Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Bob Manson sijajua kilichopo katika fikra zako ila labda wewe binafsi unafikiri nini ukiona mtoto akinyonya?
Kama unamfikiria mtoto sidhani kama kuna shida. Ila ukianza kumfikiria mama hapo ndio changamoto na mkanganyiko unatokea!

Wababa wanaojielewa wanaheshimu wadada/wamama wote wenye mimba na watoto wadogo au wachanga.
 
Akili yako ndyo imeishia hapo kwenye mawazo ya ngono tu, mimi hoja yangu ni kujistiri na kutunza heshima zao.
Wewe ndiyo unajua kutunza heshima zao kuliko wao wenyewe? Kwani wakati wakunyonyesha wanalazimishwa? Usijizungushe zungushe wewe acha kuangaika na manyonyo ya hao wanawake wakati wakinyonyesha.
 
Wewe ndiyo unajua kutunza heshima zao kuliko wao wenyewe? Kwani wakati wakunyonyesha wanalazimishwa? Usijizungushe zungushe wewe acha kuangaika na manyonyo ya hao wanawake wakati wakinyonyesha.
Sio sahihi kuonyesha sehemu za siri hadharani kwa kisingizio cha kumpa mtoto chakula.

Huo ndyo msimamo wangu.
 
Mi nikiona mwanamke ananyonyesha hadharani na mimi huwa namuomba ninyonye
 
Si ustaraabu kunyonyesha ukiwa umeyaacha maziwa wazi kabisa mbele za watu. Busara ni kutafuta faragha na kumnyonyesha mtoto na kama mazingira hayaruhusu basi jifunge wakati unanyonyesha.
 
View attachment 3077317

Katika mwili wa mwananke kifua ni sehemu nyeti na haipaswi kuonwa na watu wengine zaidi ya mwenye mamlaka tu, yaani Mume.

Lakini tunaona baadhi ya wanawake wakinyonyesha watoto wao hadharani bila kuficha au kusitiri vifua vyao, mfano katika vyombo vya usafiri au sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

Ni haki ya mtoto kupatiwa maziwa pale atakapo hitaji, lakini sidhani kama sababu hii ndyo inahalalisha mwanamke kutoa ziwa mahali popote.

Kwa walio na dini au wasio na dini wote wanafahamu kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti na haipaswi kuonekana hovyo.

Je, ni sahihi kunyonyesha mahali popote kwa kisingizio cha kumpa mtoto haki yake?

Je, kifua cha mwanamke kina thamani pale ambapo hajazaa na akizaa thamani hiyo inapotea na anaweza kuonyesha kifua chake mahali popote?
Kwangu ni sahihi x 1001 kunyonyesha hadharani. Mtoto ashibe ndo la msingi.
 
Si ustaraabu kunyonyesha ukiwa umeyaacha maziwa wazi kabisa mbele za watu. Busara ni kutafuta faragha na kumnyonyesha mtoto na kama mazingira hayaruhusu basi jifunge wakati unanyonyesha.
Sahihi Mkuu, tatzo kubwa ni kukosa busara na ustaarabu.
 
  • Thanks
Reactions: I M
Back
Top Bottom