Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Je, ni mchezo gani utotoni ulipenda kucheza na wenzako?

Wakuu nani anakumbuka MPUTO?? Ule ambao unapinga na mtu atakaekutwa na kitu mkononi kinaputwa puu, unabaki kulamba vidole tuu[emoji23] [emoji23]
 
Utoto mtu unanunua bigijii, kabla hata hujapokea toka kwa muuza duka tayari marafiki zako 10 washanyoosha mikono kuomba... Sasa huo mgao wake!!! Mpaka kila mtu anapata! [emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] afu nakumbuka kulikuaga na ile "hakiombeki"
Mtu anannua kitu afu anakuwahi hakiombeki
 
Au mputo! Watu tulikua tunaputana nyama mezani
[emoji28] [emoji28] ukiputwa kitu chako ilikua inauma kinoma, ila siku na wewe ukimuotea mtu raha sana. Mda wa pumziko wengi ndo walikua wanakomeshwa
 
Paprika 'ganda'...
Aya 'ganduka'... [emoji3][emoji3]
Hahaha! Alafu ndo ukute unafanya kitu cha maana! Ivi huu ndo ulikua unatakiwa ukunje vidole viwili ili ukiambiwa ganda unaonesha hivyo vidole basi hutakiwi kuganda!!!
 
Hahaha! Alafu ndo ukute unafanya kitu cha maana! Ivi huu ndo ulikua unatakiwa ukunje vidole viwili ili ukiambiwa ganda unaonesha hivyo vidole basi hutakiwi kuganda!!!
Hahahaaa, ndo huo mkuu. sijui hata nani alikua ni mwanzilishi wa hizo kanuni mpaka zikasambaa sehemu kibao
 
Mkuu hiyo ni kula mbakishie baba
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mchanga ukibaki kidogo mwisho mwisho watu wanakula kidogo kidogo
dah huu mchezo kipindi Niko standard 4 siku ya jumamosi nilikuwa nimeenda twisheni mida ya saa 3 asubuhi sasa nikakuta wenzangu wanacheza wamebakiza kidogo tu kamti kadondoke sasa kile kimbelembele nikijua na mbio sana nikakandondosha kale kamti sikufika mbali aisee wakanikamata nilipigwa hadi nikajuta kucheza aisee.
 
Hahahahahaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
dah huu mchezo kipindi Niko standard 4 siku ya jumamosi nilikuwa nimeenda twisheni mida ya saa 3 asubuhi sasa nikakuta wenzangu wanacheza wamebakiza kidogo tu kamti kadondoke sasa kile kimbelembele nikijua na mbio sana nikakandondosha kale kamti sikufika mbali aisee wakanikamata nilipigwa hadi nikajuta kucheza aisee.
Haahaaaaa michezo yetu hiyo mnatengeneza ugali wavumbi then unaweka kamti duu.. Doba ngumi nimemiss hizo
 
dah huu mchezo kipindi Niko standard 4 siku ya jumamosi nilikuwa nimeenda twisheni mida ya saa 3 asubuhi sasa nikakuta wenzangu wanacheza wamebakiza kidogo tu kamti kadondoke sasa kile kimbelembele nikijua na mbio sana nikakandondosha kale kamti sikufika mbali aisee wakanikamata nilipigwa hadi nikajuta kucheza aisee.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Enzi hizo suruali za biokti ilikuwa stori ya mjini
Na viatu vya HB sijui!!! Bonge la buti... Ata kunyanyua mguu mtoto wa kike ilikua shida! Basi najiona mbabe mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ambaye amezaliwa kipindi hiki anashangaa shangaa tuu huu uziii
dah kweli lazima washangae kama huku kwetu watoto wadogo kabisa hawajui chochote zaidi ya mziki tu
 
Hatari ilikuwa huu mchezo wa msingi bomoa. Yaani ukipinga na siku akikubamba umeinama unakula buti moja tu hatareeee
huu mchezo ulikuwa mbaya sana kama mtu unahasira yani ukiinama imekula kwako hiyo.
 
Kabisa!
Hii michezo saizi imepotea kabisa.

Mimi nimecheza karibia michezo yote,ukuti ukuti,Baba na mama,kombolera,"Senta",kubwa zaidi ambalo halitafutika kwa ubongo wangu-Nikiwa na miaka kama sita hivi tulifungishwa ndoa mimi na binti mmoja (kwakweli alikuwa anamuonekano uliobora na wakuvutia) ilifanyika sherehe moja matata sana ambayo ilipangwa na rika letu tu, mimi na suti na yeye na shela haha Mtaa mzima ulizizima mpaka watu wazima walipigwa na butwaa.

AISEE nikiikumbuka siku hii huwa nacheka mwenyewe moyoni,binti huyo hata Sijui yuko wapi Manaake Familia zilitawanyika.
yani mkiwa watoto mnzani hamtoachana kumbe ni kudanganyana tu
 
Back
Top Bottom