Ituzaingo Argentina
JF-Expert Member
- Jun 20, 2020
- 1,868
- 2,191
Argentina wakati wanatetea taji mwaka 1990 hawakuwa wazuri na mechi ya ufunguzi walipigwa na Cameroon 1-0, Cameroon wakicheza na wachezaji 9 tu uwanjani.
Lakini ndio hivyo Argentina walicheza hadi fainali na kutolewa kwa bao la penalti feki waliyopewa Ujerumani.
Hata mwaka 1994 Italia hawakuwa wazuri baada ya kufungwa 1-0 na Ireland ktk mechi ya ufunguzi lkn walifika fainali na kutolewa kwa matuta na Brazil.
Hata mwaka 2002 Ujerumani ilikuwa na timu mbovu kabisa iliyochapwa 3-1 na Croatia kwenye makundi lakini walifika fainali na kufungwa na Brazil 2-0 kwa mabao ya Ronaldo de Lima.
Na hata Italia 2006 na Spain 2010 walianza vibaya kwa kupoteza mechi za mwanzo lakini mwisho wa mashindano waliibuka na kombe.
Kwenye kombe la dunia waga kuna maajabu sana kwa zile timu 8 zilizowahi kulitwaa hilo taji, yeyote anaweza akaibuka bingwa wakati kimpira hayuko kwenye form.
Tatizo la watanzania wengi wao hawapo kimpira, mahaba yamewazidi.