Je, ni sahihi kwa soko la Kariakoo kuhamishiwa Ubungo?

Je, ni sahihi kwa soko la Kariakoo kuhamishiwa Ubungo?

Kuna tetesi nimesikia kwamba Soko kuu la Kariakoo linataka kuhamishiwa Ubungo, kwamba watu badala ya kwemda hadi Kariakoo, badala yake wataishiantu Ubungo. Je, hii imekaaje kaaje, ni mtizamo juu ya hili?

Video chini ina maelezo ya ziada


Haliamishwi bana labda kama Walamba asali washalambishwa mzigo.

Huo mradi hapo Ubungo ulikuwa ni wa ku modernize biashara ya Kariakoo tu. Watakaotaka kuhamia watahamia hapo Ubungo ila ilichukua muda sana hadi watu wakaona kama uzushi.

Hilo soko la Ubungo ni mkataba wa miaka 30 baina ya serikali na mwekezaji wa kichina. Atauza vyumba vya biashara hapo katika kila floor na kutengeneza business hub baina ya china suppliers na Tanzania business people. Hii itaondoa ulazima wa Kwenda China direct maana suppliers mnaanza nao pale pale.
 
Kariakoo ni kubwa sana ukilinganisha na pale ubungo ilipokuepo stand ya mkoa
Ndio wasogeze waitoe nje ya mji kabisa Ila kutanua mji na huko watakapoipeleka. Pale ubungo jam itajaa mno muda si mrefu. Hata magari yanayoshusha na kupakia mizogo patakuwa pafinyu mno.labda wawekemo maofisi halafu ma godowns wajengee nje. Kule mteja aonyeshwe sampo tu
 
Wewe unadhani jiji kama Dar kuwa na stand moja kubwa ni sawa? Mimi napita hiyo njia almost daily, stand haijawa overcrowded ni sawa, na wamejitahidi sana kuweka exit na entrance za kutosha kiasi kwamba stand iko okay.

Tatizo lipo kubwa upande wa feeder buses, daladala zimeshajaa mji wa Mbezi haupumui tena, namna gani kutatua hiyo changamoto?

Wenye mamlaka wajenge bus stands kama ya hapo kwa Magu, walau ziwe tatu. Temeke na Tegeta zinatakiwa kuwa na stands kubwa kama ya Mbezi ili kupanua jiji.

Likewise, hutakiwi kuhamisha soko la kariakoo, jenga masoko yenye hadhi ya kariakoo maeneo mengine ili kufanya wateja waamue wapi pa kwenda.
Hahahah, nimecheka sana, maana unani-adress kana kwamba mimi ndio nimeshika mpini wa maamuzi.., 😂😂😂
 
Ndio wasogeze waitoe nje ya mji kabisa Ila kutanua mji na huko watakapoipeleka. Pale ubungo jam itajaa mno muda si mrefu. Hata magari yanayoshusha na kupakia mizogo patakuwa pafinyu mno.labda wawekemo maofisi halafu ma godowns wajengee nje. Kule mteja aonyeshwe sampo tu
Pale urafiki opposite tu kuna magodown ya kufa mtu, ni kama kijiji kizima cha magodown, nenda ukatembelee uone
 
Kila manispaa ya Dar (Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo, na Kigamboni) iwe na soko la hadhi ya Kariakoo. At least that will reduce the magnitude of the problem.
Sawa, ngoja tuanze na Ubungo kwanza..
 
Na tena ingefaa each ocation kuwe specific ya bidhaa za aina fulani tu ili watu specific ndo wafike eneo hio kupunguza jam. mfano Vingunguti kuwe ni masuala ya building materials tu etc....
Wazo zuri, sio kulundika kila kitu location moja na kusababisha Chaos, mtu akiomba leseni ya biashara eneo flani la kimkakati kwa bidhaa ambayo sio ya soko hiko, anyimwe!
 
Dar inafaa kuwa na masoko kama Kariakoo 3 katika different locations
Exactly [emoji1666] [emoji1666] huwa nawaambia watu kila siku huwezi ku centralize business kwenye jiji lenye watu zaidi ya 5milion na insufficient transport infrastructures and other facilities... Imagine hizo bilioni 250 zingetawanywa into 4 centers (Ubungo, Temeke, Mbagala etc) kwanza ungekuwa umesogeza huduma kwa watu na pia kuounguza msongamano katikati ya jiji.
 
Kila manispaa ya Dar (Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo, na Kigamboni) iwe na soko la hadhi ya Kariakoo. At least that will reduce the magnitude of the problem.
Kwani Kariakoo miaka ya 2000 ilikuwaje na leo ikoje?

Sababu ya ukuaji wake ni nini?
 
Back
Top Bottom