Kwani akienda motoni wewe utakosa wewe utakosa pepo au ni vipi?
Mana Kwenye uislam ni wazi kuwa hakuna mtu anayechukua dhambi ya mtu mwingine?
Ukiwasikiloza wanazuoni wa kiislmu utaweza kudhani kuwa uislam unawahamasisha watu kuhusu maisha ya ahera zaidi lakini ukweli ni kwamba uislam unapigania maisha ya dunia zaidi kuliko ya ahera.
Na mbaya zaidi Waarabu wamefanikiwa sana kuwadanganya watu kuwa ukifa ukiwa unapigania mila zao na dini yao utaenda peponi. Lakini hii dhana inachochewa zaidi kwa maskini lakini matajiri na watawala kamwe hawajitoi kufa kwa ajili ya dini ya uislam badala yake wanapambania maslahi yao yaa kiuchumi na kisiasa. Ukimuona mtawala au mfanyabiashara wa dini ya kiislam mwenye mrengo na itikadi za kidini mara nyingi anachochea na hata kutoa mapesa mengi kwa vijana maskini ili wajitoe muhanga lakini sio watoto wake wala yeye mwenyewe ,sasa tunajiuliza inamaana yeye hataki kwenda peponi kula raha kubwa kuliko za dunia !!
Kifupi ni kwamba dhana ya ugaidi na ugaidi inatengenezwa na watawala na matajiri wa dunia kwa malengo ya kisiasa na biashara zao.
Hakuna kijana anayetokea familia maskini anayeweza kumiliki Silaha za moto kama SMG , rocket launcher, hand grenade, pistol , na risasi kwa maelfu na kukaa porini akiwa anafundishwa mbinu za kivita.
Ni wazi kuwa nyuma yake kuna watu wenye nguvu za kisiasa na kiuchumi.
Na kama ni ishu zisizohuisiana na uislama basi tungeona vijana hao wakiwa watu wa dini tofauti kama inavyokua kwenye uhalifu mwingine kama ujambazi.
Na ukichunguza zaidi utahundua kuwa sehemu zote zenye ugaidi kuna kuwa na matajiri wa kubwa sana wanye asili ya Asia . Hawa mara nyingi ndio wanaotumika kupokea na kusambaza fedha na zana za kigaidi kwa magaidi.
Uislam sio ugaidi ila Bado kuna mivutano mikubwa ya kiuchumi kati ya nchi za magharibi na nchi za Kiarabu katika kuteka uchumi na soko la Afrika Kinachofuata ni Wazungu kutumia mbinu za mauaji ya kisayansi kupitia wanasiasa na wataalam kwenye masuala ya madawa nk. Lakini Waarabu wanatumia mbinu za kubadili waafrika wengi kufuata itikadi zao ,mila zao na dini zao .Na kuwajenga kisaikolojia kuwa katika itikadi za dini maisha yatakua mazuri na ya haki kwa kila mtu wa dini inayofanana na ya kwao . Kwa sasa waafrika wanalengwa zaidi kutokana na ukosefu wa ajira na elimu duni na umaskini na kukosekana kwa Demokrasia ya kuchagua viongozi bora kwa kufuata sera za kitaifa . Ndio maana wakati mwingine kunapokaribia uchaguzi unagundua kuwa panakua na kampeni zinazogubikwa na hisia za kidini na maneno makali ya kuchochea na kutishana yote ni kwa manufaa ya wanasiasa na matajiri kutoka nje.
JPM alidhibiti ugaidi kwa kuzuia pesa zote kutoka nje kwa sababu kwa kipindi kirefu palikua na mapesa mengi sana yaliyokuwa yanaletwa kutoka nje ya nchi.
Msingi wa Ugaidi ni Chuki zinazotokana na itikadi za kidini ndani ya siasa kwa dhana potofu na tafsiri potofu za kidini.
Mfano tunaonewa kwa sababu sisi ni wa dini fulani wakati huo huo karinu nusu ya wanye nafasi za juu serikalini ni wa dini hiyo hiyo . Sasa unajiuliza hapa hoja ni dini kweli au kuna jambo lingine nyuma yake ? Ishu inakua ni madaraka na maslahi binafsi na dini ni chambo tu kilichotumiwa ili kupata uungwaji mkono.
Dunia imejaa watu wenye kiburi mithili ya Shetani ambaye alidhani kuwa yeye anapemdwa na Mwemyezi Mungu kuliko wemgine wote kutokana na kushika sana dini matokeo yake akafeli mtihani mdogo sana wa kumsujudia Adam.
Hata leo kuna watu wanaojiona kuwa wao pepo ni ya kwao kwa sababu tu eti wana swali sana au wanafunga sana au wanahiji sana.
Wameshahu Rehema za mwenyezi Mungu ni kwa kila anayejinyenyekesha mbele ya Mwenyezi Mungu.
Pepo ameiandaa Mungu mwenyewe halafu tunaigombania na kuuana ili kuipata wakati hatijui hata gharama ilipo na ilivyojengwa na gharama zake .