Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
JE NI LAZIMA KUMSAMEHE MZAZI ALIYEKUTELEKEZA?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Jibu la moja kwa moja kwa wale wasiopenda Maelezo marefu.
Jibu sio Lazima Kumsamehe mzazi au mtu yeyote aliyekukosea.
Msamaha sio lazima.
Msamaha ni moja ya vipengele muhimu katika UPENDO.
Upendo ni hiyari.
Msamaha ni hiyari.
Kwa sisi Watibeli Msamaha sio Haki. Msamaha ni Neema. Neema ni Upendo.
Ikiwa mzazi alikutelekeza ukiwa mtoto, ni kawaida kabisa kuwa na maumivu, hasira au maswali.
Na katika hayo Hakuna anayepaswa kukulazimisha usamehe au urejee kwenye uhusiano ambao bado unaumiza. Uhusiano unaokunyima furaha.
Sisi Watibeli Maisha sio Gereza. Jambo lolote. Nasisitiza lolote lile linalotunyima furaha au kutupa maumivu na huzuni, tunaliweka pembeni.
Kama Ukichagua kusamehe, haimaanishi:
kwamba alichofanya kilikuwa sahihi;
kwamba lazima umruhusu arudi kwenye maisha yako kwa kiwango kilekile;
wala kwamba umesahau yaliyotokea.
Na ukihitaji kuweka mipaka ili kujilinda, hilo pia linaweza kuwa jambo la busara.
Msamaha sio lazima.
Jamii isiwape mzigo watoto waliotelekezwa mzigo mwingine wa kuwalazimisha kuwasamehe wazazi wao.
Unakuta watu wanakuambia huyo ni Mamaako/ Babaako unapaswa au lazima umsamehe.
Watoto wanajikuta na kujiona wabaya zaidi kwa kuona wao wanashindwa kusamehe ilhali sio lazima.
Huwezi kuonekana mbaya kwa kushindwa kusamehe. Msamaha ni hiyari.
Huwezi kuonekana mbaya kwa jambo ambalo ni hiyari yako kufanya.
Ubaya unakuja pale unaposhindwa kufanya wajibu na majukumu yako.
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam