Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Ole Mushi Msando hajaandika kwa niaba ya serikali au chama chochote au kikundi chochote kilicho sajiriwa.
Kuna hoja ya msingi ya Msando kwamba kuna mikataba tuliyo tia sahini ambayo imeweka utaratibu wa jumuiya za kimatifa kuichukulia nchi flani hatua nchi au mtu mmoja anapotuhumiwa mambo ya uhalifu na uvunjanji haki aliotuhumiwa Makonda na serikali ya Tanzania kwa ujumla..

Nijia hizo ndio zinaweka utaratibu rasmi wa kuhakiki kama mtuhumiwa ana hatia na hizo tuhuma au hana hatia.
Kujisemea tu sisi nchi flani tunazo taarifa za uhakika kwamba huyu kafanya au anafanya hivi bila kupitia hizo taratibu sio sahihi, maana hata sasa tunakumbuka Marekani alisema ana taarifa za kuaminika Sadam Hussein anatengeneza silaha za maangamizi.

Kilichotokea sote tunakijua, na baadae wanarudi kusema taarifa hazikuwa sahihi. Nani analipia au anarudisha maisha na malizi za watu zilizo angamia kutokana na taarifa hizo zisizo sahihi ambazo walisema taarifa za uhakika (reliable info/intel)?

Ole Mushi anakubaliana na Marekani kusambaza tuhuma na zuio lile kwenye mitandao kabla ya hizo njia za kidiplomasia anazo taka Msando au Tanzania wafuate. Huu ni unafiki na double standard!
Basi aseme tu Marekani ana haki ya kufanya chochote na sisi watanzania tuna baadhi tu ya haki za kufanya mambo fulani na sio yote.
 
Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P

Mkuu nikumbushe Gigy Money kamalizana vipi na Kigwangala na pia nikumbushie ile crip ya Msando na Gigy pls?
 
Hapa bila kamusi jamaa katoka kapa,umeanza mambo yako
Alichokoza mwenyewe.

Watu tumeandika kwa Kiswahili kwa sababu tunajivunia lugha ya taifa, yeye akaona kika Mtanzania anayeandika Kiswahili hajui Kiingereza.

Kumbe watu wengine wanajua mpaka Esperanto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichokoza mwenyewe.

Watu tumeandika kwa Kiswahili kwa sababu tunajivunia lugha ya taifa, yeye akaona kika Mtanzania anayeandika Kiswahili hajui Kiingereza.

Kumbe watu wengine wanajua mpaka Esperanto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona kaingia mitini pengine nae anamtafuta mtu wa kumsaidia kujibu
 
Kuna watu wamekomenti upupu humu.ukisema Msando ameandika kama nani nami nikuulize maswali haya

1.Zito kabwe huwa anaandika kama nani?
2.Tundu lissu huwa anaandika kama nani?

3.na wengine huwa wanaandika kama nani?

Vile walivyowamini wandishi waliyoandika mabaya juu ya rais wetu na viongozi wengine ndivyo wanavyotakiwa kumwamni na Mr Msando katika hoja zake kama kweli hawana double standards
 
Unapoandika barua popote, uko huru kumcopy yoyote, ila pia kuna baadhi waliocopiwa kuisoma barua ndefu vile kwa lugha ile ni issue!.
P
Kwa hyo unataka tuwafundishe watoto kuwa loyal kwa viongozi maana ndio tafsir ya uzalendo awamu hii,yeyote anayekosoa maaamuzi ya serikali kupitia viongozi kutoka ccm sio mzalendo,huu utakua ni ujinga wa hali ya juu sana.Yaani awamu hawataki watu wapende taifa bali viongozi hata wakifanya mambo ya kipuuzi tuwapigie makofi.
 
Mwanahabari Huru,
Umeandika vizuri mno. Msando ameharibu badala ya kujenga. Kiki za kitoto zimemuweka kwenye kundi la wasio na weledi wa kidiplomasia.
 
Nimemsikiliza MUSIBA leo.akijinasibu kwamba amekamata waraka wa siri yaani alichokifanya ni jinai kabisa.kwamba mbowe anatafuta soln kwa watu wote yeye ndo kwanzaaaa anachimba handaki.tena kwa uongo.kesho unakutana nae kwenye corridor za usalama inashangaza sana hii
Ukishakuwa Ccm sifa kuu ni kujitoa ufahamu. Ccm inaendeshwa kwa ujanja ujanja sana na ushaidi ni uchaguzi ukifika wanaweka sera pembeni na wanaanza kutumia mbinu chafu sasa wameingia kwenye rada za Marekani.

Unanua ndege, unajenga reli halafu unateka na kuua watu kwa sababu za madalaka, unajenga chuki unafunga watu.

Bora nikose vyote lakini niwe na uhuru wa kuishi sio mtu kukatisha uhai wangu kisa tunapishana mawazo

Hapana Ccm inatosha sasa tafuteni watu makini kuongoza nchi au achieni nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nembo lakini contents zitasomwa ubalozini Shehe. Ndo mana juzi wale wapuuzi wa ccm pale DODOMA wakaacha kujadili hoja za Zzto wakajadili karatasi iliyotumika kuandikia hizo contents. Leo wewe unasema ameandika kama mtu binafsi.mbona ZZTO Kaenda kama mtu binafsi lakini mnataka Lumia akirudi?
Kwani kuna nembo ya serikali kwenye barua yake?

Chadema mnatuaibisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msando ana haki kama raia huru kutoa maoni yake....ila hiyo adress 😄
Barua inaweza kupokelewa Kimanzichana....kwenye kijiwe cha American Embassy....msomaji akawa 20%
 
Back
Top Bottom