Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Katika mwili wa mwananke kifua ni sehemu nyeti na haipaswi kuonwa na watu wengine zaidi ya mwenye mamlaka tu, yaani Mume.
Lakini tunaona baadhi ya wanawake wakinyonyesha watoto wao hadharani bila kuficha au kusitiri vifua vyao, mfano katika vyombo vya usafiri au sehemu zenye mikusanyiko ya watu.
Ni haki ya mtoto kupatiwa maziwa pale atakapo hitaji, lakini sidhani kama sababu hii ndyo inahalalisha mwanamke kutoa ziwa mahali popote.
Kwa walio na dini au wasio na dini wote wanafahamu kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti na haipaswi kuonekana hovyo.
Je, ni sahihi kunyonyesha mahali popote kwa kisingizio cha kumpa mtoto haki yake?