Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Kumeibuka Wimbi Kubwa La Wamiliki kuchapisha Picha Au Video Za Wateja Wao Katika Mitandao ya Kijamii Hali Ambayo Kwa Namna Moja Sio Nzuri Kwa Baadhi Ya Wateja.

Unaweza Kwenda Kwenye Baadhi ya Kumbi za Starehe Kipindi Ukipata Kinywaji Iadara Ya masoko Na Habari Wao hufanya Kazi Za Kurekodi Video Kwa Ajili ya Promotion .

Kwa Jicho La Marketing Strategy ni Nzuri Kwa Night Club hizo Kwani huongeza engagement Kwa Wateja Wao Na Kufikia Wateja Wengi Zaidi

Lakini Kwa uwanda Mwingine Huwa inashusha Heshima Na Hadhi hasa Pale unapojikuta Katika Mitandao ya Kijamii Bila ya Kuwa Na Idhini Mtaalam

Katika Hatua Nyingine Masters Of Ceremony Nao Wamekuwa Wakichapisha Picha Au Video Kipindi Cha Harusi Jambo Ambalo Sio Zuri Hasa Pale Ambapo Hakuna Ridhaa Kutoka Upande Wa Mteja

Watu Wengi Sana Wamekuwa Wakikuta Katika Mitandao ya Kijamii Jambo Ambalo Linatatiza Kuchanganya Katika Midhania Isiyo Sahihi

Kuna Mambo Ambayo Yanatakuwa Yafanyike Kuhakikisha kunakuwepo Na Usawa Katika ya Pande Mbili Ili kupunguza Migongano kati ya Wateja Na Wamiliki Wa Kumbi za Sherehe Au MC Katika Kazi Zao

Kisheria, wamiliki wa night club wanapaswa kuwa waangalifu wanapohusisha picha au video za wateja wao kwenye mitandao ya kijamii au kwenye matangazo bila idhini yao. Kwa ujumla, kuna kanuni kadhaa zinazopaswa kuzingatiwa:

1.Sheria za Faragha : Katika nchi nyingi, kuna sheria zinazolinda faragha ya watu binafsi. Kuchukua picha au video za mtu bila idhini yake inaweza kuzingatiwa kama uvunjaji wa faragha.

2. Idhini Wamiliki wa mali kama vile night club wanapaswa kupata idhini wazi kutoka kwa wateja kabla ya kuchapisha picha au video zao mtandaoni. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa wateja wanajua na kukubali kuwa picha zao zitashiriki Katika Machapisho ya Mitandao ya Kijamii

3. Matumizi ya Picha za Umma Katika hali fulani, kama vile matukio ya umma ambapo watu wanajulikana kuwa wanachukuliwa picha, sheria zinaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, ni vyema kuzingatia maadili na kuheshimu haki za binafsi.

4.Mkataba wa Huduma Wakati wa kuingia katika night club, kunaweza kuwa na mkataba (kwa mfano, kupitia alama au matangazo) ambao unaweza kueleza jinsi picha na video zitakavyokuwa zikitumiwa. Ni muhimu wamiliki wajue ikiwa hilo linaweza kutumika kisheria.

Katika hali yoyote, ni bora kwa wamiliki wa night club kufuata taratibu za kisheria na maadili ili kulinda haki za wateja wao na kuepuka matatizo ya kisheria.

Soma Pia: Tahadhari kwa MC's wa maharusi bongo

Post muhimu, hii inabidi ipigiwe kelele na ikemewe. Mimi nimekuja kwenye harusi, C umelipwa, kwanini tena utume picha zangu mitandaoni nikiwa nafurahia sherehe, tena bila ruhusa yangu. Kwenye kumbi huko ndio balaa, niko zangu nimelewa labda na Bar maid, au mchepuko una rekodi unatuma instagram. hii ipigwe marufuku.

Nafikiria kuja kuwashtaki hawa wahuni. Yaanbi wanafanya mambo kienyeji tu.
 
Pole sana unaenda kunywa au unaenda kupigwa picha?
 
Mjini kuna club ambazo huwezi ona video wala picha picha
Ila hizo bar sjui club zenu kitambaa cheusi kidimbwi nk mapichapicha mavideo watu wanajipigia tu

Ova
 
Post muhimu, hii inabidi ipigiwe kelele na ikemewe. Mimi nimekuja kwenye harusi, C umelipwa, kwanini tena utume picha zangu mitandaoni nikiwa nafurahia sherehe, tena bila ruhusa yangu. Kwenye kumbi huko ndio balaa, niko zangu nimelewa labda na Bar maid, au mchepuko una rekodi unatuma instagram. hii ipigwe marufuku.

Nafikiria kuja kuwashtaki hawa wahuni. Yaanbi wanafanya mambo kienyeji tu.
Umejiiba na mchepuke unashangaa picha zako hizooo
Tayar ushaletewa kesi ya kujibu 😄

Ova
 
MCs wa maharusi naona ndio trend na wanamulika zaidi pale mtu anapofanya vitu vya kijinga hata sababu ni pombe.
Binamu yangu mmoja ni Kanali, alichukua memory card ya kamera ya mpigapicha wa MC na kuondoka nayo na kumwambia ni marufuki kupiga picha au kuchukua video kwenye eneo la jeshi bila kibali maalumu.
Hiyo ilikuwa kwenye harusi pale "Golf Club".
 
kwa uhalisia kwenye sherehe inatakiwa mwenye sherehe amkanye MC haruhusiwi sambaza Video za tukio husika, wapiga picha binafsi hawaruhusiwi.
Privacy, yeye achukue pesa yake arekodi alete Flash
Camera man wanarecord then wanaenda kuedit/kufanya final cut na kukabidhi mzigo kwa wenyewe......
Vile vipande tata wanabaki navyo kwaajili ya kutupia youtube au kuuza kwa magroup
 
Natuliaga Kwenye Grocery Ya Bibie Shamimu Toto Nzuri La Tanga Naburudikaa Na Value Zangu Twala Zetu Na Kitimoto rosti Safiii
 
Back
Top Bottom