Je, ni sahihi kumtambulisha Kassim Majaliwa kuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu?

Je, ni sahihi kumtambulisha Kassim Majaliwa kuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu?

Kwahiyo nini tofauti ya former President/Prime minister na retired President/Prime minister?

Naomba tafsiri ya kiswahili tafadhali.
Former President or PM kwa kiswahili ni Rais wa zama au Waziri Mkuu wa zamani.

Retired President ni Rais mstaafu.

Kwa maoni yangu Kiongozi pekee ambaye angestahili kuitwa mstaafu kama angekuwa Hai ni Nyerere kwa kuwa aliondoka madarakani kwa kustaafu. Wengine waliofuata waliondoka kwa vipindi vyao kuisha kwa mujibu wa katiba.
 
Kustaafu maana yake hukufukuzwa au kuachishwa au kujiuzulu, muda wako ulifika kikomo. Kwa wafanyakazi ni 60 yrs, 55,yrs kwa hiari. Kwa awaziri, wabunge 5 yrs.
 
Nawauliza watu wa itifaki kama ni halali kwa kipindi hiki cha mpito kumtambulisha Waziri mkuu wa awamu ya 5 Mh Kassim Majaliwa kama Waziri Mkuu Mstaafu.

Naomba majibu Tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
Hii ni dalili ya wazi kuwa hatamchagua tena kuwa waziri mkuu.
 
Kwahiyo nini tofauti ya former President/Prime minister na retired President/Prime minister?

Naomba tafsiri ya kiswahili tafadhali.
Former President -- Rais Msabiki
Retired Prime Minister -- Waziri Mkuu Mstaafu
 
Nimeangalia tena ibara ya 50, kama Makamu wa Rais tofauti hajaapishwa, yule wa awali anaendelea kuwa Makamu wa Rais.

Yani hata kama Tundu Lissu angeshinda, Magufuli angekuwa Rais na Samia angekuwa Makamu wa Rais mpaka Lissu na Makamu wake wanapoapishwa.

Hii ni kuzuia "power vacuum".

Nchi haitakiwi kukaa hata siku moja bila Rais na Makamu wake.
Kudos kwa mfano mzuri, ila kamwe usiweke jina la Mr Mzungu na cheo cha Urais kwenye sentensi moja. Huyo jamaa hafai cheo chochote cha uongozi kwenye nchi yetu. Anaweza kuwa raia kama raia wengine. Period.
 
Tupe tofauti yake!
KIUMRI -- ni ule ukomo wa utumishi wa kiongozi fulani kwa kuzingatia miaka ya umri wake kisheria.
KIAWAMU -- kukoma utumishi ama utendaji baada ya awamu ama muhula wa utawala kupita, kujiuzulu, kuondolewa madarakani au sababu nyingineyo kama kushindwa kutekeleza majukumu yake ya utawala kwa mujibu wa sheria, nk.
 
Niko nje ya Mada kidogo, Shein amekuwa addressed kama Makamo wa Rais mstaafu na Rais mstaafu wa Zanzibar hilo sio shida

Je linapokuja swala la stahiki zake kama mstaafu atapewa zote kama ambavyo ametambulishwa ama kuna moja itaaachwa?
Makamu wa Rais siyo makamo.
 
KIUMRI -- ni ule ukomo wa utumishi wa kiongozi fulani kwa kuzingatia miaka umri wake kisheria.
KIAWAMU -- kukoma utumishi ama utendaji baada ya awamu ama muhula wa utawala kupita, kujiuzulu, kuondolewa madarakani au sababu nyingineyo kama kushindwa kutekeleza majukumu yake ya utawala kwa mujibu wa sheria, nk.
Kwahiyo Majaliwa ni waziri mkuu mstaafu?
 
Back
Top Bottom