Naomba watalamu wa sheria watujuze kama ni sahihi kikatiba mahakama kuzuia shughuli za chama kwa chama ambacho ni hai kama CDM???
Je kuzuia jambo au mwanachama asijadiliwe, sio kuzuia shughuli za chama?? chama si kina taratiu zake na uongozi wake??? kama mahakama inaona fahari kueneza kundi la wabunge wa mahakama, je ni tiija kwa taifa??
Naomba msaada wa watalaamu tu,wenye akili zao.
Simple:-
1. Vyama vya siasa vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za Bunge;
2. Kwa kuwa sheria za Bunge huanzisha vyama vya siasa, na tunafahamu wazi kabisa kuwa Katiba ya Nchi inaipa mahakama mamlaka ya kutoa haki, ikiwemo kufafanua sheria mbalimbali, basi Mahakama inayo mamlaka na haki ya kusikiliza na kutoa uamuzi dhidi/kuhusu jambo lolote linalohusu chama cha siasa;
3. Mamlaka ya Mahakama yanaweza kutumika ikiwa kama chama cha siasa kinavunja haki za msingi za mwanachama wake, na haki hizo lazima ziwe zinatambuliwa na sheria za nchi, ikiwemo Katiba ya Nchi, sheria za Vyama vya Siasa, n.k;
4. Hivyo basi, ktk msingi niliosema hapo juu, hakuna ubishi kuwa shughuli za vyama vya siasa zinaweza kuamliwa na mahakama kwa namna na kiasi kile ambacho mahakama itaombwa kuamua dhidi ya baadhi (au yote) ya matendo ya chama cha siasa.
5. Mwisho, matendo ovu ya chama cha siasa hayawezi kuachiwa chama chenyewe kushughulika kwayo kwa msingi kuwa chama kinayo Katiba, Kanuni, etc. In any case, Courts are vested with mandate to hear and determine such matters which may appear violative of rules of natural justice, laws of the land.
I humbly submit.