Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Ikiwa wewe unakula hadharani basi hakuna tatizo kwa mtoto kunyonyeshwa hadharani.

Ikitokea ukatamani ziwa lala mama anaenyonyesha basi una walakini mkubwa.
Kula hadharani sio sawa na kuonyesha sehemu za Siri mbele za watu
 
  • Thanks
Reactions: I M
Kula hadharani sio sawa na kuonyesha sehemu za Siri mbele za watu
Usiri wa sehemu unakuja kutokana na matumizi/kitendo husika.

Ikiwa mama ananyonyesha mtoto hapo ni kulisha mtoto ila ikiwa anayaanika nje pasi na sababu za msingi au kushikwa shikwa na mwanamue basi hapo ni matumizi mabaya ya maungo na yatakuwa maungo ya siri.

Na nina hakika hakuna mwanamke mwenye akili timamu anaanika maziwa yote hadharani akiwa ananyonyesha mtoto sehemu ya halaiki.
 
Sijalalamika ila nimeuliza
Kwa wanawake wa Kiafrika hakuna shida na imekuwa hivyo kwa muda mrefu hata bibi zetu na mama zetu wamekuwa wakifanya hivyo bila shida sema siku hizi kuna watu wamezibeba tamaduni za Ulaya na Amerika na kuziona ndiyo bora hata malezi ya watoto wetu miaka hii limekuwa tatizo kubwa kwa kisingizio cha kulinda haki za watoto sasa watoto wengi wamaharibikiwa na wazazi hawana cha kufanya tena.
 
Usiri wa sehemu unakuja kutokana na matumizi/kitendo husika.

Ikiwa mama ananyonyesha mtoto hapo ni kulisha mtoto ila ikiwa anayaanika nje pasi na sababu za msingi au kushikwa shikwa na mwanamue basi hapo ni matumizi mabaya ya maungo na yatakuwa maungo ya siri.
Usiri wa maumbile haupo kwa matumizi maalum tu.

Kuonyesha sehemu hizo hadharani kwa kisingizio cha mtoto sio sawa, yapo maeneo ambayo anaweza kwenda na kufanya hivyo pasipo kuonekana na watu.
 
Kwa wanawake wa Kiafrika hakuna shida na imekuwa hivyo kwa muda mrefu hata bibi zetu na mama zetu wamekuwa wakifanya hivyo bila shida sema siku hizi kuna watu wamezibeba tamaduni za Ulaya na Amerika na kuziona ndiyo bora hata malezi ya watoto wetu miaka hii limekuwa tatizo kubwa kwa kisingizio cha kulinda haki za watoto sasa watoto wengi wamaharibikiwa na wazazi hawana cha kufanya tena.
Hayo ni mazoea tu, lakini kiuhalisia siyo jambo nzuri na halifai.
 
Ni sahihi kulingana na mazingira.. Labda kwenye gari safari ya Dar - Mbeya. Mtoto lazima ale La sihivyo kilio ..

Pengine labda wawe na kitenge or something cha kumfunika mtoto anaponyonya na sio kuyaachia wazi ..
 
Mtoto akililia nyonyo apewe haraka sana ni haki yake. Mtoto chakula chake ni maziwa. Kuhusu kujisitiri na blah blah zingine hazihusiani. Cha msingi mtoto anayenyonya apate maziwa kutoka kwa mama.
Ni haki yake na ni lazima apewe, lakini ni muhimu Mama kuhakikisha anaficha na kutoruhusu watu wengine kuona sehemu hiyo nyeti.
 
Yaani wakati mtoto ananyonya wewe unapeleka mawazo yako sehemu nyingine kwa ujinga wako tu halafu useme haifai mama kumnyonyesha mwanawe hadharani! Wewe ndiyo utakuwa na tatizo.
 
Yaani wakati mtoto ananyonya wewe unapeleka mawazo yako sehemu nyingine kwa ujinga wako tu halafu useme haifai mama kumnyonyesha mwanawe hadharani! Wewe ndiyo utakuwa na tatizo.
Akili yako ndyo imeishia hapo kwenye mawazo ya ngono tu, mimi hoja yangu ni kujistiri na kutunza heshima zao.
 
Back
Top Bottom