Soma hii sehemu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2005) inavyosema hasa kifungu kidogo cha 3(a). Huenda ukapata jibu.Nawauliza watu wa itifaki kama ni halali kwa kipindi hiki cha mpito kumtambulisha Waziri mkuu wa awamu ya 5 Mh Kassim Majaliwa kama Waziri Mkuu Mstaafu.
Naomba majibu Tafadhali.
Maendeleo hayana vyama!
SEHEMU YA TATUWAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI
Waziri Mkuu
51(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi- (a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake; au (b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au (c) siku atakapojiuzulu; au (d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu; au (e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu wa masharti mengineyo ya Katiba hii.