Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Kama haukuwa mtoto wa geti kali lazima michezo mingi ya utotoni utakuwa unaikumba binafsi nilikuwa napenda michezo mitatu tu ambayo ni;

1. Michezo ya vita hapo unaashumu wewe ni Rambo ukiwa na bunduki ya mabomba ya mipapai.

2. Komborela

3. Mpira huku magoli yakiwa ndala au mawe.

Je, wewe ulikuwa unapenda michezo gani?
Ngumi za wakati wa kutoka shule na siku ya kufunga shule. Mimi sikuwa na ubavu ila nilikuwa promota mkuu wa hizi ngumi na nikichonganisha lazma zipigwe tu. Tulikuwa na shule nyingine ya msingi jirani, basi watukutu wote wa kule walikuwa wanaijua kazi yangu na akipatikana mbabe kule lazima nijuzwe nimtafutie mbabe mwenzake kwetu wazichape jioni mojawapo.
 
IMG_20170318_181437.jpg
IMG_20170318_181259.jpg


Chandimu hiyo omba mungu usiwekewe bambiko au upige domaa au dochii halafu uchimbe chini
 
Back
Top Bottom