Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimba wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.​
Haina shida kama wanaliombea taifa
 
Kwa hiyo tumuache aendelee kuchezea wimbo wa taifa kanisani kwake?
Usiandike tuache,andika niache, usifanye na wengine waingie kwenye kitu ambacho haukijui ,kutokujua kwako hakufanyi kila mtu asiwe na ufahamu wa wapi na kwanini wimbo wa Taifa unaimbwa .
 
Sasa ndio atumie wimbo wa taifa kwenye mapambio kanisani? Huoni kwamba anajichonganisha na serikali?
 
Wewe ni mjinga ,na mpumbavu sana ..asa wimbo akiimba Kuna shida Gani.. hakuna neno zaidi linalokufaaa zaidi ya kukuita mpumbavu usiyejitambua.
Anachezea wimbo wa taifa kwa kuutumia kwenye mapambio kanisani. Kama angekuwa na nia nzuri angeuimba kistaha tofauti na alivyotanya.
 
Sasa ndio atumie wimbo wa taifa kwenye mapambio kanisani? Huoni kwamba anajichonganisha na serikali?
Serikali aijaona kosa lake ni wewe ndio unafikiri kakosea ,sasa ni ngumu kukuelewesha kwasababu unachuki na huyo unaye mwita mwamposa na waumini wake.
 
Wewe jamaa Mwamposa alikuchapia Manzi yako nini mbona mishipa imekutoka sana kwa kumsagia kunguni?
Au ni Dingi yako wa kambo na hujapenda anavyomfaidi Bi mdashi?
Maana Sio kawaida kwa wanaume tunaohustle kusagiana viroboto kihivyo!
😁😁
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimba wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.
Hata wewe unaweza kuimba wimbo wa Taifa. Cha muhimu ni heshima kwa wimbo wa Taifa. Heshima kwa wimbo wa Taifa ni kusimamia name kuimba kwa utulivu au kufanya kama mtu anayesali. Hilo tu. Imba wimbo wa Taifa lakini usiuimbe kwa dharau au kwa kutoonyesha heshima kwa wimbo huo.
 
Asante sana mkuu. Wewe ndiye umechambua vizuri hili jambo. Mwamposa alidharau wimbo wa taifa kwa kuutumia kama pambio kanisani huku wafuasi wake wakipiga ngoma na kucheza.

Hii ni dharau kubwa sana kwa wimbo wa taifa. Rais Samia anapaswa amchukulie hatua za kisheria na kinidhamu huyu jamaa.
 
Wala siyo Rais Samia. Wazee wa nyaraka za Taifa na Idara ya maadhimisho ya kitaifa wanatosha.
 
Sasa wewe unatofauti gani na mwamposa mbona ni kama wewe ndio umekosa akili kabisa.Unawaitaje misukule watu waliozaliwa na baba na mama kama wewe au pengine unatofauti gani na wao
 
National Anthem is sung under three or 4 conditiin
1. National events
2. When the president adress the nation
3. When presidents host felow presidents
 
Mambo mengi ninakuunga mkono, ila hili naona umechemsha. Kuikmba wimbo wa Taifa ni part of Patriotism, itakuwaje ni kufuru? Labda zile sheria za Nyerere? Wakati ule hata ukishika bendera ya Taifa unawekwa ndani
Hii ilikuwa inanishangaza, halafu hapo ukienda mtumbani unakutana na leso, tisheti na hata bendera halisi ya marekani. Yaani ulikuwa upuuzi wa kijinga sana.
 
National Anthem is sung under three or 4 conditiin
1. National events
2. When the president adress the nation
3. When presidents host felow presidents
Ulilishwa tango poli. Kanisani Katoliki hua tunaimba mbona pia. Hapo bado mashuleni siku za paredi.
 
Back
Top Bottom