Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Tz yetu mlaji halindwi kwa sheria ya aina yoyote, by mlagi namaanisha mtumia huduma wa mwisho.

A random tuesday nimeenda na dogo kula jioni samakisamaki ya mlimani, sijakaa vizuri kuna mkaka mdogo mdogo akatufata, sorry akinadada, mimi ni content nini nini wa hapa naomba niwapige picha, Nilijibu tu NO! bila kumtazama usoni. Mi sijaja kula bata nimekuja kula chakula tu na kuondoka picha za nini tena? Sasa bora hata hapo tuliulizwa…..


Nchi yetu kuna uholela wa hali ya juu sana katika kila nyanja. Only pesa yako itakusaidia kuchagua maeneo ya kwenda yenye privacy kupunguza hizi kadhia japo si garantii.
 
Wadanganyika mmezidi UKONDOO,haki haiombwi.

Pelekeni mhakamani hao wajinga wenye hela ila hawana akili na maarifa.Mkikaza hao matajiri uchwara wataanza kufanya vitu kiprofessional.

Nchi hii wanaume kwa wanawake ni walalamishi mno bila kuchukua hatua za kisheria.

Amkeni sasa mambo ya kutegemea kila kitu serikali iwasimamie huo ni umasikini.

Infact hii nchi kuna hela nyingi za madai ya kesi kiasi kwamba kila uchwao mtu unaweza kuwa unafungua kesi mbalimbali kujikusanyia utajiri kwa fidia kedekede utakazolipwa🀝
 
Mtafute mmoja au wawili tu wafungulie kesi mahakamani adabu itafata mkondo wake.

Mkiendelea kulalamika mtaendelea hivyohivyo mpaka muingie kaburini chukueni hatua.


Serikali inamambo mengi ya kufanya haiwezi kuhangaika na vitu vidogo kama hivyo wakati sheria zipo wazi kama mtu anahisi kavunjiwa haki basi akaidai.

πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒWatanzania amkeni tatizo mmezoeshwa kimayai mayai kuishi kwa hisaniπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.Haki haiombwi inadaiwa!!!
 
Sijui kwanini watu wanapata uvivu au labda hawajazoea maisha ya kwenda mahakmaniπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kuna watu nadhani wananotion kuwa mahakamani wanaenda wahalifu🀣🀣🀣🀣au wengine wanahisi huko siko mahali pazuri au ni nyara ya serikaliπŸ€—

Wengine mpaka wanaingia utu uzima hawajawahi kwenda mahakamani kusikiliza kesiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

πŸ“ŒπŸ“ŒHuko mashuleni walimu badala ya kila mwaka kupeleka wanafunzi huko maporini au beach ni bora waangale namna ya kuwa wanawapeleka kwenye hizi taasisi angalau wawe na abc.
 
ungeliwa kizazi
 
Huku mtaani kwetu kuna raia wanatulia viunga vya mahakama, kama mtu ni muoga muoga wakujieleza wao wako tayari kununua kesi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mfano hii picha hawa wote wanatakiwa wadai fidia ila kwasababu ya ung'ombe wao wametulia tu.

Mkiwahenyesha hawa wamiliki uchwara wa hizi bar wataanza kujitambua na kuweka legal adviser ili kupunguza kesi zisizo na msingi.

Shida hii nchi kila mtu aliyefeli maisha anaisi kufanya biashara ndo kimbilio.Professionalism hakuna kabisa.

πŸ“ŒPoor Africa,poor Tz!!!
 
Kuna ulikumbukeni sana katika hilo nyakati hizi unaweza kuingia mgahawani kula Lunch mara gafla unajikuta kwenye mtandao wa kijamii bila hata kujua umepigwa picha wakati gani.
Muwe watata hata kidogo taani mmekuwa makondoo sana😬😬😬😬
 
Ukiingia mahali maana yake umekubaliana na Masharti yake.
Tuwe tunasoma Sheria za hayo maeneeo kwanza.

Na kama hawana hizo sheria pia,imekula kwao,unaweza kupiga mpunga mrefu.

Nawatakia Maandalizi mema ya Valentine Day

NB: Kesho kuanzia asubuhi nitakuwa Off hivyo nitaanzia Malaika Beach,then nitasogea Kunduchi Beach na usiku nitaumalizia Club Element,kwa yeyote atakayekua free na atakua maeneo hayo namkaribisha,PM ipo wazi hadi saa sita mchana ya leo
 
kwa uhalisia kwenye sherehe inatakiwa mwenye sherehe amkanye MC haruhusiwi sambaza Video za tukio husika, wapiga picha binafsi hawaruhusiwi.
Privacy, yeye achukue pesa yake arekodi alete Flash
Yaani unalipa mchango alafu bado unaenda kurushwa huko mitandaoni.

Hao maMC uchwara kama wanataka kufanya promo kazi zao waigize kama wafanyavyo wasanii kwenye music videos hakuna shortcut kwenye biashara.

Huu ujinga wa kitanzania mimi siuwezi ntawawashia moto na varangati balaa yaani watatamani aridhi ipasuke wakajifiche.

πŸ“ŒπŸ“ŒUmasikini na kujiendekeza kumefanya watu wafanye mambo kiholelaholela.
 
Maeneo gani wanasheria za kupiga watu picha???

Hivyo vijihela mnashikashika visiwafanye mkawa vipofu.
 
Binamu yangu mmoja ni Kanali, alichukua memory card ya kamera ya mpigapicha wa MC na kuondoka nayo na kumwambia ni marufuki kupiga picha au kuchukua video kwenye eneo la jeshi bila kibali maalumu.
Hiyo ilikuwa kwenye harusi pale "Golf Club".
SAFI SANAπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

πŸ“ŒπŸ“ŒNi muhimu wajinga wajinga wakaelekezwa kwa vitendo!!!
 
Huku mtaani kwetu kuna raia wanatulia viunga vya mahakama, kama mtu ni muoga muoga wakujieleza wao wako tayari kununua kesi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ni shida unakuta mtu kila siku yupo kijiweni badala hata baadhi ya free days awe anaenda kusikiliza kesi na kujijengea confidence ila maskini wa Tanzania utayakuta yapo radhi siku nzima yanatokwa mishipa ya kichwa kubishania simba na yanga.

πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒUjinga wa raia wa hii nchi upo beyond normal levelπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Mambo mengine mnakuza tu ukiona hatutaki kupigwa picha usiende
Huna akili,bila watu kuenda hivyo vinywaji watawauzia nani.

Kutokufata sheria ndio kunasababisha ufunguaji wa kiholela wa vigrosari/vijibaa mitaani.Hili nalo ni uvunjifu wa sheria za mipango miji.

Nchi hii uvunjifu wa sheria ni mkubwa sana na kuna mijitu tangu izaliwe hawajui kufata sheriaπŸ₯±
 
Tembea uone bloangu,usiishie kitambaa cheupe tu
Hizo sheria zipo available kiasi kwamba zimebandikwa kila meza au kuna bango kubwa lipo mlangoni limeorodhesha hizo sheria.

Maana huwezi kunipiga picha au kuchukua video alafu nikikuuliza unitolee kikaratasi mfukoni cha sheria zenu za kiwaki.

πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒJe hizo sheria mtu anaonyeshwa akiwa sober ili mkianza ujinga na ushamba wenu wa kurekodi msilete sintofahamu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…