Je, ni sahihi kuwasalimia watu kwa kusema: “Bwana Yesu Asifiwe” au “Tumsifu Yesu Kristo”?

Katika jamii mbalimbali maneno: “Bwana Yesu asifiwe” au “Tumsifu Yesu Kristo,” yamekuwa yakitumika kama salaam za kawaida - wakati mtu anapowasalimia waliohudhuria sherehe, mkutano, ibada nk.

Kwa ujumla, maneno hayo sio ya kusalimiana. Hayo ni maneno ya kumsifu Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tunapaswa kuyataja tunapomsifu Yesu kwa upendo wake, msamaha wake, uponyaji wake nk.

Jambo wasilolijua wengi ni kwamba Mungu hapendi watu wanaolitaja Jina lake huku wanaishi maisha ya dhambi. Katika 2 Timotheo 2:19 tunaambiwa hivi:
“Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii: Bwana awajua walio wake, na kila mtu alitajae jina la Bwana na auache uovu.”

Aya hii inatufundisha kwamba kila alitajaye Jina la Bwana, anapowasalimu wenzake au anapomsifu Yesu, anapaswa kuwa mbali na dhambi au uovu. Anapaswa kuwa mtu anayeishi maisha matakatifu.

Kwahiyo hatupaswi kulitaja jina la Yesu huku tunaendelea kukumbatia dhambi kwa makusudi. Kufanya hivyo ni kumchukiza Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Katika Mathayo 15:8-9 tunaanbiwa kwamba kuna watu wanaomheshimu Mungu kwa midomo yao lakini mioyo yao iko mbali naye; yaani ni watu wanaoishi dhambini. Watu wa namna hii Mungu anasema wanamuabudu bure. Kwa maneno mengine, wanamtukuza bure au wanamsifu bure.

Kwahiyo ndugu, kama bado unapiga tungi; kama uongo kwako ni kitu cha kawaida; kama unafurahia uzinzi na wizi; kama hujaamua kutubu dhambi na kumfuata Yesu Kristo kwa moyo wote, ni heri uache kuyatumia maneno hayo mpaka moyo wako utakapokuwa safi. Tumia salaam za kawaida tu: "Shkamooni." "Habari za leo." "Hamjambo?" "Kwema?" Vinginevyo unajiweka matatani bure.

Barikiwa sana
 
Sio sahihi kuwa na salamu za kidini, hata asalameko.
 
Umesema Mungu hapendi kutajwa na watenda dhambi, sisi tunamtaja Yesu shida iko wapi!? Au Yesu ndo Mungu?
 
Na mimi nikuulize: kipi kitangulie? Utamke kwanza: "Bwana Yesu asifiwe" halafu ndio uache uovu, au uache kwanza uovu ndio utamke: "Bwana Yesu asifiwe"
Mbona maandishi ya hicho kifungu yapo wazi? Unataka nitunge maandishi yangu?
 
Kwanza fahamu kuwa Biblia imetafsiriwa kutoka kwenye lugha za mwanzo zilizotumika kuandika Biblia: Kiebrania na Kiyunani.
Kwa lugha hizo, uovu ni kutenda dhambi kwa makusudi. Kwa mfano, unajua uzinzi ni dhambi lakini unaendelea tu kuzini. Hapo unafanya sio tu dhambi, bali uovu.
Rudi darasani ukasome uovu unarithiwa na dhambi hairithiwi hivi vitu ni viwili tofauti
 
Back
Top Bottom