Je, ni Morocco watakaovunja rekodi ya kufika Semi's?

Je, ni Morocco watakaovunja rekodi ya kufika Semi's?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kwenye Cup Competitions unahitaji zaidi defense; unaweza ukawa timu mbovu ila kama una discipline na unapaki basi matuta yanaweza yakakufikisha mbali.

Sasa huyu Kocha tangia achukue timu hapo 2nd September; Hajafungwa Goli hata Moja.... (5 Clean Sheets).

Belgium 0 - 2 Morocco; Morocco 0 - 0 Croatia; Morocco 3 - 0 Georgia; Paraguay 0 - 0 Morocco; Morocco 2 - 0 Chile.

Na unajua kwenye round ya mitoano usipofungwa basi lazima utapita tu....; Kwahio Je wataweza kufika pale ambapo Ghana, Senegal na Cameroon walishindwa kufika kwa bahati mbaya na kwa kucheza vizuri..., kwa wao kuhakikisha wana discipline?
 
Ni kanuni...mwenye nacho ataongezewa.
Hivyo Morocco ameonyesha ubora amejiongezea washabiki.
Twende naye
Sidhani kama ameonyesha Ubora timu zilizopita nyingine za Africa zilizofika Last 8 zilikuwa zinacheza mpira wa kuvutia na attacking na zote zilitoka kwa bahati mbaya Camerooun vs England (kwa penati mbili na walitoka kwenye extra time 2-3) Senegal alifungwa na Uturuki bao Moja na Ghana alifungwa kwa Penati baada ya Suarez Kujifanya kipa...

Kwahio tumeshindwa kwa kucheza All out Attacking huenda ni Wakati wa Kushinda kwa ku-Play Ugly (Defensive Minded)
 
Bahati mbaya ubora au ushindi wa soka unaamuliwa na magoli, hata kama timu itajifunga yenyewe mpinzani anapewa ushindi.

Ubora na ushindi hauko ndani ya uwanja bali golini mkuu kwa eidha kuzuia usifungwe au kufunga basi
 
Hivi unajua kwanini Brazil ni ina mashabiki wengi duniani na kwa kipindi kirefu ingawa Ujerumani nayo ina Rekodi nzuri watu walikuwa wanaichukia?

Ingawa Football ni Results pia ni Entertainment ukiwa kama Jose Mourinho, na kila mtu akicheza hivyo watu wataacha kutazama mpira
 
Sidhani kama ameonyesha Ubora timu zilizopita nyingine za Africa zilizofika Last 8 zilikuwa zinacheza mpira wa kuvutia na attacking na zote zilitoka kwa bahati mbaya Camerooun vs England (kwa penati mbili na walitoka kwenye extra time 2-3) Senegal alifungwa na Uturuki bao Moja na Ghana alifungwa kwa Penati baada ya Suarez Kujifanya kipa...

Kwahio tumeshindwa kwa kucheza All out Attacking huenda ni Wakati wa Kushinda kwa ku-Play Ugly (Defensive Minded)
Sio lazima kila mtu apite njia moja ya mafanikio. Kwa style yao iyo iyo akiwa na nidhamu anaweza akafika mbali zaidi ya hao wengine
 
Duh huenda Safari ikafikia Kikomo.....

Wakipenya ni either German au Spain....

Nadhani ni Bora iwe German sababu wakimfunga huyo ni either Portugal / Swiss alafu huenda ikawa France then Fainali

Ni mwendo wa discipline na Defense..., Matuta all the Way...
 
Ficha ujinga wako

Ka sare na crotia mshindi wa pili wa world cup

Kampiga number 4 wa FIFA RANKING

Nani wa kumshindwa?
Aisee !!!!! Duh!!!!!!

Kwahio Senegal 2002 alivyomfunga France ingebidi achukue Kombe la Dunia ? (Sio Sare bali alimfunga Kabisa)

Au unadhani mpira ni kama Draft au Chess ukimfunga huyu basi unawazidi wote waliofungwa nae...
 
Kwani ufaransa ilikuwa na nini?

Asa kama senegal alimfunga ufaransa ile

Mbona morroco imekifunga kizazi cha dhahabu cha Beligimu?

