Umemchambua vizuri kabisa.Hakuna kitu ambacho ni cha moja kwa moja.Muda wakati ni mwamuzi wa mambo mengi.
Zile siasa za ubabe ubabe na uwekezaji mkubwa katika masuala ya ulinzi zinakwenda kubadilika kadri muda unavyosonga mbele.
Rwanda ina maadui wawili wakubwa ambao katika kipindi chote cha Utawala wa PAKA ameshindwa kuyadhibiti.
Adui Number moja yupo ndani.Ukabila ambao upo kwasababu za kihistoria.Bahati mbaya PAKA kaukuza na kuutukuza ukabila katika kipindi chote cha Utawala wake.Kabila lake la Tutsi ndio kila kitu huko Rwanda na kibaya zaidi anaamini sana katika himaya ya Bahima.
Tatizo la pili linazalishwa na tatizo la kwanza.PAKA ana amini makabila yote yenye asili ya Tutsi wana uhalali wa kutawala eneo lote la maziwa makuu.Alianzisha operation ya kuwatumia watutsi bila kujali wanatoka nchi gani,matokeo yake waangaza wa Tanzania au banyamulenge wa Congo wakaanza kukosa uhalali au kuaminika katika nchi zao za asili.
PAKA anajikuza sana kuliko uhalisia wa nchi yake ndogo ya Rwanda ambayo inazidiwa ukubwa wa eneo na hifadhi ya taifa ya Serengeti.Mkubwa wa hifadhi ya Serengeti ana tawala eneo kubwa kuliko nchi ya Rwanda.PAKA hawezi kuwa sawa na Rais wa Tanzania lakini hizo kelele mbwembwe utafikiri Rwanda labda ni Russia kila mahali penye ugomvi atapeleka wanajeshi wake wa kitutsi.Akienda Ulaya atasign mikataba ya kuchukua wakimbizi wakati Rwanda ni nchi ya tatu duniani kwa msongamano wa watu.
Wakati wa PAKA kuondoka unazidi kukaribia mbegu yake akiyoipanda ya ukabila ndio itakayomwondoa mapema zaidi.
Kujivimbisha kote alikokuwa akikufanya alitegemea 'sponsors'; sasa na wao wamegundua uchizi alionao na kumwambia wazi juu yake.
Yule mzee wa Hotel Rwanda kalazimishwa kumwachia huru.