Je, ni sahihi kwa majaji kuvaa mawigi ya kikoloni katika zama hizi?

Yale mavazi yana maana zake kiundani...yaani kwa mfano ukishapigwa death sentence pale mahakama kuu...Jaji anavua Yale mavazi na hausiki yeye Personally as Judge fulani...Kifupi mavazi yanamaanisha yupo kwenye kivuli cha sheria anapotoa hukumu na siyo yeye kama yeye.
 
Kama tuachane na kila kitu basi tuanze kuvaa kama wale Bushmen maana huko ndiko asili yetu. Acha kuva suruali, skirt wala chupi. Haya majaji wanavaa hivyo kuonyesha MAMLAKA YAO. Akirudi nyumbani ni yule yule juzi, jana na leo. Akivaa kama afsa wa kawaida kuna kitu kinapungua sana kiutendaji hata kama Rais ameshitakiwa haileti uzito akiwa na nywele kipiripiri chake.
 
Nani kasema tuachane na kila kitu, tuachane na ya hovyo yanyoonyesha ukoloni mamboleo, mamlaka hayaonyeshwi kwa wigi pekee, anaweza akavalishwa hata batiki yenye mshono aina ya kipekee. kuvaa mawigi blonde ya kizungu ni utumwa wa kifikra
 
Naona cultural renaissance kwa Mwanamajumui kijana wa Afrika Traore. Wengi waliandika kwenye Uzi huu kuwa mawigi yale ni kasumba za ukoloni na kuiga kwa kutojitambua (mimicking) kwa watangulizi katika nchi zilizokuwa makoloni ya watawala wa Kiyuropa na hata Waajemi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…