Joshua Mbezi
JF-Expert Member
- Oct 18, 2024
- 1,994
- 4,446
Katika halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera vipo vijiji ndani ya kata za Isingiro,Kaisho,Rutunguru Rubwera nk
Hizi ni kata ambazo zimepakana na nchi za Rwanda pamoja na Uganda
Huwapo ndani ya hizi kata mitandao ya mawasiliano ya simu ni shida kiasi kwamba ukiingia tu unaanza kukaribishwa na Sms kutoka mitandao ya nchi jirani (Rwanda) % kubwa ya taarifa utazopokea zitakuwa katika lugha ya kinyarwanda au kifaransa
Ndani ya maeneo hayo usikivu wa redio za Tanzania ni changamoto sana redio zinazosikika zaidi ni kinyarwanda pamoja na kinyankole
Tunaomba serikali iangalie namna ya kutatua changamoto hizo kwa kuboresha mawasiliano ya simu pamoja na redio ili kuwapa wananchi fursa ya kujua yanayojiri ndani ya nchi yao.