Je, ni sahihi kwa soko la Kariakoo kuhamishiwa Ubungo?

Je, ni sahihi kwa soko la Kariakoo kuhamishiwa Ubungo?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Sioni hilo likitokea, Kariakoo ni soko la Afrika mashariki na kati kama sikosei, unalihamisha ili iweje?

Hii tabia yetu ya kuhamisha magoli kila mara ni ukosefu wa ubunifu au shida iko wapi? Boresheni sehemu zingine, fungueni magoli mengine yenye hadhi kubwa yapambane na Kariakoo, mji hautakiwi kuwa centralised lakini Kariakoo ndio center ya biashara kubwa na ndogo.

Pale ubungo kwenye space ya stand ya zamani si wanajenga business hub(center)? Sasa ile space ndogo inatoshaje kuweka Kariakoo yote.
 
Kuna tetesi nimesikia kwamba Soko kuu la Kariakoo linataka kuhamishiwa Ubungo, kwamba watu badala ya kwemda hadi Kariakoo, badala yake wataishiantu Ubungo. Je, hii imekaaje kaaje, ni mtizamo juu ya hili..
Inawezekana kweli umesikia au unataka kujua, ukweli ni kwamba soko la K'koo halihami isipokuwa Soko jipya litakalojengwa eneo ilipokuwa Stand ya Mabus ubungo, soko litakalokuwa na maduka 2000+ litakuwa likiuza vitu sawa na vile vya Kariakoo na kutakuwa na extra improvement kwa maana ya access ya bidhaa, infrastructures etc....haya nilimsikia Mkuu wa mkoa wa Dsm Amos Makalla aliainisha alipotembelea eneo hilo mapema week hii!

Hayo ndiyo ninayojua na ambayo nimeyasikia!!
 
Sioni hilo likitokea, Kariakoo ni soko la Afrika mashariki na kati kama sikosei, unalihamisha ili iweje?

Hii tabia yetu ya kuhamisha magoli kila mara ni ukosefu wa ubunifu au shida iko wapi? Boresheni sehemu zingine, fungueni magoli mengine...
Ni sawa, ila hata Stendi ya mabasi imehamishiwa Mbezi Luis kwa mafanikio makubwa sana, jiji linapumua sasa angalau.., japo bado kuna wabishi wanakomaa pale shekilango, ila uhamaji umefanikiwa kwa asilimia kubwa
 
Inawezekana kweli umesikia au unataka kujua, ukweli ni kwamba soko la K'koo halihami isipokuwa Soko jipya litakalojengwa eneo ilipokuwa Stand ya Mabus ubungo, soko litakalokuwa na maduka 2000+ litakuwa likiuza vitu sawa na vile vya Kariakoo na kutakuwa na extra improvement kwa maana ya access ya bidhaa, infrastructures etc....haya nilimsikia Mkuu wa mkoa wa Dsm Amos Makalla aliainisha alipotembelea eneo hilo mapema week hii!

Hayo ndiyo ninayojua na ambayo nimeyasikia!!
Sasa si ndio kuhama kwenyewe huko ndugu yangu? Pale Kariakoo hebu hesabu zile frame uone kama zinazidi 2,000, tena wanauza vitu vile vile..., au kwani kuhama maana yake nini?
 
Umefanya vizuri sana kujibu hivi. Huwa nashangaa sana hii tabia ya watu humu kudandia tu mada bila uelewa na kuanza kukimbilia kulaumu tu.
 
Kuna tetesi nimesikia kwamba Soko kuu la Kariakoo linataka kuhamishiwa Ubungo, kwamba watu badala ya kwemda hadi Kariakoo, badala yake wataishiantu Ubungo. Je, hii imekaaje kaaje, ni mtizamo juu ya hili?

Video chini ina maelezo ya ziada

Labda kama wanataka kuua dhana nzima ya ukubwa na diversity ya soko la Kariakoo, Hapo Ubungo ni eneo gani linaweza ku-accommodate Kariakoo? Stend ya zamani?! Au kuna mshenzi anataka kuuwa K’Koo ili watu wapangishe fremu anazojenga Ubungo!
 
Sasa si ndio kuhama kwenyewe huko ndugu yangu? Pale Kariakoo hebu hesabu zile frame uone kama zinazidi 2,000, tena wanauza vitu vile vile..., au kwani kuhama maana yake nini?
Mkuu, kwa common sense yako unaona hilo eneo la Ubungo linatosha maduka yote ya Kariakoo yakihama? Hiyo Kkoo yenyewe haitoshi kwa ukuaji wa biashara na population inayokua. Hapo wanapanua wigo wa mapato na fursa mpya za biashara ndio wanatafuta Ubungo
 
Kuna tetesi nimesikia kwamba Soko kuu la Kariakoo linataka kuhamishiwa Ubungo, kwamba watu badala ya kwemda hadi Kariakoo, badala yake wataishiantu Ubungo. Je, hii imekaaje kaaje, ni mtizamo juu ya hili?

Video chini ina maelezo ya ziada

Mkuu nimekisikiliza kideo mwanzo mwisho sijasikia Kariakoo kuhamishiwa hapo, isipokuwa naona huu ni mradi juu ya mradi.

Ni sawa na kuanzisha stend nyingine ya mabasi ya mikoani Kibaha kuisapoti stend ya Magufuli.

Jinsi jiji linavyoongezeka na population inaongezeka pia.

Kuwa na "Kariakoo" hata nne ni jambo jema na ndiyo maendeleo.
 
Mfumo wa zamani nilielezwa kuwa kariKoo ni soko la masoko mengine,yaani wafanyabiashara wa masoko ya pembeni ndio walitakiwa kuja kuchukua mzigo wa jumla hapo kkoo.
Kilichopo ni tofauti na hata mikoani masoko mengi ni yale ya enzi za ujamaa ,yalijengwa sambamba na ramani rasmi za serikali.
Sasa tumepoteana.
 
Ni sawa, ila hata Stendi ya mabasi imehamishiwa Mbezi Luis kwa mafanikio makubwa sana, jiji linapumua sasa angalau.., japo bado kuna wabishi wanakomaa pale shekilango, ila uhamaji umefanikiwa kwa asilimia kubwa
Wewe unadhani jiji kama Dar kuwa na stand moja kubwa ni sawa? Mimi napita hiyo njia almost daily, stand haijawa overcrowded ni sawa, na wamejitahidi sana kuweka exit na entrance za kutosha kiasi kwamba stand iko okay.

Tatizo lipo kubwa upande wa feeder buses, daladala zimeshajaa mji wa Mbezi haupumui tena, namna gani kutatua hiyo changamoto?

Wenye mamlaka wajenge bus stands kama ya hapo kwa Magu, walau ziwe tatu. Temeke na Tegeta zinatakiwa kuwa na stands kubwa kama ya Mbezi ili kupanua jiji.

Likewise, hutakiwi kuhamisha soko la kariakoo, jenga masoko yenye hadhi ya kariakoo maeneo mengine ili kufanya wateja waamue wapi pa kwenda.
 
Back
Top Bottom