Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF, Richard Mbaruku akisoma uamuzi wa Kamati yake katika Rufaa aliyokata aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara, amesema mtuhumiwa alikuwa na makosa mawili na uamuzi wa rufaa kwa kila kosa umebaki hivyo hivyo kama ifuatavyo:
1) Offensive behavior - kufungiwa miaka miwili na sh. 10M
2) Tabia ya vitisho - kufungiwa miaka miwili na sh. 10M
Lakini kuhusu utekelezaji wa adhabu hizo, adhabu za faini ya sh. 10M kwa kila kosa nayo imetajwa kuwa zitaenda sambamba kwa pamoja kwa makosa yote mawili, hivyo mkata rufaa atalipa sh. 10M tu.
Mimi hoja yangu ninaielekeza upande wa faini, sio wa muda wa kutofanya kazi ya kimichezo. Swali langu ni hili: Je, ni sahihi adhabu za faini kwa kila kosa kutoka katika makosa mawili tofauti kwenda sambamba na hivyo kuwa kama faini ya kosa moja tu?