Je, ni nini Yesu alimaanisha?

Je, ni nini Yesu alimaanisha?

ulimi waupanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
493
Reaction score
1,223
Wakuu napata shida sana pale nikitafakari kauli ya yesu kwa wanafunzi wake, kuwa '" NENDENI MKAYABATIZE MATAIFA YOTE KWA JINA LA BABA, LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU"
Shida naipata hapa, je baba ni jina? Kama siyo jina alimaanisha jina gani?
ii) Mwana ni jina? Kama siyo ni lipi alimaanisha?
iii) Roho mtakatifu ni jina? Kama siyo jina ni jina gani alimaanisha?

Mimi kwa uelewa wangu naona baba, mwana na Roho mtakatifu ni vyeo au sifa lakini siyo majina, sasa napata shida kwanini wakati wa kubatiza wachungaji/ mapadre wanataja ivyo vyeo badala ya kutaja majina ambayo Yesu alitaka?
Mfano: Ukiagizwa kwamba kwa jina la Raisi wa Tanzania peleka barua hii, ukifika kule ulikoagizwa utasema kuwa:
I) Kwa jina la Raisi ya Tanzania nalileta barua hii? Au
ii) Kwa Mamlaka ya JPM, Raisi wa Tanzania nalileta barua hii?

Tafadhali mwenye mwanga kidogo
juu ya hii kauli ya Yesu kwa wanafunzi wake atupatie ufafanuzi.

Ahsanteni!
 
Jina la Baba wa Yesu ni Yesu, maana yake ni kwamba Yesu alipokuwa hapa duniani alitumia jina la baba, kwa hiyo basi baba na mwana wanatumia jina moja, ila sijajua kwa roho mtakatifu jina lake ni lipi.
 
Baba ni Sifa sio jina,
Mwana ni sifa pia,
Roho Mtakatifu ni Jina, na sifa yake ni Msaidizi wetu.
Kwani hukielewi kiswahili ?
 
Baba=Jehovah
Mwana=Yesu
Roho mtakatifu ndo jina lake hilo, sifa yake ni msaidizi kama Che mittoga alivyoeleza.
Niko tayari kurekebishwa.
 
Wakuu napata shida sana pale nikitafakari kauli ya yesu kwa wanafunzi wake, kuwa '" NENDENI MKAYABATIZE MATAIFA YOTE KWA JINA LA BABA, LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU"
Shida naipata hapa, je baba ni jina? Kama siyo jina alimaanisha jina gani?
ii) Mwana ni jina? Kama siyo ni lipi alimaanisha?
iii) Roho mtakatifu ni jina? Kama siyo jina ni jina gani alimaanisha?

Mimi kwa uelewa wangu naona baba, mwana na Roho mtakatifu ni vyeo au sifa lakini siyo majina, sasa napata shida kwanini wakati wa kubatiza wachungaji/ mapadre wanataja ivyo vyeo badala ya kutaja majina ambayo Yesu alitaka?
Mfano: Ukiagizwa kwamba kwa jina la Raisi wa Tanzania peleka barua hii, ukifika kule ulikoagizwa utasema kuwa:
I) Kwa jina la Raisi ya Tanzania nalileta barua hii? Au
ii) Kwa Mamlaka ya JPM, Raisi wa Tanzania nalileta barua hii?

Tafadhali mwenye mwanga kidogo
juu ya hii kauli ya Yesu kwa wanafunzi wake atupatie ufafanuzi.

Ahsanteni!
Ndugu yangu hii falsafa ya kiyunani inaweza kukuchanganya ila ukweli ndio huu.Kila mtu ana tafsiri yake
 
hata kama nimekubali kurekebishwa sio sababu ya kunidanganya kama kitoto,Mungu mwenyewe kwenye Biblia anasema jina lake ni Jehovah(Yahweh) hata manabii kwenye Biblia wameandika jina la Mungu ni Jehovah.
hata kama nimekubali kurekebishwa sio sababu ya kunidanganya kama kitoto,Mungu mwenyewe kwenye Biblia anasema jina lake ni Jehovah(Yahweh) hata manabii kwenye Biblia wameandika jina la Mungu ni Jehovah.[/QUOTnipe hilo andiko mungu kasema jina lake ni yehova
musa alimuuliza unaitwa nani hakusema anaitwa jehova au Mungu ana majina mangapi mkuu
 
Kutoka 6:3
Isaya 42:8
Inaonekana hausomi Biblia.
Mungu anamwita Mose
2 Mungu akamwambia Mose, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu. 3Nilimtokea Abrahamu, Isaka na Yakobo nikijulikana kama Mungu Mwenye Nguvu, ingawa kwa jina langu, Mwenyezi-Mungu, sikuwajulisha.
 
Exodus 6:3. : “I used to appear to Abraham, Isaac and Jacob as God Almighty, but as respects my name Jehovah I did not make myself known to them.”

Isaiah 42:8
8 I am Jehovah. That is my name;I give my glory to no one else,*Nor my praise to graven images.
Ndugu yangu huwa sikuelewi kabisa sababu uko vizuri sana kwenye Bible lakini unapinga uwepo wa huyu Mungu wa kwenye Biblia!
Were you once a good christian?
 
Mungu anamwita Mose
2 Mungu akamwambia Mose, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu. 3Nilimtokea Abrahamu, Isaka na Yakobo nikijulikana kama Mungu Mwenye Nguvu, ingawa kwa jina langu, Mwenyezi-Mungu, sikuwajulisha.
shida ipo kwenye aina ya Biblia unayosoma,inawezekana unasoma Biblia ya kikatoliki ambayo haitaji jina Yehovah bali mwenyezi Mungu.
Kasome King James,hata Biblia za kiebrania zimetaja jina Yahweh.
Usinitaabishe kwa vitu vidogo.
 
Wakuu napata shida sana pale nikitafakari kauli ya yesu kwa wanafunzi wake, kuwa '" NENDENI MKAYABATIZE MATAIFA YOTE KWA JINA LA BABA, LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU"
Shida naipata hapa, je baba ni jina? Kama siyo jina alimaanisha jina gani?
ii) Mwana ni jina? Kama siyo ni lipi alimaanisha?
iii) Roho mtakatifu ni jina? Kama siyo jina ni jina gani alimaanisha?

Mimi kwa uelewa wangu naona baba, mwana na Roho mtakatifu ni vyeo au sifa lakini siyo majina, sasa napata shida kwanini wakati wa kubatiza wachungaji/ mapadre wanataja ivyo vyeo badala ya kutaja majina ambayo Yesu alitaka?
Mfano: Ukiagizwa kwamba kwa jina la Raisi wa Tanzania peleka barua hii, ukifika kule ulikoagizwa utasema kuwa:
I) Kwa jina la Raisi ya Tanzania nalileta barua hii? Au
ii) Kwa Mamlaka ya JPM, Raisi wa Tanzania nalileta barua hii?

Tafadhali mwenye mwanga kidogo
juu ya hii kauli ya Yesu kwa wanafunzi wake atupatie ufafanuzi.

Ahsanteni!
baba ni mungu mwana ni yesu na roho mtakatifu ni msaidizi wa yesu baada ya yesu kwenda mbinguni kwa ufupi hizo ni nafsi tatu za utatu mtakatifu
 
Back
Top Bottom