Nakwambia morroco hakuna team ya kumtisha
 
Kwani ufaransa ilikuwa na nini?
Umesema Croatia iliingia Fainali World Cup iliyoisha Nakwambia Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia let alone kufika Fainali na wakiwemo kina Zidanne
Asa kama senegal alimfunga ufaransa ile
Unajua ile France ilikuwa na kina nani ?
Mbona morroco imekifunga kizazi cha dhahabu cha Beligimu?
Hicho kizazi kimefanya nini mpaka sasa ?
Nakwambia morroco hakuna team ya kumtisha
Cup competition haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani unaweza ukawa timu mbovu ukachukua Kombe la Dunia au Cup Competition yoyote ile..., na mimi nimeanzisha huu uzi nikisema hivyo Morocco wanaweza kufika mbali sio kwa kuwa na timu mahili bali kwa kuwa na discipline imeshaweka clean sheets kama tano au sita tangia huyu kocha achukue timu....

Ila ukikutana na timu ambazo zinaweza ku-unlock defense na individual brilliance ni ngumu kuliko otherwise..., Pia World Cup inategemea bahati unaweza ukakuta na vibonde mpaka fainali; lakini German na Spain sio Vibonde...
 
Umesema Croatia iliingia Fainali World Cup iliyoisha Nakwambia Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia let alone kufika Fainali na wakiwemo kina Zidanne

Unajua ile France ilikuwa na kina nani ?

Hicho kizazi kimefanya nini mpaka sasa ?

Cup competition haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani unaweza ukawa timu mbovu ukachukua Kombe la Dunia au Cup Competition yoyote ile..., na mimi nimeanzisha huu uzi nikisema hivyo Morocco wanaweza kufika mbali sio kwa kuwa na timu mahili bali kwa kuwa na discipline imeshaweka clean sheets kama tano au sita tangia huyu kocha achukue timu....

Ila ukikutana na timu ambazo zinaweza ku-unlock defense na individual brilliance ni ngumu kuliko otherwise..., Pia World Cup inategemea bahati unaweza ukakuta na vibonde mpaka fainali; lakini German na Spain sio Vibonde...
Ujinga mtupu
 
Argentina wakati wanatetea taji mwaka 1990 hawakuwa wazuri na mechi ya ufunguzi walipigwa na Cameroon 1-0, Cameroon wakicheza na wachezaji 9 tu uwanjani.

Lakini ndio hivyo Argentina walicheza hadi fainali na kutolewa kwa bao la penalti feki waliyopewa Ujerumani.

Hata mwaka 1994 Italia hawakuwa wazuri baada ya kufungwa 1-0 na Ireland ktk mechi ya ufunguzi lkn walifika fainali na kutolewa kwa matuta na Brazil.

Hata mwaka 2002 Ujerumani ilikuwa na timu mbovu kabisa iliyochapwa 3-1 na Croatia kwenye makundi lakini walifika fainali na kufungwa na Brazil 2-0 kwa mabao ya Ronaldo de Lima.

Na hata Italia 2006 na Spain 2010 walianza vibaya kwa kupoteza mechi za mwanzo lakini mwisho wa mashindano waliibuka na kombe.

Kwenye kombe la dunia waga kuna maajabu sana kwa zile timu 8 zilizowahi kulitwaa hilo taji, yeyote anaweza akaibuka bingwa wakati kimpira hayuko kwenye form.
 
Imeloa Sio Kombe la Dunia tu.., ni kwamba Cup Competition kushinda haimaanishi wewe ni bora bali inategemea na bahati pia unaokutana nao kitu cha kupima ubora ni ligi..., pia kwenye haya mambo defense ni muhimu zaidi...

2006 timu bora kabisa ilikuwa Argentina; (ambao hawakushinda) wakiwa na mtaalamu wao Juan Román Riquelme.... Huku Messi akitoka akiwa Bench...

Tujikumbushe goli lao ambao lilipatikana baada ya pasi 24
 
Hivi unapata wapi ujasiri wa kuifananisha morocco na kitaifa stars!!

Kwa sasa morocco ndie wakutuwakilisha japo senegal na ghana wamepata matokeo mazuri, lakini kimpira morocco is the best.
Duh hivi tunaelewana lakini ?!!!

Jamaa kasema Morocco anaweza kumfunga mtu yoyote ndio nikamjibu kwenye karatasi hata Taifa Stars anaweza kufanya hivyo..., Ni kama ambavyo realistically kwa Saudi Arabia Kumfunga Argentina ni ni ngumu hata wakirudiana huenda mechi ikawa tofauti ila iliwezekana...

Au wenzangu hamjui maana ya kuwezekana ? (Mathematically hata wewe na familia yako unaweza kuwafunga Brazil) ingawa realistically its something else....

Na unaongelea Kimpira Morocco is the Best ? Statistically Senegal ndio Mabingwa wa Africa.... na kwenye ligi huenda Morocco asitoboe ila kwenye mituano Defense bora ni zaidi ya uwezo wa kufunga..., (Hapa hakuna point tatu ni unafungwa unaondoka).....
 
Back
Top Bottom