Je ni sahihi mahakama kuzuia shughuli za chama hai?

Je ni sahihi mahakama kuzuia shughuli za chama hai?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,071
Naomba watalamu wa sheria watujuze kama ni sahihi kikatiba mahakama kuzuia shughuli za chama kwa chama ambacho ni hai kama CDM???

Je kuzuia jambo au mwanachama asijadiliwe, sio kuzuia shughuli za chama?? chama si kina taratiu zake na uongozi wake??? kama mahakama inaona fahari kueneza kundi la wabunge wa mahakama, je ni tiija kwa taifa?
 
So haki.Vyama vinataratibu zake ,na vina referee wake ambae ni Msajili wa vyama.
 
Hata mimi nashindwa kuelewa hata kama sina ufahamu sana katika mambo ya sheria. Kwa kufatilia yaliyokuwa yanajili mahakamani hoja mojawapo heti ni madhala yatakayompata Zitto akifukuzwa katika Chama. Je nani kawaambia kuwa agenda ya kikao ni kumfukuza Zitto? Katika Agenda nilizoona ni kujadili utetezi wa Zitto dhidi ya kuhuma zinazomkabili ndani ya chama?
Kwangu hii inatosha kutupilia mbali pingamizi la Zitto
 
So haki.Vyama vinataratibu zake ,na vina referee wake ambae ni Msajili wa vyama.

Mtu aweza onewa au kosewa na mtu binafsi,taasisi,serikali au chama hivyo anaruhusiwa kumburuza mahakamani mtu binafsi,taasisi,serikali au chama pale anapoona kakosewa.

Vyama ni body corporates zaweza shitaki au kushtakiwa pia.Hakuna aliye juu ya sheria vikiwemo vyama kama CHADEMA inaweekana CHADEMA mnajua people`s power hamjui Court power.People`s POWER sio last resort kuna Court POWER.
 
Kwahiyo wanazuia chama kisifanye shughuri zake eti kisa wanaofia hari ya ZZK endapo akifukuzwa? sasa mtu kweli akosee makusudi kabisa alafu eti tuzuie asichukuliwe hatua eti kisa hatma yake,kama alijua hatma yake ni mbaya kwanini aliamua kwenda kinyume na taratibu za chama chake? hizi mahakama zinafanya kazi kwa maagizo ila ipo siku Mungu ni mwema
 
Dah! Hakika wafuasi wa chadema mnaonesha umbumbumbu wa hali ya juu sana. Poleni sana. Mnachanganya kama afanyavyo Lissu
 
sasa mtu kweli akosee makusudi kabisa alafu eti tuzuie asichukuliwe hatua eti kisa hatma yake,kama alijua hatma yake ni mbaya kwanini aliamua kwenda kinyume na taratibu za chama chake?

Mahakama ndio yaweza thibitisha kama alikosea au chama ndicho kilikosea.Lazima ukubali kuwa chama chaweza kosea pia Kwani chama sio Mungu.
 
Chama kina taratibu zake, sasa mahakaman kuzuia taratibu za chama kufayika ni mtihani, wanachama tunaheshimu chama kuliko kitu kingine chochote.
 
Mahakama ndio yaweza thibitisha kama alikosea au chama ndicho kilikosea.Lazima ukubali kuwa chama chaweza kosea pia Kwani chama sio Mungu.
mbona kalugendo hakwenda mahakamani alipovuliwa upadri na papa!? Taasisi uliyoingia kwa hiari maana yake ulikubali kanuni na taratibu zake. Ukikiuka wanakuondoa kwa kanuni na taratibu zilezile..!
 
mbona kalugendo hakwenda mahakamani alipovuliwa upadri na papa!? Taasisi uliyoingia kwa hiari maana yake ulikubali kanuni na taratibu zake. Ukikiuka wanakuondoa kwa kanuni na taratibu zilezile..!

Ndugu umenena,natumia kamchina ningekupa like hapo. Atakayebisha hapo ni mchawi tu.
 
mpaka uamuzi ukafikiwa hayo maswali yako yote yalifikiriwa kwanza! Anyway cdm si chama huru kama unavyodhani vingnevyo kisingekuwa na ubaguz namna hii.
Chama kupitia viongozi wake wasiokuwa makini kinatengeneza migogoro isiyokuwa ya lazima alafu vikao vinaanza kukaa kuijadili! Unadhan gharama za huu up**mbv atalipa nani kama c nyie MNAODHANI ni wanacdm kutembezewa bakuli na ruzuku ya mamilion kuishia kwenye vikao hv visivyokuwa vya lazma? Poor u blind!
 
mbona kalugendo hakwenda mahakamani alipovuliwa upadri na papa!? Taasisi uliyoingia kwa hiari maana yake ulikubali kanuni na taratibu zake. Ukikiuka wanakuondoa kwa kanuni na taratibu zilezile..!

nawe ni dv5 kama bavicha wenzako! Hv unadhan taasis zote zina miiko inayofanana? Ile ya karugendo ni ya kidini na iko organised zaid ya hiyo saccos yenu muitayo cdm
 
hofu yangu ni kwamba mtindo huu ukilelewa na kuendele, huenda chaguzi zijazo tutaona mengi sana. Tulizoea baada ya maamuzi walioumizwa kwenda mahakaman eg Rashid na Kafulila, ila hii hisia tu zimefanyiwa kazi, sijui watakaokosakuchaguliwa urais na ubunge mwakan itakuwaje. Naamini wanasheria watendelela kuchelewesha maamuzi kwa vyama vyote. Mungu apishe mbali hali hii.
 
