Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 25,258
- 48,589
Sijawai kukutana na iyo kadhaa ila for sure nitaua mtu kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angekupiga parachute na kukupakia mkongoImagine huyo afande jirani yangu angeona picha mitandaoni niko bar nakunywa pombe na mkewe ingekuwaje?!
Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Kumeibuka Wimbi Kubwa La Wamiliki kuchapisha Picha Au Video Za Wateja Wao Katika Mitandao ya Kijamii Hali Ambayo Kwa Namna Moja Sio Nzuri Kwa Baadhi Ya Wateja.
Unaweza Kwenda Kwenye Baadhi ya Kumbi za Starehe Kipindi Ukipata Kinywaji Iadara Ya masoko Na Habari Wao hufanya Kazi Za Kurekodi Video Kwa Ajili ya Promotion .
Kwa Jicho La Marketing Strategy ni Nzuri Kwa Night Club hizo Kwani huongeza engagement Kwa Wateja Wao Na Kufikia Wateja Wengi Zaidi
Lakini Kwa uwanda Mwingine Huwa inashusha Heshima Na Hadhi hasa Pale unapojikuta Katika Mitandao ya Kijamii Bila ya Kuwa Na Idhini Mtaalam
Katika Hatua Nyingine Masters Of Ceremony Nao Wamekuwa Wakichapisha Picha Au Video Kipindi Cha Harusi Jambo Ambalo Sio Zuri Hasa Pale Ambapo Hakuna Ridhaa Kutoka Upande Wa Mteja
Watu Wengi Sana Wamekuwa Wakikuta Katika Mitandao ya Kijamii Jambo Ambalo Linatatiza Kuchanganya Katika Midhania Isiyo Sahihi
Kuna Mambo Ambayo Yanatakuwa Yafanyike Kuhakikisha kunakuwepo Na Usawa Katika ya Pande Mbili Ili kupunguza Migongano kati ya Wateja Na Wamiliki Wa Kumbi za Sherehe Au MC Katika Kazi Zao
Kisheria, wamiliki wa night club wanapaswa kuwa waangalifu wanapohusisha picha au video za wateja wao kwenye mitandao ya kijamii au kwenye matangazo bila idhini yao. Kwa ujumla, kuna kanuni kadhaa zinazopaswa kuzingatiwa:
1.Sheria za Faragha : Katika nchi nyingi, kuna sheria zinazolinda faragha ya watu binafsi. Kuchukua picha au video za mtu bila idhini yake inaweza kuzingatiwa kama uvunjaji wa faragha.
2. Idhini Wamiliki wa mali kama vile night club wanapaswa kupata idhini wazi kutoka kwa wateja kabla ya kuchapisha picha au video zao mtandaoni. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa wateja wanajua na kukubali kuwa picha zao zitashiriki Katika Machapisho ya Mitandao ya Kijamii
3. Matumizi ya Picha za Umma Katika hali fulani, kama vile matukio ya umma ambapo watu wanajulikana kuwa wanachukuliwa picha, sheria zinaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, ni vyema kuzingatia maadili na kuheshimu haki za binafsi.
4.Mkataba wa Huduma Wakati wa kuingia katika night club, kunaweza kuwa na mkataba (kwa mfano, kupitia alama au matangazo) ambao unaweza kueleza jinsi picha na video zitakavyokuwa zikitumiwa. Ni muhimu wamiliki wajue ikiwa hilo linaweza kutumika kisheria.
Katika hali yoyote, ni bora kwa wamiliki wa night club kufuata taratibu za kisheria na maadili ili kulinda haki za wateja wao na kuepuka matatizo ya kisheria.
Soma Pia: Tahadhari kwa MC's wa maharusi bongo
Utaua mtu au mnyama au ndege?Sijawai kukutana na iyo kadhaa ila for sure nitaua mtu kabisa
Pole sana unaenda kunywa au unaenda kupigwa picha?Post muhimu, hii inabidi ipigiwe kelele na ikemewe. Mimi nimekuja kwenye harusi, C umelipwa, kwanini tena utume picha zangu mitandaoni nikiwa nafurahia sherehe, tena bila ruhusa yangu. Kwenye kumbi huko ndio balaa, niko zangu nimelewa labda na Bar maid, au mchepuko una rekodi unatuma instagram. hii ipigwe marufuku.
Nafikiria kuja kuwashtaki hawa wahuni. Yaanbi wanafanya mambo kienyeji tu.
Aise mkuuu mbona Kam nimo hiv
Dah umeshamchoma mzee mweusi hapo yupo na kingasti chake 🤣.....
Umejiiba na mchepuke unashangaa picha zako hizoooPost muhimu, hii inabidi ipigiwe kelele na ikemewe. Mimi nimekuja kwenye harusi, C umelipwa, kwanini tena utume picha zangu mitandaoni nikiwa nafurahia sherehe, tena bila ruhusa yangu. Kwenye kumbi huko ndio balaa, niko zangu nimelewa labda na Bar maid, au mchepuko una rekodi unatuma instagram. hii ipigwe marufuku.
Nafikiria kuja kuwashtaki hawa wahuni. Yaanbi wanafanya mambo kienyeji tu.
Usi jaribu, wenzio walio jichanganya wali ishia kupostiwa na mishumaaWe jimix by yas tu upostiwe nayo
au sio kwako ni fish market 🤣😂Hahahaha sio maeneo yangu hayo mimi, hayo ni maeneo local sana 😂😂
Binamu yangu mmoja ni Kanali, alichukua memory card ya kamera ya mpigapicha wa MC na kuondoka nayo na kumwambia ni marufuki kupiga picha au kuchukua video kwenye eneo la jeshi bila kibali maalumu.MCs wa maharusi naona ndio trend na wanamulika zaidi pale mtu anapofanya vitu vya kijinga hata sababu ni pombe.
Huko kupigwa picha ni kugusa tu, kesho unajikuta ushakua maarufu kama piere Liquidau sio kwako ni fish market 🤣😂
Watu wana ishia kusema boyka wa vikindu ni mchumba tu 🤣😂Huko kupigwa picha ni kugusa tu, kesho unajikuta ushakua maarufu kama piere Liquid
Camera man wanarecord then wanaenda kuedit/kufanya final cut na kukabidhi mzigo kwa wenyewe......kwa uhalisia kwenye sherehe inatakiwa mwenye sherehe amkanye MC haruhusiwi sambaza Video za tukio husika, wapiga picha binafsi hawaruhusiwi.
Privacy, yeye achukue pesa yake arekodi alete Flash
Wenzangu wanakwaya au?Usi jaribu, wenzio walio jichanganya wali ishia kupostiwa na mishumaa
Maboya wenzio😂🤣Wenzangu wanakwaya au?
Fala sana we mkuuMaboya wenzio😂🤣