Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngumi za wakati wa kutoka shule na siku ya kufunga shule. Mimi sikuwa na ubavu ila nilikuwa promota mkuu wa hizi ngumi na nikichonganisha lazma zipigwe tu. Tulikuwa na shule nyingine ya msingi jirani, basi watukutu wote wa kule walikuwa wanaijua kazi yangu na akipatikana mbabe kule lazima nijuzwe nimtafutie mbabe mwenzake kwetu wazichape jioni mojawapo.Kama haukuwa mtoto wa geti kali lazima michezo mingi ya utotoni utakuwa unaikumba binafsi nilikuwa napenda michezo mitatu tu ambayo ni;
1. Michezo ya vita hapo unaashumu wewe ni Rambo ukiwa na bunduki ya mabomba ya mipapai.
2. Komborela
3. Mpira huku magoli yakiwa ndala au mawe.
Je, wewe ulikuwa unapenda michezo gani?