Kweli sasa nimeelewa kwanini FIFA huwa hawaruhusu mambo yao kuamliwa mahakamani nahisi waliona mbali sana na kujiridhisha mahakama ina mpaka vilaza wanaopindisha maamuzi ya taasisi ili kukwamisha mambo yasiende

Na kwa mtazamo huu msajiri wa vyama apewe mamlaka ya mambo yote ya vyama lakini pia siyo lazima uwe CDM ama CCM, siyo lazima uwe CUF ndo maana ya demokrasia,nenda panapokufaha wewe hata Mwl. Nyerere alisema CCM haikumzaa eti afie mle
 
Naomba watalamu wa sheria watujuze kama ni sahihi kikatiba mahakama kuzuia shughuli za chama kwa chama ambacho ni hai kama CDM???

Je kuzuia jambo au mwanachama asijadiliwe, sio kuzuia shughuli za chama?? chama si kina taratiu zake na uongozi wake??? kama mahakama inaona fahari kueneza kundi la wabunge wa mahakama, je ni tiija kwa taifa??

Naomba msaada wa watalaamu tu,wenye akili zao.

Simple:-

1. Vyama vya siasa vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za Bunge;

2. Kwa kuwa sheria za Bunge huanzisha vyama vya siasa, na tunafahamu wazi kabisa kuwa Katiba ya Nchi inaipa mahakama mamlaka ya kutoa haki, ikiwemo kufafanua sheria mbalimbali, basi Mahakama inayo mamlaka na haki ya kusikiliza na kutoa uamuzi dhidi/kuhusu jambo lolote linalohusu chama cha siasa;

3. Mamlaka ya Mahakama yanaweza kutumika ikiwa kama chama cha siasa kinavunja haki za msingi za mwanachama wake, na haki hizo lazima ziwe zinatambuliwa na sheria za nchi, ikiwemo Katiba ya Nchi, sheria za Vyama vya Siasa, n.k;

4. Hivyo basi, ktk msingi niliosema hapo juu, hakuna ubishi kuwa shughuli za vyama vya siasa zinaweza kuamliwa na mahakama kwa namna na kiasi kile ambacho mahakama itaombwa kuamua dhidi ya baadhi (au yote) ya matendo ya chama cha siasa.

5. Mwisho, matendo ovu ya chama cha siasa hayawezi kuachiwa chama chenyewe kushughulika kwayo kwa msingi kuwa chama kinayo Katiba, Kanuni, etc. In any case, Courts are vested with mandate to hear and determine such matters which may appear violative of rules of natural justice, laws of the land.

I humbly submit.
 
Mtu aweza onewa au kosewa na mtu binafsi,taasisi,serikali au chama hivyo anaruhusiwa kumburuza mahakamani mtu binafsi,taasisi,serikali au chama pale anapoona kakosewa.

Vyama ni body corporates zaweza shitaki au kushtakiwa pia.Hakuna aliye juu ya sheria vikiwemo vyama kama CHADEMA inaweekana CHADEMA mnajua people`s power hamjui Court power.People`s POWER sio last resort kuna Court POWER.

hivi unakumbuka mgogoro wa TFF na wizara!? Kikitaka kutokea nini endapo FIFA ingejiridhisha serikali imeingilia TFF ktk maamuzi na uendeshwaji wa soka?
 
Dah! Hakika wafuasi wa chadema mnaonesha umbumbumbu wa hali ya juu sana. Poleni sana. Mnachanganya kama afanyavyo Lissu

Ungeeleza kinachotakiwa nadhani ungeonekana sio mbumbumbu lakini ulivojibu ndio umekuwa mbumbumbu zaidi
 
mbona kalugendo hakwenda mahakamani alipovuliwa upadri na papa!? Taasisi uliyoingia kwa hiari maana yake ulikubali kanuni na taratibu zake. Ukikiuka wanakuondoa kwa kanuni na taratibu zilezile..!

kanisa katoliki lina mahakama zake wana sheria zao (canon laws) kama kwa waislamu walivyo na islamic laws.Nimepitia KESI za karugendo aliridhika na hukumu ya huko kanisani akijua kuwa yale aliyofanya hayalingani na matakwa na Sheria Za kanisa kama vile Padri Mfukuzwa Slaa alivyoridhika na kutimuliwa upadri kwa kuwa sheria za kanisa haziruhusu padri kuning`inia kwenye vifua vya wanawake kitandani wawe masista au waumini walei kama mushumbusi au Rose Kamili ndio maana hata yeye hakwenda mahakamani.

Zitto kabwe hajaridhika ndio maana kaenda mahakamani
 
Back
Top Bottom