia nyingi ziwe za Wakristo au Waislamu wamechanganyikana kwenye koo moja wengine mpaka familia unakuta watoto wamemfata mama wengine baba hizo mambo ziacheni ni ndugu mmoja tu ninyi Wazungu na Waarabu walikuja kuwatenganisha nanyi mmechukua Copy zao..
 
Umeuliza tunakujibu hutaki! Sasa kama ulikuwa na majibu yako umeuliza ili iweje?Waislamu tunahudhuria misiba ya mtu yeyote isipokuwa kwenye ibada hatushiriki,wakiumwa tunakwenda kuwajulia hali iwe nyumbani au hospitali, wakitukaribisha chakula tunakula ili mradi viwe halali kwa mujibu wa dini yetu na ikitokea amekudanganya na wewe hukubaini yeye ndiye atakayepata dhambi na ataadhibiwa na Mwenyezi Mungu, yaani kwa kifupi hakuna katazo lolote katika kushirikiana na asiye Muislamu ili mradi lisiwe ni jambo la kumuasi Mwenyezi Mungu.
Usikurupuke mkuu, mimi nimeuliza nini
Pia huko kushiriki misiba wa ukristo umetoa ktk Sunnah au quraan,
Pia kushiriki huo msiba bila ya ibada zao thubutu, kimsingi uislamu wa sasa ni ule alio uhusia mtume, hizi ni dalili za kiyama , kila haramu itaoneka ni kawaida, kama pombe, kamari, zinaa nk
Uislamu sio jina wala kanzu bali ni kufuata misingi sahihi ya dini

Hawata kuwa radhi mayahudi na manaswara mpaka mfate mila zao
 
Kwahiyo hilo uliloleta siyo swali! Haya sheikh.
 
Back
Top Bottom